Rais Samia, ripoti ya mashirika ya umma inakuja; nashauri fanya hivi utanishukuru

Rais Samia, ripoti ya mashirika ya umma inakuja; nashauri fanya hivi utanishukuru

Sifi Leo

Platinum Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
6,408
Reaction score
12,100
Mh Rais nianze Kwa kukupa pole Kwa uchovu wa majukumu, maana Jana nilikuona kwetu Zanzibari, Leo nmekuona bara pale Arusha na wazee wa kitu ya Arusha.

Mh Rais sijui kesho utakuwa wapi ila napatwa na hisia utakuwa Tabora hata usipo kuwepo stolalamika Mimi na wenzangu tupo hapa tunakula upepo maana utakuwa hakika umechoka sana.

Mh Rais Kwa kuwa natambua utakuwa umechoka nisikuchoshe, Nina ushauri ufatao.

Kwa Kuwa msajili wa hazina mkuu wangu aliyeinua shirika la Nyumba Tanzania, anakarbia kukuletea taarifa ya mashirika ya umma ambayo yanajiendesha Kwa hasara, Ili uweze kutumia mamlaka Yako kuyafuta na kuwafikisha wanapostaili walio pelekea mashirika hayo yajiendeshe Kwa hasara nilikuwa Nina ushauri mmoja tu.

Mh Rais kabla ya KUFUTA mashirika hayo, nashauri uchukue sampo ya mashirika mawili tu uyakabidhi Kwa watu ambao hawatakuwa wateule wako yaani nafasi za ajira zitangazwe Kwa watu walioko nje system waombe kuendesha shirika ilo.

Wafanyiwe usaili kuanzia ngazi ya juu mpak chini alafu wape ofa ya KUWAPA ruzuku Kwa mwaka mmoja uone kama shirika ilo litakuwa kwenye mazingira gani?

NAKUHAKIKISHIA ukifata ushauri huu ipo siku utabinafusisha mashirika yote Kwa private entiti kabisa.

Najua Kuna watu wanakumbuka Uzi wangu nilio utoa hapa wa kuomba Nini nifanye Ili baba yangu mzazi mkuu wa Shirika ambalo halina faida zaidi ya miaka MITATU na Mzee Kila akirudi home anarudi na wine ya mama na kilo Tano za kitomoto wataisi hii njia nmeishauri Ili Mimi mtoto Nile shavu Kwa shirika la Dingi wakati yeye akiwa jera hapana Mimi stoomba hizo post.

Mh Rais nje ya serikali Kuna vichwa vikali mno kuliko hivyo ambavyo umekuwa ukiviteua vyenye vyeti na elimu za kusomea pensheni na sio kuwajibika Kwa umma.jarbu utaacha historia.
 
Moderetor umeniaribia Uzi tafadhal
 
Back
Top Bottom