Rais Samia, Ondoa RC Tabora na DC Nzega, Hawajitambui

Rais Samia, Ondoa RC Tabora na DC Nzega, Hawajitambui

Yule mkuu wa chuo alionyesha utovu wa nidhamu wa Hali ya juu sana Tena mbele ya halaiki.
Sijajua alipewaje kuwa mkuu wa chuo kwa nidhamu ile
 
Nawashauri waende na hapo Nzega DC wakamsweke ndani DED!

Hiyo Halmashauri inadaiwa na wastaafu wa toka 2019,mwajiri hapeleki michango PSSSF wanapata mafao pungufu.
 
Attachments

  • Screenshot_20250216-182754_1.jpg
    Screenshot_20250216-182754_1.jpg
    363.2 KB · Views: 1
  • images (2) (1).jpeg
    images (2) (1).jpeg
    44.3 KB · Views: 1
Mleta mada hujui mkuu wa mkoa na wilaya ni akina nani

Hao kwanza ni viongozi wawakilishi wa Raisi kwenye maeneo yao Ni maamiri jeshi wa maeneo yao ndio maana hupigiwa saluti na vyombo vya ulinzi na usalama
Wao ndio viongozi wakuu wa kusimamia taasisi za serikali katika maeneo yao

Kuajiriwa Chuo kikuu cha Dar hakumfanyi yeye kuwa juu ya mkuu wa mkoa au wilaya yuko chini yao kama alivyo chini ya Raisi
Kama ambavyo mkuu wa UDSM yuko chini ya Raisi

Tafsiri mbaya kabisa uliyoitoa, ambayo haipo mahali popote kwenye katiba ya nchi.

Hakuna mahali popote ambapo katiba inasema kuwa RC ni mwakilishi wa Rais, au DC ni mwakilishi wa Rais, au Mtendaji wa Kijiji au Kata ni wawakilishi wa Rais. Hao watu katiba na sheria, vinataja kuwa ni wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama. Kama kuna mahali ambapo kuna matukio yanayotishia usalama, wanaingia bila kizuizi.

Siyo kila anayepigiwa salute maana yake ni mwakilishi wa Rais.

Kwa tafsiri yako mbovu, basi wafanyakazi wote ambao wapo kwenye eneo fulani, wanatakiwa kuripoti kwa RC au DC. Jambo ambalo siyo la kweli. Ujinga huo uliwahi kufanywa hata na RC na RCO wa Morogoro dhidi ya mkurugenzi wa kampuni moja pale Morogoro, Rais Magufuli aliamua kuwatimua kazi.

Narudia tena, chuo hicho ni sehemu ya UDSM, japo mamlaka za mahali walipo zina haki ya kujua au kupewa taarifa ya mambo yanayogusa mamlaka zao, lakini mamlaka hizo siyo mamlaka za kinidhamu za uongozi wa taasisi hiyo.

RC na DC kuamua kumweka lockup na kuagiza kuwa mkuu huyo afukuzwe, ni ujinga tu huyo DC na RC. DC na RC wana haki ya kuyafikisha malalamiko yako kwa mamlaka ya UDSM, nayo itapima na kuona kama tuhuma dhidi yake zinakiuka masharti ya ajira yake, na kisha watachukua hatua kulingana na kosa lake, kama lipo.
 
Tuliza makalio hakuna unachojua, umeandika upupu. Huelewi ht RC ni nani. RC yuko kwa niaba ya Rais ktk eneo lake la utawala. Tuambie mipaka ya Rais? Anahitaji pongezi kubwa sana amani ingevunjika eneo lile ungeenda wewe? Ur empty headed

You are completely mind crippled without any knowledge about the matter.

MNaokoteza habari za mitaani unaketa hapa. Someni, mtaendelea kuishi katika ujinga wa namna hii mpaka lini?

Leta kifungu kwenye katiba kinachotamka kuwa RC ni mwakilishi wa Rais.

Huko mitaani, wapo watu wanawadanganya wajinga:

Utasikia
RC ni mwakilishi wa Rais
DC ni mwakilishi wa Rais
Waziri mwakilishi wa Rais
VEO mwakilishi wa Rais
WEO mwakilishi wa Rais

Kikatiba, hizo kauli zote ni uwongo. Katiba inatamka kuwa Baraza la Mawaziri ni chombo cha ushauri kwa Rais.
Hawa wateulewengine wote, katiba inatamka kuwa anawateua kumsaidia Rais kutimiza wajibu wake. Hii siyo kwa maRC na maDC pekee bali hata wakuu wa taasisi mbalimbali. Na wanapomsaidia Rais kutimiza wajibu wake, ni muhimu sana kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, mipaka ya mamlaka yao na mamlaka ya taasisi nyingine. Kinyume cha hapo, ni ulimbukeni, na unatakiwa kufukuzwa au kupumzishwa.
 
Hujaelewa, hicho chuo cha madini kipo eneo lao la kazi means Kiko Tabora. Fikiria kukitokea uvunjifu wa amani na hao wachimbaji wadogo wadogo wataita FFU wa UDSM?

Hujaelewa hoja iliyopo. Chuo kipo kwenye eneo la kiutawala la RC na DC. Na hao wawili ni wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama. Kwenye masuala ya usalama, ndio wahusika wakuu.

Lakini unatakiwa ujiulize, huyo mkuu wa chuo kushindwa kujibu swali, alikuwa anahatarisha usalama gani, kiasi kwamba asipowekwa ndani angesababisha maafa gani?

Wapo wanaosema kuwa mkuu huyo wa chuo alishindwa kujibu maswali ya mkuu wa mkoa kwa sababu alikuwa amelewa. Kama ni kweli alikuwa amelewa, tena muda wa kazi, ni kosa. Lakini mamlaka ya kumwajibisha kwa kosa hilo siyo RC au DC, na adhabu yake siyo kuwekwa lockup!!
Kama ni watu kuingia kuchimba madini ndani ya leseni ya chuo, kuna mamlaka nyingine pia inahusika, Tume ya madini. Tume ya madini ndiyo yenye mamlaka ya kusimamia sekta ya madini, na ndiyo yenye uwezo wa kumhoji mmiliki wa leseni ambaye ni UDSM, kama kuna ukiukaji wowote ya masharti ya leseni. Kama kuna uvamizi, na kunahitajika nguvu ya kuwaondoa wavamizi, ni mwenye leseni (ambaye ni chuo) au Tume ya madini ndio wanaowajibika kuomba nguvu za dola ili kuwaondoa kwa nguvu wavamizi.

Kama hukuzingatia hayo, na mwenye leseni hajalalamika, utakuwa na uhakika gani kuwa wanaochimba ni wavamizi? Je, UDSM, Tume ya Madini au Wizara ya Madini, waliwapelekea malalamiko RC na DC kuwa leseni yao imevamiwa au kuna uchimbaji haramu unaendekea kwenye leseni hiyo ya chuo?
 
Upo sahihi. Kumuweka mtu ndani kama kumkomoa ni ulimbukeni. Pale walitakiwa wamuweke ndani na kumfungulia kesi ya uhujumu uchumi kwa kufanya uchimbaji eneo la serikali.
 
Mleta mada hujui mkuu wa mkoa na wilaya ni akina nani

Hao kwanza ni viongozi wawakilishi wa Raisi kwenye maeneo yao Ni maamiri jeshi wa maeneo yao ndio maana hupigiwa saluti na vyombo vya ulinzi na usalama
Wao ndio viongozi wakuu wa kusimamia taasisi za serikali katika maeneo yao

Kuajiriwa Chuo kikuu cha Dar hakumfanyi yeye kuwa juu ya mkuu wa mkoa au wilaya yuko chini yao kama alivyo chini ya Raisi
Kama ambavyo mkuu wa UDSM yuko chini ya Raisi
Hii ni democratic country hayo mambo ya kikoloni yaliyorithiwa ni ya kufutilia mbali.

Nchi inatakiwa iendeshe kwa misingi ya sheria,taratibu na kanuni.Mkuu wa mkoa ni nani labda acheni kujipa umuhimu hapa duniani tena kwenye nchi maskini viongozi wetu wanahitajika kuwa wanyenyekevu kuliko kutanua mabavu.Hii sio nchi ya kijeshi.

Machawa mkae mtambue dunia imebadilika na hakuna nafasi kwa watu wasiowastaarabu.
 
Hujaelewa hoja iliyopo. Chuo kipo kwenye eneo la kiutawala la RC na DC. Na hao wawili ni wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama. Kwenye masuala ya usalama, ndio wahusika wakuu.

Lakini unatakiwa ujiulize, huyo mkuu wa chuo kushindwa kujibu swali, alikuwa anahatarisha usalama gani, kiasi kwamba asipowekwa ndani angesababisha maafa gani?

Wapo wanaosema kuwa mkuu huyo wa chuo alishindwa kujibu maswali ya mkuu wa mkoa kwa sababu alikuwa amelewa. Kama ni kweli alikuwa amelewa, tena muda wa kazi, ni kosa. Lakini mamlaka ya kumwajibisha kwa kosa hilo siyo RC au DC, na adhabu yake siyo kuwekwa lockup!!
Kama ni watu kuingia kuchimba madini ndani ya leseni ya chuo, kuna mamlaka nyingine pia inahusika, Tume ya madini. Tume ya madini ndiyo yenye mamlaka ya kusimamia sekta ya madini, na ndiyo yenye uwezo wa kumhoji mmiliki wa leseni ambaye ni UDSM, kama kuna ukiukaji wowote ya masharti ya leseni. Kama kuna uvamizi, na kunahitajika nguvu ya kuwaondoa wavamizi, ni mwenye leseni (ambaye ni chuo) au Tume ya madini ndio wanaowajibika kuomba nguvu za dola ili kuwaondoa kwa nguvu wavamizi.

Kama hukuzingatia hayo, na mwenye leseni hajalalamika, utakuwa na uhakika gani kuwa wanaochimba ni wavamizi? Je, UDSM, Tume ya Madini au Wizara ya Madini, waliwapelekea malalamiko RC na DC kuwa leseni yao imevamiwa au kuna uchimbaji haramu unaendekea kwenye leseni hiyo ya chuo?
Machawa na kupe wako empty headed😅😅😅😅

Watu kabla ya kupewa uongozi wawe wanapewa hata shortcourse ya miezi mitatu ya UONGOZI.Tunatia aibu huko duniani,tunaoneoana hatujielewi na kuna matumizi makubwa ya mabavu katika hii nchi.
 
Wewe ndio limbukeni na mbumbumbu wa utawala. Yani mkuu wa wilaya aache kuhoji taasisi yeyote ya serikali iliyopo katika wilaya yake hivi una akili timamu kweli wewe? Unajua majukumu ya mkuu wa wilaya kikatiba.?
Wakahojiane OFISINI.Hizi drama mbele ya kamera hazina afya.Ofisi ndio mahali pekee pa kujadiliana mkishindwana mnalimana barua.Huo ndio utaratibu.Hizi DRAMA za uongozi hazina afya acheni maigizo wananchi wanataka maendeleo sio MATAMASHA ya kutoana nishai.

📌📌📌Acheni kutetea uhuni.
 
Yule mkuu wa chuo alionyesha utovu wa nidhamu wa Hali ya juu sana Tena mbele ya halaiki.
Sijajua alipewaje kuwa mkuu wa chuo kwa nidhamu ile
Ndio muanze kufata miongozo ya kiuongozi.Mtaendelea kudhalilishana mpaka lini vyeo vyenyewe leo upo kesho haupo.Kuna siku mtahitajiana kwanini muishi kwa mabavu na mabifu.

Vyeo ni dhamani,viongozi wajifunze kujishusha kuna siku hata huyo Dc au RC WANANAWEZA KUWA ORDINARY CITIZEN MTAA UNAHITAJI UNYENYEKEVU HAKUNA WAKUMLETEA MABAVU HUKO.
 
Unakuwa kiongoz halafu huwaheshimu viongozi wa juu yako Sasa ww unakuwa kiongoz au takataka ndo maana tunapata mashaka aliteuliwaje mtu mwenye kibuli namna Ile kuwa mkuu wa chuo
 
Unakuwa kiongoz halafu huwaheshimu viongozi wa juu yako Sasa ww unakuwa kiongoz au takataka ndo maana tunapata mashaka aliteuliwaje mtu mwenye kibuli namna Ile kuwa mkuu wa chuo
Nyumbani ili familia iwe na utii na adabu inabidi baba, mama na watu wazima wengine wawe mfano bora kwa kila jambo.Tofauti na hapo watoto watakuwa viburi na watukutu.Adabu,utii na heshima vinaanzia juu kwenda chini.

Ni ngumu sana maji kupanda mlima.Huku Afrika/Mavumbini viongozi wanataka kuheshimiwa bila wao kujiheshima na ndio maana kila siku tupo sehemu moja hatusongi mbele.
 
Back
Top Bottom