Mabibi na mabwana mheshimiwa Rais wetu mpendwa mama Samia amepasua mbarika tena leo.
Akiongea na vijana Mwanza, mh. Rais katamka angependa kuendelea kukaa zaidi Mwanza, ila taratibu na sheria hazimruhusu kukaa zaidi ya siku 3 katika mkoa mmoja.
Bila shaka akimaanisha kukaa siku 3 mkoani nje ya ofisi rasmi za Magogoni au Chamwino:
Hizi sheria au taratibu ni mpya zilizoanza baada ya awamu ya sita kuingia ofisini au ndiyo ilivyo ila ilikuwa kupigana ma-changa ya macho?
Kumbukumbu zingali hai kwani si zamani tulipoaminishwa katika awamu ile kuwa rais anaweza kuweka kambi popote na kazi ikaendelea bila ukomo!
Kama aliyosema mama leo ndiyo ukweli wenyewe basi pongezi sana mama Samia kwa kuzingatia maadili, taratibu na sheria.
Unatudhihirishia kwa vitendo kuwa unayo nia ya dhati ya kuhakikisha kuwa kama tunavyowajibika sote kwa mujibu wa sheria wewe kama rais siyo exceptional.
Hongera sana mama Samia kwa kuzingatia utawala wa sheria kazi inapoendelea!