Rais Samia, Serikali kusimamisha ghafla uuzaji wa chakula nje ya nchi ni unyama dhidi ya wafanyabiashara na wakulima

Majirani si huwa mnajiona wajanja mwaka huu mtakula sukuma week na mtura,mahindi na mchele hatuuzi nje
 
WWe
Well said
 
Kafyeke vichaka upate shamba uweze kulima tuitosheleze nchi acheni kukaa mjini mkilamba lips na kubetua midomo kama wadada nyie vijana njooni Pori tulime.
Kuna maji ya kumwagilia, kituo cha afya na barabara ya kusafirisha pembejeo na mazao??
 
Mimi nataka iwe hivyo na ikiwezekana ikolezwe zaidi wafikiwe wamachinga, wafikiwe wachimbaji wadogo wa madini n.k. ili hasira za watu zisogee Karibu

Kukiitishwa maandamano iwe rahisi kuotikia nchi nzima kwa sababu kila mmoja kaguswa kwenye maslahi yake
 
Kuna maji ya kumwagilia, kituo cha afya na barabara ya kusafirisha pembejeo na mazao??
Ndo shida inapoanzia nyie shambani upelekewe kituo cha afya tangu lini wagonjwa wanalima? HUku bushirombo hakuna irrigation scheme hata moja lkn tunalima mpunga na mavuno ni makubwa kuliko hata hao wa kapunga irrigation so Acha kubweteka kijana.
 
Wauze chakula ndani ya Tanzania
 
Actually, wafanyabiashara ndiyo wameguswa zaidi na hili sababu kiuhalisia wao ndiyo wanafaidika zaidi na hii export trade.

Mfano msimu uliopita mipaka ilifungwa na gunia la mahindi debe sita lilifika hadi 150,000 February 2023!

Je ni wakulima wangapi walikuwa na akiba February na kuuza kwa 25K/debe? Hawapo sababu wengi waliuza June-September 2022 kwa 60K-80K kwa gunia bei ambayo misimu yote wanauzia.

February mazao yanakuwa kwenye maghala ya wafanyabiashara na wakulima wananua huko.

Ili wakulima wanufaike na hii export trade inabidi wao wenyewe wayafikie hayo masoko ya nje labda kupitia vyama vya ushirika tofauti na hapo ni siasa tu.
 
inaitwa government interventions, elimu ni muhimu sana tusipuuzuie kusoma . entreprenuer should be
tolerant
risk bearing etc
 
Hivi huwaonei huruma wananchi bei ya vyakula imepanda? Unaangalia upande wako na majirani zako, je! Kwa watanzania! Nimefurahi sana mama kuzuia kupeleka nje
 
Kafyeke vichaka upate shamba uweze kulima tuitosheleze nchi acheni kukaa mjini mkilamba lips na kubetua midomo kama wadada nyie vijana njooni Pori tulime.

JF kumbe ni pori zuri la kuanzia kulima mwenzetu uko mbali πŸ˜› πŸ˜› πŸ˜›
 
Hivi huwaonei huruma wananchi bei ya vyakula imepanda? Unaangalia upande wako na majirani zako, je! Kwa watanzania! Nimefurahi sana mama kuzuia kupeleka nje
Nazungumzia namna uzuiaji huo unavyofanyika bila taarifa ya muda mrefu ili wafanyabiashara hao wajipange. Umeelewa?
 
Madhara ya kuzuia mahindi kutoka nje ya nchi ni makubwa vijana wanazidi kuongezeka mjini ni hatari sana kila mkulima amegeuka kuwa machinga na boda sijui uchumi tutaujenga vipi ukimzui mfanyabiashara ni nani ataenda kununua hayo mazao maghala ya serikali wananunua mazao bei ya chini sana kuliko mfanyabiashara ni propaganda tu zinaendelea ili kuonekana mfanyabiashara ni mnyonyaji
 
inaitwa government interventions, elimu ni muhimu sana tusipuuzuie kusoma . entreprenuer should be
tolerant
risk bearing etc
Ndugu yangu watanzania wengi ni wajinga ndio maana tunaona sawa tu kutopewa taarifa. Na wewe inaonekana ni mjinga pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…