Rais Samia, safari za nje ziambatane na hotuba zenye mvuto. Hongera Mama wa Barbados, umetikisa kikao

Rais Samia, safari za nje ziambatane na hotuba zenye mvuto. Hongera Mama wa Barbados, umetikisa kikao

Rais siyo mtaalamu wa kila kitu, ukiona hotuba haijakaa sawa wataalamu waliobobea kwenye hilo eneo hawajawa consulted kutoa mitazamo yao au chambuzi zao kuhusu hilo eneo kabla ya kuandaa hotuba......
Kuna maswali ya papo kwa papo ambapo kabla hajaondoka nchini lazima wataalam wamweke shule ingawa naye anatakiwa kuwa na kichwa cha kupokea haraka.
 
Suala la hotuba zisizo na mvuto limekuwa ni tatizo sugu kwa awamu zote nne zilizopita na sasa hii ya tano zimeendelea kusikika, nimeondoa awamu ya Nyerere.

Wakati wa Magufuli hazikujitokeza kabisa kwa kuwa hakusafiri nje ya nchi. Rais Samia ameingia na tabia ya kusafiri nje kwa kujitangaza, kuifungua nchi. Tatizo ni ubora duni wa hotuba zake.

Hatukuhitaji hotuba ya kueleza madhara ya Climate change. Hii ni mikutano ya kuwaambia waharibifu kubeba mzigo. FINITO! COP ni tofauti na jukwaa la Dodoma unaposhangiliwa kwa kila sentensi unayozungumza.

Huyu ndo Samia wa TZ



Huyu ni Mia wa Barbados
CCM wanadai ni hotuba ya karne tumshauri hawe anachukua airbus ya watu 250 wa CCM afu akifika huko anawaweka wakae upande moja ili chochote atachoongea wao kazi yao kushangilia tu. Make wao ilimradi wewe ni Rais hata ukiongea pumba watakushangilia hadi uzimie.
 
Lugha lugha hii ya kigeni tujifunze, ukiwa na vocabulary chache sana inakuwa ngumu kucheza na lugha ya kigeni ukaleta mvuto wa kusikilizwa.
Kweli mkuu, mchawi wa lugha ni kuwa na misamiati ya kutosha kichwani vinginevyo fluency inakosekana, unakuwa unapiga goko....
 
..mimi nadhani kwenye hotuba hutakiwi kutumia misamiati migumu-gumu.

..ukiwasikiliza maraisi kama Obama au Biden hotuba zau huwa zina misamiati ya kawaida ambayo inaeleweka hata na mtu mwenye elimu ya kawaida.

..Maza hakujiandaa kwa hii kazi na ndio maana anaonekana anapwaya.
Haimaanishi kuwa na misamiati migumu, ila ni kuwa na maneno mengi mbadala au tungo mbadala kuongelea hoja au mantiki ile ile.........kwa maana nyingine unacheza na lugha.
 
Wanatofautiana namna ya kupresent, Huyu wa Barbados anaonekana kujiamini na anakemea na kukosoa. Huyu wa kwetu anatumia lugha tuliyozoea watanzania - ya kubembeleza na kuomba (malezi yetu)
Pia tukumbuke kuwa pamoja na kuwa mabadiriko ya tabia nchi yanatuathiri sote, yanatuathiri kwa namna tofauti, Hawa visiwa vyao vinaenda kumezwa na bahari kwa haraka sana ndio maana anatumia lugha kali ya death sentence. Kwetu Zanzibar ikimezwa, watakuja Tanganyika maana yote ni Tanzania
Lingine ni uzoefu wa kuongea kwenye hadhara kubwa kama hii.
Pamoja na yote huyu PM wa Barbados 'ameupiga mwingi'
 
Tatizo lugha Samia anasoma kwenye karatasi, mbarbados anayatoa kwenye ubongo
 
Hotuba nzuri zinasaidia nini wakati watanzania wako hawako wamoja, utawala wa sheria, kuheshimu haki za binadamu kunabakia kwenye vitabu.
 
Haimaanishi kuwa na misamiati migumu, ila ni kuwa na maneno mengi mbadala au tungo mbadala kuongelea hoja au mantiki ile ile.........kwa maana nyingine unacheza na lugha.
..asante. umeiweka vizuri hoja ya bagamoyo.

..nadhani Maza haitumii kabisa lugha ya Kiingereza.

..ukimuangalia wakati anahutubia unamuona anataabika kuhakikisha hakosei matamshi, na gestures ktk hotuba yake.

..waandalizi wake wameandika hotuba ambayo Maza anatakiwa awe conversational, lakini akifika jukwaani anakuwa kama mtu anayesoma na sio anayezungumza / anayehutubia.
 
Hotuba ya Rais wetu ni kama anahutubia BUNGE LA NDUGAI Dodoma...

Content ya hotuba ya Rais wetu 95% ni "out of the context"...

Yaani ni kama vile hawajui lengo na kusudi la mkutano huo ni nini...

Msikilizeni kwa makini. Hotuba yake haina tofauti na ya M/kiti Wa CCM akihutubia wazee wa DSM...!!

Au ni kama vile anaelezea utekelezaji wa ilani ya CCM mbele ya mkutano mkuu wa CCM lakini aikiwa Glasgow - Scotland...!!

Halafu sijui ni kwanini ana muonekano ya kinyonge, kiasi cha kuzungumza kinyonge pia, hajiamini kama vile hakula vizuri kabla ya kwenda ukumbini na hata hashirikishi hadhira inayomsikiliza...!

Tuandaeni viongozi kabla ya kuwapa majukumu makubwa kama hili la URAIS...!!!

HAPA HATUNA KIONGOZI bali tuna RAIS PICHA NA TITLE TU waingereza wanasema CEREMONIAL LEADER/PRESIDENT..!
 
Bora Mama katufikisha hapo... Tuliko toka ni kubaya zaidi!
Oooh yes exactly!

Kwanza huwezi kumlinganisha mama yetu SSH na Waziri Mkuu wa Barbados anaeongoza kainchi kenye jumla ya watu 287,000.😆😆😆
 
Acheni ujinga mnampangia cha kuongea kama nani, enzi zile hazirudi tena kwenu jifunzeni historia. Rais SSH wa viwango vya juu piga kazi. Kazi iendelee
 
Kwa kawaida Rais anapozungumzia masuala yanayohusu jumuiya ya kimataifa anakuwa anazungumza kwa niaba ya sisi Watanzania kwa maana kuwa anaueleza Ulimwengu Tanzania inasema nini katika agenda inayojadiliwa. Ushauri wangu wa dhati kabisa ni kila mikutano hii mikubwa ambayo Rais wetu anategemewa kuzungumza kwa niaba yetu wote basi atumie hazina ya vipaji vyote vya Watanzania kuhusu somo hilo. Draft ya kwanza (zero draft) itokane na jopo la wataalam wa somo husika. (Ni jukumu mojawapo la Idara ya Utumishi kuwa na data bank ya wataalam mbali mbali waliobobea na wenye uzoefu wa taaluma mbali mbali).Wasaidizi wapendwa wa Rais na Rais mwenyewe watumie hiyo draft ya kwanza kuifinyanga hutoba kwa kuqeka lugha rafiki kwa msomaji, Rais wetu kama anavyotaka lakini substance ya jambo analoongelea itokane na wataalam wa kiwango cha juu kabisa. Uzoefu wa kawaida unaonesha hakuna mtaalam mwenye hekima ya wastani ambaye hawezi kuwa radhi kusaidia Rais wake afanye vizuri kwenye masuala ya heri kama haya. Tusitengeneze, kwa mfano, timu ya mpira ya taifa inayokwenda kwenye mashindano ya world cup inayotokana na ligi ya mpira kutoka daraja la tatu! Watanzania lazima tukubali kuwa kutumia uwezo na vipaji vyote tulivyonavyo ndiyo siri ya hao viongozi wenzetu ambao tunaona wanafanya vizuri!
Yote ni saw a kabisa. Lakini kwa kuongezea tu ni;

1. Waelewe lengo la ziara ni nini. Kama Rais anahudhuria mkutano au kongamano, at the first place wahusika watambue linahusu nini ili wamwandalie hotuba inayobeba maudhui ya kusanyiko hili...

Mf. Ukisikiliza hotuba hii ya Rais wetu, kuna eneo kataja Mlima Kilimanjaro lakini binafsi nimeshindwa kuelewa alitaka hadhira ipate picha gani kuhusu Mount Kilimanjaro in relationship to the global climate changes...

2. Ma Rais wetu waachane na hotuba za mfumo "full text" za kusoma mwanzo mwisho NENO KWA NENO, SENTENSI KWA SENTENSI na AYA KWA AYA. Zimepitwa na wakati na zinadumaza akili..

Badala yake awe na hotuba iliyo katika mtindo wa "mifupa" au "skeleton" na nyama unajaza mwenyewe in the process...

Huu ndiyo mtindo Wa hotuba za Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Mwl J. K. Nyerere...

å Aidha mtindo huu wa hotuba ndio unaovutia na kuvuta attention ya hadhira/watazamaji na ni kipimo cha uelewa na ufahamu wa mhutubiaji....

Ni mtindo unaotumiwa/uliotumiwa na watu wa aina ya Tundu Lissu, Mwl. J. K. Nyerere, Nelson Mandela, Martin Luther Jr, Rais wa sasa wa Zambia Hakainde Hichilema nk. Ni mtindo wa hotuba zenye kuvuta hisia na kuhamasisha watu kutenda na kushiriki....

å Aidha, ni kwa sbb ni mtindo unaohitaji watu wenye exposure na uelewa mpana wa past and prevailing current global issues na wanaojisumbua kutafuta maarifa na kujisomea kwa wingi kila wakati...

Nasikitika kusema hili kwa ndugu zangu wa CCM ya leo, kuwa mimi sioni mtu wa kariba hii huko...

Na sababu ni moja tu, wamechoka, wamebweteka, wanadhani wameshafika Kanaani, hawana cha kuwasumbua, akili zao zimelala usingizi wa pono na walishalewa madaraka...

Kilicho mbele yao kwa sasa ni kula na kunywa kujaza Marumbo yao hadi kusaza, baaaasi..

Hiki ndicho kinachomsumbua Rais wetu huyu Samia S. Hassan...

Kuna kila dalili kuwa, amekwenda Scotland kupiga "misele" tu na kutalii. Anadhani kila wakati ni Wa kufanya ROYOL TOUR tu...!!
 
Kwa kawaida Rais anapozungumzia masuala yanayohusu jumuiya ya kimataifa anakuwa anazungumza kwa niaba ya sisi Watanzania kwa maana kuwa anaueleza Ulimwengu Tanzania inasema nini katika agenda inayojadiliwa. Ushauri wangu wa dhati kabisa ni kila mikutano hii mikubwa ambayo Rais wetu anategemewa kuzungumza kwa niaba yetu wote basi atumie hazina ya vipaji vyote vya Watanzania kuhusu somo hilo.

Draft ya kwanza (zero draft) itokane na jopo la wataalam wa somo husika. (Ni jukumu mojawapo la Idara ya Utumishi kuwa na data bank ya wataalam mbali mbali waliobobea na wenye uzoefu wa taaluma mbali mbali).Wasaidizi wapendwa wa Rais na Rais mwenyewe watumie hiyo draft ya kwanza kuifinyanga hutoba kwa kuqeka lugha rafiki kwa msomaji, Rais wetu kama anavyotaka lakini substance ya jambo analoongelea itokane na wataalam wa kiwango cha juu kabisa.

Uzoefu wa kawaida unaonesha hakuna mtaalam mwenye hekima ya wastani ambaye hawezi kuwa radhi kusaidia Rais wake afanye vizuri kwenye masuala ya heri kama haya. Tusitengeneze, kwa mfano, timu ya mpira ya taifa inayokwenda kwenye mashindano ya world cup inayotokana na ligi ya mpira kutoka daraja la tatu! Watanzania lazima tukubali kuwa kutumia uwezo na vipaji vyote tulivyonavyo ndiyo siri ya hao viongozi wenzetu ambao tunaona wanafanya vizuri!
Mama kazungukwa na wapigaji tu
 
Oooh yes exactly!

Kwanza huwezi kumlinganisha mama yetu SSH na Waziri Mkuu wa Barbados anaeongoza kainchi kenye jumla ya watu 287,000.[emoji38][emoji38][emoji38]
But she's good at platform than our president who leading a millions of people
 
Back
Top Bottom