Rais Samia: Sekta binafsi wakitaka kushirikiana na Serikali wanazungushwa mpaka wanakata tamaa wanaondoka

Rais Samia: Sekta binafsi wakitaka kushirikiana na Serikali wanazungushwa mpaka wanakata tamaa wanaondoka

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Rais Samia akitoa hotuba katika kongamano la kumuenzi Hayati Benjamini Mkapa linalofanyika Zanzibar leo 14/ 7/ 2022 amesema kuwa watu wa sekta binafsi ni muhimu katika kufanikisha kasi ya maendeleo ya taifa letu.

Lakini Serikali imekuwa na uzito katika kuwaamini sekta binafsi, wanapotaka kufanya mashirikiano na Serikali wamekuwa wakizungushwa sana hadi wanakata tamaa na kuondoka, hiyo inakuwa tofauti kwa kuwa Seriakali imekuwa inaimba wimbo wa sekata binafsi lakini kiuhalisia hautendei kazi wimbo huo.

Kumekuwa na misingi ya kutoamini sekta binafsi hali inayochelewesha maendeleo kwani ili kuendana na kasi ya kiuchumi Sekta binafsi haikwepeki, ametoa wito kwa Serikali kuwa na ushirikiano na sekta binafsi.

RAIS SAMIA: SEKTA BINAFSI ZIZINGATIE AFYA NI STAHILI YA UMMA NA SIO BIASHARA
Amesema, “Kwa upande wa Sekta Binafsi natarajia watapokea wito wetu na kutoa ushirikiano na kwamba watazingatia kuwa Afya ni stahili ya Umma na sio biashara, hivyo lazima mzingatie urari kati ya kupata faida kiasi na kuwekeza katika kutoa huduma endelevu za Afya kwa Wananchi na kuwekeza pale kwenye mahitaji makubwa zaidi kwa maslahi ya Umma”

Amesema Serikali imejipambanua wazi kushirikiana na Sekta binafsi kwa tija na kwa mkakati bayana na kwa maslahi mapana ya taifa na anatarajia Sekta Binafsi wataitikia wito wa Kutoa ushirikiano kwa Serikali

Vile vile ametoa wito kwa Sekta hizo kutopoteza lengo kuu la kufikisha huduma bora za afya, kwa wote, popote na kwa gharama inayohimilika
 
Anazungumzia awamu ya 5 au 6 hii ya nchi kufunguka na Royal tour
 
Siku hizi kwenda hospitali bila kuwa na bima ya afya ni sawa na kujipeleka machinjioni.
 
Hili ni Tatizo kubwa sana kwenye nchi hii, wafanyakazi wengi wa serikali wanajiona miungu watu.
 
Mfumo wa kuwapata watumishi wa serikali kuanzia mkuu wa mkoa, wilaya, DED ni wa kizamani sana enzi za ujamaa hivyo una athari kubwa sana hadi kwa ngazi nyingine za chini.
 
Hili ni Tatizo kubwa sana kwenye nchi hii, wafanyakazi wengi wa serikali wanajiona miungu watu.
Yuko sahihi mfano watu wanataka kuleta misaada bure ikifika huju kodi inapigwa kubwa kiasi hiyo jamii maskini lengwa haiwezi komboa huo msaada custom unaishia kuozea custom na kuuzwa kwa bei ya kutupwa

Serikali ina jicho kali isiachie tu maofisa TRA, Mabenki na taasisi za money laundering nk kujiamulia kipi kithibitiwe

Nje ya nchi huko kuna watu wana pesa nyingi kuliko hata bajeti ya nchi wakifa wanarithisha hadi mbwa na paka.Anayebisha aingie google a search richest cat or dog in the world wako kibao!

Sasa mtu mtanzania ikatokea uka lobby kwa mtu kama huyo akaamua kukuletea mabilioni ya midola kwa nini tukwamishane ohh money laundering kwa hiyo ni sawa arithishe paka au mbwa huo utajiri wake?
Mama Samia yuko vizuri kutafuta pesa lakini Private sector na NGO na watu binafsi pia wako vizuri pia

Kama nchi inabidi tusitazamane vibaya .Hasa maofisa wa Serikali waelewe mishahara yao kuwa mikubwa na marupurupu makubwa kunategemea sekta binafsi kujiona miungu watu haiwasaidii.Sekta binafsi ikikaa vizuri wao ndipo watatoka kimaisha na kula raha .Wamuone mwananchi wanayemhudumia kama mwajiri wao.Sio wao kujiona mabosi wake
 
Yuko sahihi mfano watu wanataka kuleta misaada bure ikifika huju kodi inapigwa kubwa kiasi hiyo jamii maskini lengwa haiwezi komboa huo msaada custom unaishia kuozea custom na kuuzwa kwa bei ya kutupwa

Serikali ina jicho kali isiachie tu maofisa TRA, Mabenki na taasisi za money laundering nk kujiamulia kipi kithibitiwe

Nje ya nchi huko kuna watu wana pesa nyingi kuliko hata bajeti ya nchi wakifa wanarithisha hadi mbwa na mpaka.Anayebisha aingie google a search richest cat or dog in the world wako kibao!

Sasa mtu mtanzania ikatokea uka lobby kwa mtu kama huyo akaamua kukuletea mabilioni ya midola kwa nini tukwamishane ohh money laundering kwa hiyo ni sawa arithishe paka au mbwa huo utajiri wake?
Mama Samia yuko vizuri kutafuta pesa lakini Private sector na NGO na watu binafsi pia wako vizuri pia

Kama nchi inabidi tuditazamane vibaya .Hasa maofisa wa Serikali waelewe mishahara yao kuwa mikubwa na marupurupu makubwa kunategemea sekta binafsi kujiona miungu watu haiwasaidii.Sekta binafsi ikikaa vizuri wao ndipo watatoka kimaisha na kula raha .Wamuone mwananchi wanayemhudumia kama mwajiri wao.Sio wao kujiona mabosi wake
Roho mbaya za wafrika Kaka
 
mama Samia aanzie customs mali zote za NGo zilizoshikililiwa muda mrefu sababu walishindwa kulipa ushuru wa forodha ziachiwe wakabidhiwe wahusika kama alivyofanya kwenye taasisi za fedha afanye huko customs sababu wenyewe uwezo wa kulipa hawana ni misaada ya wafadhili wa nje vitaoza bure
 
Back
Top Bottom