Rais Samia: Rais haruhusiwi kukaa mkoa mmoja kwa zaidi ya siku tatu

Unajua siku zote Mtu Mbinafsi hutafuta sababu zisizo za msingi ili kuwaaminisha watu kuwa yeye yupo sahihi na hivi ndivyo alivyofanya awamu ya tano.

Huwezi kuniambia walioweka utaratibu walikosea mpka wewe uje useme kuwa popote inawezekana mmh!

Okay Ahsante mama kwa kuturudisha kwenye utaratibu na sheria.

Tutaona mengi ambayo yaliliwa na mwingine
 
Ujinga mtupu
 
Na Kuna mwingine alifanyia kazi za nchi yake akiwa nchi za ugenini. Hadi watu wake wakaamua kuweka kumbukumbu za idadi ya Safari zake nje ya nchi.
 
Eti nyumbani kwao pale pale Kijijini kwao pale... Karibu na JJ lodge jamaa alipafanya kuwa Ikulu na kufanyika kazi za kiserikali... Akiwapokea wageni mashuhuri na kuapisha wateule wake... Very pathetic!!
 
Wewe unasumbuliwa na ulimbukeni, ungetafuta kwanza sheria inayoipa nguvu kauli yake kuliko kushadadia kiu kisichokuwepo.

Mwulize, kwanini yeye amekaa Dar Es Salaam ambako ni mkoani kwa zaidi ya miezi miwili sasa huku akijua ofisi kuu ya Rais ni Dodoma-Chamwino?

Usipende kurukia kipande cha sentensi kisicho na ushahidi kisha unaanza kukinyambulisha kukidhi matakwa yako.

Weka hapa kifungu cha sheria ama kutoka kwenye katiba, mamlaka ya Rais, Matamko ya Rais nk ambacho kinathibitisha kilichosemwa ni kweli bila hivyo hizo ni siasa tu za kujaribu kumnanga mtu. Mbona JK alikaa miezi minne nje ya nchi huku akiendelea kutea watendaji na kutoa maagizo kama kawaida.

Jimbo la Rais ni Tanzania sio Magogoni au Chamwino hivyo popote anaweza kutekeleza majukumu yake ilimradi hakuna sheria inayovunjwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…