Unakuta mfanyabiashara amechukua mkopo 200M benki, ameweka watu wamkusanyie mahindi semi 10 kutoka Dodoma, Manyara, Arusha, etc.
Semi zimesheheni chakula kuelekea mpakani ghafla unasikia serikali imesimamisha usafirishaji wa vyakula nje ya nchi na hapo gari zipo tayari mpakani.
Jamani, hivi serikali inawajali wafanyabiashara au ndio chanzo cha matatizo na kufilisika kwa wafanyabiashara? Mtu atarejeshaje mkopo kwa utaratibu huu? Kwanini serikali isiwe na utaratibu wa kutoa notisi angalau ya mwezi mmoja kabla ya kisitishwa kwa vibali? Hivi serikali kwanini inatuadhibu hivi na wakati sisi tunafanya biashara halali na leseni tunazo?
Mkulima wa Tanzania naye hana uhakika na soko la mazao yake mara leo bei nzuri kesho bei mbovu. Serikali inamtumia mkulima kwa ajili ya food security tu bila kujali anafaidika vipi na kilimo chake.
Serikali mnafanya unyama mkubwa kwa wafanyabiashara na wakulima acheni unyama huu! Mama Samia tusaidie tafadhali wekeni utaratibu mzuri wa kutoa taarifa kabla la sivyo mnatuumiza mno wafanyabiashara na wakulima!