Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Mh Rais Mama Samia nakusalimu kwa jina la JMT.
Naomba kukupongeza na kukushukuru namna unavyopigania kuinua UTALII kupitia ROYAL TOUR.Ni wazi tena pasipo shaka kwamba ROYAL TOUR inakwenda kusaidia kuongeza idadi ya watalii Tanzania.Hili ni jambo jema linastahili pongezi za dhadi kwakuwa idadi ya WATALII ikiongezeka maana yake fedha za kigeni zitaongezeka mara dufu,ajira zitaongezeka na kipato cha mwananchi mmoja mmoja kitaongezeka.
Baada ya jitihada zako binafsi na serekali yako,naomba kwa moyo wa dhati kukufahamisha hali ya kifedha katika hifadhi zetu ni mbaya sana.Hifadhi zetu zipo shughuli nyingi zinazohitaji fedha kama ujenzi wa madaraja,ukarabati wa barabara ambazo zinatakiwa kufanyiwa matengenezo mara kwa mara.Ununuzi wa Magari na mitambo,ununuzi wa spare parts,posho za maaskari kwaajili ya shughuli za ulinzi na nk.
Mambo yote yanahitaji fedha bahati mbaya kupitia Waziri wa fedha kipindi cha Rais Magufuli Bunge lilipitisha sheria ya kuchukua mapato yote ya taasisi za umma hasa TAWA,TANAPA & NCAA.Kinachotokea sana taasisi hizi zinatakiwa kuomba fedha kwaajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo HAZINA.Mara nyingi fedha zinazoombwa zinaletwa kidogo sana na wakati mwingine kwa kuchelewa.
Majangili wa wanayamapori wakifahamu kwamba sasa taasisi hizi zipo hoi kifedha maana yake utapatikana mwanya wa kuanza kuwinda wanyama pori wetu kwa speed kubwa na kupelekea wanyama wengi kupungua na wengine kutoweka.Jitihada zako kupitia ROYAL TOUR itakuwa kazi bure kwakuwa hifadhi zetu nyingi zitakuwa na upungufu mkubwa wa wanyamapori.
Kazi ya kulinda MAPORI & HIFADHI za wanyama si lelema,tukifanya makosa ya kukumbatia fedha pale HAZINA mambo mengi yataharibika na Serekali yako italaumiwa kwa kushindwa kulinda maliasili ya taifa.
Naomba kuwasilisha, Dr Ngongo kwasasa Tarangire National Park.