Rais Samia, safari za nje ziambatane na hotuba zenye mvuto. Hongera Mama wa Barbados, umetikisa kikao

Rais siyo mtaalamu wa kila kitu, ukiona hotuba haijakaa sawa wataalamu waliobobea kwenye hilo eneo hawajawa consulted kutoa mitazamo yao au chambuzi zao kuhusu hilo eneo kabla ya kuandaa hotuba......
Kuna maswali ya papo kwa papo ambapo kabla hajaondoka nchini lazima wataalam wamweke shule ingawa naye anatakiwa kuwa na kichwa cha kupokea haraka.
 
CCM wanadai ni hotuba ya karne tumshauri hawe anachukua airbus ya watu 250 wa CCM afu akifika huko anawaweka wakae upande moja ili chochote atachoongea wao kazi yao kushangilia tu. Make wao ilimradi wewe ni Rais hata ukiongea pumba watakushangilia hadi uzimie.
 
Lugha lugha hii ya kigeni tujifunze, ukiwa na vocabulary chache sana inakuwa ngumu kucheza na lugha ya kigeni ukaleta mvuto wa kusikilizwa.
Kweli mkuu, mchawi wa lugha ni kuwa na misamiati ya kutosha kichwani vinginevyo fluency inakosekana, unakuwa unapiga goko....
 
Haimaanishi kuwa na misamiati migumu, ila ni kuwa na maneno mengi mbadala au tungo mbadala kuongelea hoja au mantiki ile ile.........kwa maana nyingine unacheza na lugha.
 
Wanatofautiana namna ya kupresent, Huyu wa Barbados anaonekana kujiamini na anakemea na kukosoa. Huyu wa kwetu anatumia lugha tuliyozoea watanzania - ya kubembeleza na kuomba (malezi yetu)
Pia tukumbuke kuwa pamoja na kuwa mabadiriko ya tabia nchi yanatuathiri sote, yanatuathiri kwa namna tofauti, Hawa visiwa vyao vinaenda kumezwa na bahari kwa haraka sana ndio maana anatumia lugha kali ya death sentence. Kwetu Zanzibar ikimezwa, watakuja Tanganyika maana yote ni Tanzania
Lingine ni uzoefu wa kuongea kwenye hadhara kubwa kama hii.
Pamoja na yote huyu PM wa Barbados 'ameupiga mwingi'
 
Tatizo lugha Samia anasoma kwenye karatasi, mbarbados anayatoa kwenye ubongo
 
Hotuba nzuri zinasaidia nini wakati watanzania wako hawako wamoja, utawala wa sheria, kuheshimu haki za binadamu kunabakia kwenye vitabu.
 
Haimaanishi kuwa na misamiati migumu, ila ni kuwa na maneno mengi mbadala au tungo mbadala kuongelea hoja au mantiki ile ile.........kwa maana nyingine unacheza na lugha.
..asante. umeiweka vizuri hoja ya bagamoyo.

..nadhani Maza haitumii kabisa lugha ya Kiingereza.

..ukimuangalia wakati anahutubia unamuona anataabika kuhakikisha hakosei matamshi, na gestures ktk hotuba yake.

..waandalizi wake wameandika hotuba ambayo Maza anatakiwa awe conversational, lakini akifika jukwaani anakuwa kama mtu anayesoma na sio anayezungumza / anayehutubia.
 
Hotuba ya Rais wetu ni kama anahutubia BUNGE LA NDUGAI Dodoma...

Content ya hotuba ya Rais wetu 95% ni "out of the context"...

Yaani ni kama vile hawajui lengo na kusudi la mkutano huo ni nini...

Msikilizeni kwa makini. Hotuba yake haina tofauti na ya M/kiti Wa CCM akihutubia wazee wa DSM...!!

Au ni kama vile anaelezea utekelezaji wa ilani ya CCM mbele ya mkutano mkuu wa CCM lakini aikiwa Glasgow - Scotland...!!

Halafu sijui ni kwanini ana muonekano ya kinyonge, kiasi cha kuzungumza kinyonge pia, hajiamini kama vile hakula vizuri kabla ya kwenda ukumbini na hata hashirikishi hadhira inayomsikiliza...!

Tuandaeni viongozi kabla ya kuwapa majukumu makubwa kama hili la URAIS...!!!

HAPA HATUNA KIONGOZI bali tuna RAIS PICHA NA TITLE TU waingereza wanasema CEREMONIAL LEADER/PRESIDENT..!
 
Bora Mama katufikisha hapo... Tuliko toka ni kubaya zaidi!
Oooh yes exactly!

Kwanza huwezi kumlinganisha mama yetu SSH na Waziri Mkuu wa Barbados anaeongoza kainchi kenye jumla ya watu 287,000.πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Acheni ujinga mnampangia cha kuongea kama nani, enzi zile hazirudi tena kwenu jifunzeni historia. Rais SSH wa viwango vya juu piga kazi. Kazi iendelee
 
Yote ni saw a kabisa. Lakini kwa kuongezea tu ni;

1. Waelewe lengo la ziara ni nini. Kama Rais anahudhuria mkutano au kongamano, at the first place wahusika watambue linahusu nini ili wamwandalie hotuba inayobeba maudhui ya kusanyiko hili...

Mf. Ukisikiliza hotuba hii ya Rais wetu, kuna eneo kataja Mlima Kilimanjaro lakini binafsi nimeshindwa kuelewa alitaka hadhira ipate picha gani kuhusu Mount Kilimanjaro in relationship to the global climate changes...

2. Ma Rais wetu waachane na hotuba za mfumo "full text" za kusoma mwanzo mwisho NENO KWA NENO, SENTENSI KWA SENTENSI na AYA KWA AYA. Zimepitwa na wakati na zinadumaza akili..

Badala yake awe na hotuba iliyo katika mtindo wa "mifupa" au "skeleton" na nyama unajaza mwenyewe in the process...

Huu ndiyo mtindo Wa hotuba za Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Mwl J. K. Nyerere...

βˆšβ€’ Aidha mtindo huu wa hotuba ndio unaovutia na kuvuta attention ya hadhira/watazamaji na ni kipimo cha uelewa na ufahamu wa mhutubiaji....

Ni mtindo unaotumiwa/uliotumiwa na watu wa aina ya Tundu Lissu, Mwl. J. K. Nyerere, Nelson Mandela, Martin Luther Jr, Rais wa sasa wa Zambia Hakainde Hichilema nk. Ni mtindo wa hotuba zenye kuvuta hisia na kuhamasisha watu kutenda na kushiriki....

βˆšβ€’ Aidha, ni kwa sbb ni mtindo unaohitaji watu wenye exposure na uelewa mpana wa past and prevailing current global issues na wanaojisumbua kutafuta maarifa na kujisomea kwa wingi kila wakati...

Nasikitika kusema hili kwa ndugu zangu wa CCM ya leo, kuwa mimi sioni mtu wa kariba hii huko...

Na sababu ni moja tu, wamechoka, wamebweteka, wanadhani wameshafika Kanaani, hawana cha kuwasumbua, akili zao zimelala usingizi wa pono na walishalewa madaraka...

Kilicho mbele yao kwa sasa ni kula na kunywa kujaza Marumbo yao hadi kusaza, baaaasi..

Hiki ndicho kinachomsumbua Rais wetu huyu Samia S. Hassan...

Kuna kila dalili kuwa, amekwenda Scotland kupiga "misele" tu na kutalii. Anadhani kila wakati ni Wa kufanya ROYOL TOUR tu...!!
 
Mama kazungukwa na wapigaji tu
 
Oooh yes exactly!

Kwanza huwezi kumlinganisha mama yetu SSH na Waziri Mkuu wa Barbados anaeongoza kainchi kenye jumla ya watu 287,000.[emoji38][emoji38][emoji38]
But she's good at platform than our president who leading a millions of people
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…