Rais Samia: Polisi angalieni upya taratibu zenu za upelelezi, kuwaweka watu mahabusu muda mrefu ni gharama kwa Serikali

Rais Samia: Polisi angalieni upya taratibu zenu za upelelezi, kuwaweka watu mahabusu muda mrefu ni gharama kwa Serikali

Na wao kwanini wawatake watu wenye division 4 pekee wakati wa division 1 na 2 na 3 wapo wengi?
Wa hizo division wengi wanakuwa wameshachagua kada nyingine, kama ualimu, unesi, udaktari n.k.
 
Ni vyema kabla ya kuhukumu ungesikiliza hotuba yote, huyu John yeye kachomoa kakipande kadogo sana katika hili, Rais kaongea kirefu zaidi, nimemsikiliza mwanzo mwisho, ingia you tube ya tbc kuna hiyo hotuba yote, then utacomment ukiwa full informed
Sisi tuna comment kilichowekwa hapa na sio kingine.
Mambo ya kuwaambia polisi wajiangalie ni upuuzi haswa. Wanatakiwa kukemewa na kuchukuliwa hatua...kesi zipo, malalamiko yapo.

Hakuna rais humo...bellow average
 
Ni lazima tukubali kama 90% ya jeshi letu la police na la ulinzi wakosa elimu, wakosa malezi, wahuni, wavuta bangi na majambazi yaliyojificha ndani ya uniform.
Hata ukiwaona wanavyo behave hata kwenye public huwezi kupingana na hoja yangu.
Utaalamu mwingine walionao polisi ni kunyoa pank kichwani,ndo mambo wanayoyaweza
 
Rais Samia ameliagiza jeshi la polisi kuhakikisha linakamilisha upelelezi kwa haraka na kuwaachia huru watuhumiwa ambao kesi zao hazina mashiko.
Rais amesema hivi sasa idadi ya wafungwa inakaribiana kuwa sawa na idadi ya mahabusu.

Kadhalika Rais Samia amemtaka IGP Sirro kuhakikisha hawatumii mabavu bila tija na tabia ya mahabusu kufia rumande hayatoi picha nzuri kwa jeshi hilo.

Chanzo: TBC

=======

Rais Samia Suluhu Hassan amelitaka Jeshi la Polisi kukaa na wadau wengine kuangalia uwezekano wa kurekebisha Sheria ya kuweka watu mahabusu, akisema kwenye Nchi nyingine mtu hakamatwi mpaka upelelezi utimie

Ameeleza Kesi nyingi zinakwama Mahakamani kutokana na kucheleweshwa kwa upelelezi au kukosekana ushahidi akisema, "Hizi tunaita kesi za kubambikiza"

Amesisitiza, "Kama kesi haina mwelekeo watu watolewe. Kwa kesi ambazo mna uhakika upelelezi utatimia basi uharakishwe"
Suluhisho: Katiba Mpya ambayo itarekebisha sheria na taratibu zote zilizopinda kwa kuwa katiba ndiyo shina la sheria zote.
 
Jeshi la Polisi limejaa wahuni wengi waliokuwa Green Guard, ambao hawana mafunzo, sifa wala weledi kwa kazi nyeti ya upolisi.
Wakati nasoma shule zile njemba zilizokuwa zinashinda mstuni na kushika mikia darasani wengi walikuwa wanasema wataenda japo upolisi. Sijui kama walishaingia huko? may be ndio sababu
 
Back
Top Bottom