Rais Samia: Rais haruhusiwi kukaa mkoa mmoja kwa zaidi ya siku tatu

Rais Samia: Rais haruhusiwi kukaa mkoa mmoja kwa zaidi ya siku tatu

Unajua siku zote Mtu Mbinafsi hutafuta sababu zisizo za msingi ili kuwaaminisha watu kuwa yeye yupo sahihi na hivi ndivyo alivyofanya awamu ya tano.

Huwezi kuniambia walioweka utaratibu walikosea mpka wewe uje useme kuwa popote inawezekana mmh!

Okay Ahsante mama kwa kuturudisha kwenye utaratibu na sheria.

Tutaona mengi ambayo yaliliwa na mwingine
 
Hapo zamani za kale kuna mtawala matata wa Tanzania aliwahi kukaa na kufanya kazi za kiserikali nyumbani kwao kwa zaidi ya miezi kadhaa... Aliwaapisha watendaji wake na kuwapokea wageni nashuhuri kwenye mazingira ya kienyeji enyeji sana kule kwao!
Na wote walijifanya kumkubali...
Alivyoenda zake kuzimu hakuna aliyetaka kufuata nyendo zake ovu!
Hadithi yangu imeishia hapo.
Fundisho: tujenge taasisi imara na si miungu-watu
Ujinga mtupu
 
Na Kuna mwingine alifanyia kazi za nchi yake akiwa nchi za ugenini. Hadi watu wake wakaamua kuweka kumbukumbu za idadi ya Safari zake nje ya nchi.
 
Unajua siku zote Mtu Mbinafsi hutafuta sababu zisizo za msingi ili kuwaaminisha watu kuwa yeye yupo sahihi na hivi ndivyo alivyofanya awamu ya tano.

Huwezi kuniambia walioweka utaratibu walikosea mpka wewe uje useme kuwa popote inawezekana mmh!

Okay Ahsante mama kwa kuturudisha kwenye utaratibu na sheria.

Tutaona mengi ambayo yaliliwa na mwingine
Eti nyumbani kwao pale pale Kijijini kwao pale... Karibu na JJ lodge jamaa alipafanya kuwa Ikulu na kufanyika kazi za kiserikali... Akiwapokea wageni mashuhuri na kuapisha wateule wake... Very pathetic!!
 
Umetenguliwa kiuno, nyonga au madaraka?
hii pcha naona kama inamhusu huyo mwamba alie tenguka[emoji41]
IMG-20210614-WA0014.jpg
 
Mabibi na mabwana mheshimiwa Rais wetu mpendwa mama Samia amepasua mbarika tena leo.

Akiongea na vijana Mwanza, mh. Rais katamka angependa kuendelea kukaa zaidi Mwanza, ila taratibu na sheria hazimruhusu kukaa zaidi ya siku 3 katika mkoa mmoja.

Bila shaka akimaanisha kukaa siku 3 mkoani nje ya ofisi rasmi za magogoni au chamwino.

Hizi sheria au taratibu ni mpya zilizoanza baada ya awamu ya sita kuingia ofisini au ndiyo ilivyo ila ilikuwa kupigana ma-changa ya macho?

Kumbukumbu zingali hai kwani si zamani tulipoaminishwa katika awamu ile kuwa rais anaweza kuweka kambi popote na kazi ikaendelea bila ukomo!

Kama aliyosema mama leo ndiyo ukweli wenyewe basi pongezi sana mama Samia kwa kuzingatia maadili, taratibu na sheria.

Unatudhihirishia kwa vitendo kuwa unauo nia ya dhati ya kuhakikisha kuwa wewe kama tunavyowajibika sote kwa mujibu wa sheria wewe kama rais siyo exceptional.

Hongera sana mama Samia Ku kuzingatia utawala wa sheria kazi inapoendelea!
Wewe unasumbuliwa na ulimbukeni, ungetafuta kwanza sheria inayoipa nguvu kauli yake kuliko kushadadia kiu kisichokuwepo.

Mwulize, kwanini yeye amekaa Dar Es Salaam ambako ni mkoani kwa zaidi ya miezi miwili sasa huku akijua ofisi kuu ya Rais ni Dodoma-Chamwino?

Usipende kurukia kipande cha sentensi kisicho na ushahidi kisha unaanza kukinyambulisha kukidhi matakwa yako.

Weka hapa kifungu cha sheria ama kutoka kwenye katiba, mamlaka ya Rais, Matamko ya Rais nk ambacho kinathibitisha kilichosemwa ni kweli bila hivyo hizo ni siasa tu za kujaribu kumnanga mtu. Mbona JK alikaa miezi minne nje ya nchi huku akiendelea kutea watendaji na kutoa maagizo kama kawaida.

Jimbo la Rais ni Tanzania sio Magogoni au Chamwino hivyo popote anaweza kutekeleza majukumu yake ilimradi hakuna sheria inayovunjwa.
 
Back
Top Bottom