Wewe unasumbuliwa na ulimbukeni, ungetafuta kwanza sheria inayoipa nguvu kauli yake kuliko kushadadia kiu kisichokuwepo.
Mwulize, kwanini yeye amekaa Dar Es Salaam ambako ni mkoani kwa zaidi ya miezi miwili sasa huku akijua ofisi kuu ya Rais ni Dodoma-Chamwino?
Usipende kurukia kipande cha sentensi kisicho na ushahidi kisha unaanza kukinyambulisha kukidhi matakwa yako.
Weka hapa kifungu cha sheria ama kutoka kwenye katiba, mamlaka ya Rais, Matamko ya Rais nk ambacho kinathibitisha kilichosemwa ni kweli bila hivyo hizo ni siasa tu za kujaribu kumnanga mtu. Mbona JK alikaa miezi minne nje ya nchi huku akiendelea kutea watendaji na kutoa maagizo kama kawaida.
Jimbo la Rais ni Tanzania sio Magogoni au Chamwino hivyo popote anaweza kutekeleza majukumu yake ilimradi hakuna sheria inayovunjwa.