Mbna hawapewi km hawa wengine, watoto wa nyerere wenyewe wamesahaulika.Watoto tu wa nyerere ndomana mpaka leo wanakula good time,ndomana hata kufanya kazi hawataki...mpunga wanaingiziwa,matatizo yao wanatatuliwa
Ova
Siyo kucheka n wazo zuri sana hiloWangempa toyota ist isiyokula mafuta pia[emoji23][emoji23][emoji23]
Wanapewa huduma zote waleMbna hawapewi km hawa wengine, watoto wa nyerere wenyewe wamesahaulika.
Nimemjibu mtu kwa muktadha fulani, kwa habari nilizokuwa nazo. Kwa kuanza na ku cover the basic.Inaelekea wewe hukusikia alichosema mama au unataka tu kupotosha kwa makusudi.
Alisema hivi,.... anampa zawadi ya birthday gari ndogo (MB) kwakua lile jingine (V8) walilomnunulia liko juu sana na mzee hua anapata shida kulitumia.....
Sasa kama kuna fursa hiyo hii Zawadi ilikuwa na umuhimu/ulazima gani?.Marais, Makamu Rais na Mawaziri wakuu wastaafu wanachagua magari mapya kila baada ya miaka mitano If I am not mistaken na service wanafanyiwa bure. Na nyumba wanapewa, mpaka mpishi na mtunza bustani wanapewa.
Ni sehemu ya package kustaafu ya viongozi wa kitaifa wastaafu.
Sasa hapa wamefanya kutangaza tu, lakini hawa viongozi wastaafu wote wanachagua magari na wananunuliwa na serikali tangu wanastaafu.
Acha roho ya kichawi mfKwahiyo unalinganisha Tausi na 450m?na akili yako ikaishia hapo?bado tunasafati ndefu Sana hapa Tz,sijui nani katuloga,
Mwanae ni Rais wa Zanzibar na kabla alikuwa waziri kwa miaka kibao huku Bara, kwamba hakuona baba anashindwa kupanda V8? Lakini mzee analipwa robo tatu ya mshahara wake kila mwezi Kama akiona shida kupakia V8 kwanini asinunue Gari?
Hata ukishindwa kuzalisha utasema ccm
Mwinyi kama anapata tabu, je yeye hawezi kununua kwa pesa yake?Sioni umuhimu wa kutolea zawadi maelezo.
Lakini upo uwezekano pia kuwa hizo shuruba anazopata mzee Mwinyi wakati wa wa kupanda na kushuka kwenye hiyo V 8 zoezi mujarabu kwake katika umri mkubwa aliojaliwa ingawa kwa hili mama anaweza kuwa amepata ushauri kwa physiotherapist wa mzee.
Ni matumaini yangu kuwa mzee Mwinyi ambaye anaheshimika sana na watanzania wengi, na Rais Samia, ambaye anabeba matumaini makubwa ya watanzania hawatasongwa sana na mawazo juu ya huu mjadala ulioibuka sababu ya hii birthday gift.
Kwamba mama Samia ataliangalia hili katika mwanga chanya na kurekebisha pale panapostahili bila jazba ambayo inategemewa na baadhi ambao hawakutaka aiongoze Tanzania.
Halafu anatoa sababu za kipuuzi tu! Eti amempa gari dogo kwa sababu anapata tabu kupanda kwenye V8! Na baadae akishindwa kupanda hata hiyo Benz aliyo mnunulia itakuwaje?Huyi mzee ana pensheni kubwa, mroto wake keshampatia urais Zanzibar wanae wengine kawapa ubunge wa east afrika kwa kifupi huyu mama ni bomu linalosubiri mida kulipuka
CCM ni MCHWA! Isingekuwepo ccm, huenda nchi hii ingekuwa mbali sana kimaendeleo.CCM haiwezi kubadilika asilani
Mwinyi kama anapata tabu, je yeye hawezi kununua kwa pesa yake?
Nchi ina maajabu sana hii! Makosa ya 2015 bado yanaendelea tu kututesa kama Taifa! Mama ana miezi miwili tu, lakini ameshaanza kulewa madaraka kwa kasi ya ajabu! Sijui mpaka ifike 2025, itakuwaje!!Mwinyi kama anapata tabu, je yeye hawezi kununua kwa pesa yake?
Ndiyo maana tuna mlaumu sn huyu mama kwa matumizi mabaya ya fedha za ummaMkuu nadhani ni sehemu ya mazoezi yanayomwezesha kuwa fit kwenye huo umri alio nao.
A blessing in disguise so as to speak.
Kwa kweli siwezi jua kama anaweza nunua hiyo gari kwa pesa yake au la, lakini hata hivyo yeye ni mpewa zawadi tu na hivyo sio defendant kwenye hii issue.
Kama kuna mtu wa kulaumiwa hapa ni mama, kwa kujaribu ku rationalize zawadi na hivyo kuwapa wale ambao washatoa visu vyao kwenye ala na kuvinoa dhidi yake, nafasi ya kuli- blow hili suala zima out of proportions kiasi cha hata kuwateka wengine ambao walishaonesha imani kwake.
Amefeli mapema sn kuliko mtu yoyoteNchi ina maajabu sana hii! Makosa ya 2015 bado yanaendelea tu kututesa kama Taifa! Mama ana miezi miwili tu, lakini ameshaanza kulewa madaraka kwa kasi ya ajabu! Sijui mpaka ifike 2025, itakuwaje!!
Ndiyo maana tuna mlaumu sn huyu mama kwa matumizi mabaya ya fedha za umma
Hakika umenena vyema mkuu, Rais akifanya vizuri tumpongeze japo ni wajibu wake na akikosea tumkosoe.Nakubali mkuu.
Viongozi wetu, hasa Rais wanapaswa kuwa sensitive sana kwenye masuala yote yanayohusu fedha za umma.
Lakini kuna wengine pia ambao wanalitumia tu hili tukio la zawadi kama kisingizio cha kumnanga mama yetu bila kuwa na hata chembe ya dhamira njema juu ya matumizi ya fedha za umma.
Najua kuwa wewe si mmoja wa hao.