Pre GE2025 Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini

Pre GE2025 Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Bwawa la Nyerere kulikoni? Si umeme tuliambiwa uko mwingi wa ziada, kuna jambo sijaelewa
 
"Umeme unakatikatika maeneo ya Kaskazini huku lakini Serikali yenu inachukua hatua ya kununua umeme nje maalum kwa Mikoa hii ya Kaskazini ili umeme upatikane masaa 24 muda wote bila kukatikakatika"

"Tuko kwenye hatua za mwisho kusaini mikataba ili tuweze kununua umeme ule uungwe Kanda ya Kaskazini na Wananchi wafaidi na umeme, kwahiyo tutakuwa na umeme wa uhakika, maji ya uhakika kila pahali, Vijiji vyote vina umeme tunakwenda Vitongojo na umeme wa kutosha tunaununua unaingia ili kazi za maendeleo ziendelee"
Shocking news!!!
 
Wakuu Mama ni kama amepewa taarifa Sio wame mislead Sijapenda kabisa, Kwasasa Total Capacity ya Uzalishaji wa Umeme Countywide ni 3040MW against matumizi ambayo hayafiki ata 2500MW kitu ambacho tunaweza Kusema kwa Sasa tuna Surplus

Issue ya Kukatika Kwa umeme sidhani kama Ni scarcity isipokuwa Miundo Mbinu ya Usambazaji na Usafirishaji ndio sio rafiki Ministry of Energy ime take ilo onboard na Kuna Miradi ya Usafirishaji Inafanyika Kuongeza Expansion ya Grid mfano wanajenga Mradi Wa 400KV kutoka Chalinze mpaka dodoma Ili umeme unaotoka Bwawa la Mwalimu Nyerere uwe distributed Vyema.

Mwezi uliopita walifanikiwa Kuunganisha Line za Msongo wa 400KV kutoka isenye Kenya Mpaka Singida Via Arusha Na Kujenga Kituo Kikubwa cha Kupooza umeme Substation Arusha Namuguru (400KV) Kiasi kwamba Muunganiko Huo utasaidia Cross-border trading ya Umeme kati yetu sisi Kenya kupitia (Ketraco) na Ethiopia ambaye Ethiopia ndio giant kwenye Ukanda Huu Muunganiko huo Uko guided na Kitu kinaitwa Eastern African power pool Power(EAPP) chenye wanachama Mataifa 13 to date

Ivo issue ya Kusema sisi tununue umeme hakuna sababu kabisa ya msingi ya Kufanya Ivo unless tupate scarcity kitu ambacho kwa sasa hatuna ujenzi wa Line ya msongo 400Kv chalinze dodoma utasaidia Vituo Vinne Kuwa interconnected vya 400Kv ambacho ni Chalinze, Zuzu pamoja Kituo kikubwa cha Singida na Namguru Arusha Ivo izo infrastructure zikishakuwa Constructed tutakuwa na Usafirishaji mzuri na Kaskazini itaenda Kuwa Stable upande wa Nishati

Mheshimiwa Naibu waziri Mkuu ni zaidi ya Mara Moja Tumesikia Ukisema Kuwa Kwa sasa nchi ina Kiwango cha Ziada(Surplus) upande wa uzalishaji ila tu Changamoto Ni Miundo Mbinu ya Usafirishaji na Usambazaji ambalo ni swala wote tunaelewa kuwa Linarekebishwa kwa Muda na ni swala Progressive hii Policy ya kusema tununue Umeme Kenya au Ethiopia sana sana Ethiopia ila Tupitishie kenya Naona Haijakaa Vizuri kabisa
Wakenya kwa sasa tumewapita Upande wa Capacity ya Grid zetu.
 
Hivi mfano sisi wa Tanzania tukamuomba Elon Musk awe raisi wa taifa letu kwa mkabata maalumu wa miaka 10 wenye kufungu cha kumtoa kama atakiuka,hivi inashindikana?

Atupeleke mchaka mchaka wa miaka 10 akituachia tuwe hatua tatu nyuma ya china.
Tumpe Mpina tu hata kwa mwezi mmoja anaweza, huko kwa EM mbali mno
 

Attachments

  • 20250309_170426.jpg
    20250309_170426.jpg
    223.6 KB · Views: 1
  • 20250309_170434.jpg
    20250309_170434.jpg
    252.9 KB · Views: 1
Unaweza kuwa unaipenda sana mchi yako, ila kila ukimsikiliza huyu bibi lazima kichwa kikuume.

Nadhani ndio maana nchi kaachia kina Wazir Salum na Mchengerwa.

Bor kumekucha.

Siku akimaliza madaraka, 2030 kunaweza kutokea vita kama ile ya Kikwete na Lowassa, ambayo at least Mkapa alotumia Ubabe.

Sasa hivi wapo kina Kikwete hofu juu juu, mpaka watu wanapitishwa kugombea HEY HEY bila taratibu za chama.

Sijui.
 
Tumpe Mpina tu hata kwa mwezi mmoja anaweza, huko kwa EM mbali mno
Hakuna mtanzania anaweza simamia system kama wenzetu wa nje.

Sifa moja inawafanya wenzetu kupiga hatua ni kuwa na mfumo wa kiutendaji unaoendana na uhalisia.

Mtawekewa magari mazuri ya usafiri,chakula ,mtapewa posho, per diem nzuri,na mshahara mzuri. Ila eneo la kazi hakuna kuchekeana na uzembe haufumbiwi macho.

Kimsingi wenzetu wanaweka mifumo na kuwajibika nayo sisi tunaweka mifumo na kuichezea.

Ukimuweka mtu kama Elon Musk hapa ndani ya mwaka hamtaamini hili taifa namna litabadilika na kuwa kitu cha tofauti.
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ipo kwenye hatua za mwisho za kusaini mikataba ya kununua umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini ili Mikoa hiyo ipate umeme wa uhakika na iondokane na adha ya umeme kukatikakatika.
View attachment 3264483
Rais Samia amesema hayo baada ya kufungua mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe kwenye hafla iliyofanyika Mwanga Mkoani Kilimanjaro leo March 09, 2025.

Soma: Rais Samia: Tanzania inayo nafasi ya kuuza umeme nje

Rais Samia amesema "Umeme unakatikatika maeneo ya Kaskazini huku lakini Serikali yenu inachukua hatua ya kununua umeme nje maalum kwa Mikoa hii ya Kaskazini ili umeme upatikane masaa 24 muda wote bila kukatikakatika"

"Tuko kwenye hatua za mwisho kusaini mikataba ili tuweze kununua umeme ule uungwe Kanda ya Kaskazini na Wananchi wafaidi na umeme, kwahiyo tutakuwa na umeme wa uhakika, maji ya uhakika kila pahali, Vijiji vyote vina umeme tunakwenda Vitongojo na umeme wa kutosha tunaununua unaingia ili kazi za maendeleo ziendelee"


Chanzo: Millard Ayo
Pale same upepo mwingi na jua la kutoshwa kwann tusifunge mitambo ya umeme kwa njia ya upepo na jua..?
 
EEeheee...ngoja nikae kimyaaa nisi comment kitu maana....daah basi tu
R.I.P...Magufuli
 
Gharama kupeleka Toka unapozalishwa heri kuchukulia Moi
Kuwa na Grid Ni salama zaidi usisahau Pia Energy ni National security matters Muunganiko na Majirani Ni kitu Kizuri sana kwasbabu kitakupa wide range ya Choice incase pakitokea Blackout ila Pia Kuhakikisha Nchi Iko Connected yote Na Grid ni Swala zuri zaidi na Majirani iwe kama Back Up kwasababu leo tupo salama Kesho ikitokea Vita na Hao Majirani wanaokuuzia Umeme tegemea Kukatiwa Umeme Ili uwe Gizani
 
Hii kauli ni sawa na ile ya mabomba yatatoa maziwa badala ya maji , ana kichwa kizima kweli uyu
 
Sifa moja inawafanya wenzetu kupiga hatua ni kuwa na mfumo wa kiutendaji unaoendana na uhalisia.
Sisi tunaangalia namna mtu anavyofunga kilemba

Au tumuombe Ibrahim Traore
 
Back
Top Bottom