Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 4,016
- 6,759
SOCIAL DISTANCING
Hakuna asiyejua hii ndo key element ya kupunguza maambukizi ya magonjwa yanayofanana na Corona. Nimeanza na hilo Tangazo hapo juu ili hili suala lieleweke kwa sababu tukiacha matangazo ya uwepowa Corona nchini ambayo yanahusishwa na "Kujenga Mazingira ya kupata misaaa" kutoka huko Duniani; lakini utekelezaji wa protocols za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huu imekuwa ni kama Maigizo tu.
Tukisema tufanye Lockdown sidhani kama litakuwa ni jambo sahihi kutokana na vipato vyetu na hali zetu lakini kuna mengine ambayo yanaweza kufanywa kwa maagizo ya serikali kwani tulishafanya hapo Mwanzo na tuliweza kuendelea na maisha kwa kiasi fulani japo changamoto zilikuwa chache. Mfano wa haya , mpaka sasa tumetangaziwa maambukizi kufikia 400+ waliopimwa so far, achilia mbali kijiji kitakachokuwa mitaani na hakijapimwa which concludes kuwa hali si nzuri.
Licha ya Alerts hizi na taarifa hizi zenye kuhitaji tahadhari kubwa kwani tumesikia pia kuna uhitaji wa mitungi huko Shinyanga Hospital baada yaile ya Bugando kuongezwa lakin bado Serikali imeachia na inaendelea kuachia mikusanyiko isiyo na ulazima ikiwemo Mikutano ya Viongozi kama Mh. Rais wa JMT, Rais wa ZNZ, ziara ziara za mawaziri, Maonesho ya sabasaba. Mengine ni Mikutano ya vyama vya Siasa Vikiongozwa na CCM na Chadema. Haya matukio yameleta mikusanyiko mikubwa isiyofuata dhana ya "social distancing" wala uvaaji wa barakoa wala pia unawaji wa mikono au utumiaji wa vitakasa mikono. Tunashuhudia pia mibanano ya kwenye madaladala hususan ya wale ndugu zetu wa kama Mbagala, vipi wanaokimbiza mwenge nchini na mikusanyiko yake, Lakini pia Hofu yangu NI VIPI USALAMA WA VIONGOZI WETU NYETI KAMA MAMA YETU NA DK MWINYI?
Ajabu sasa ni hili Tamasha lililoandaliwa na Serikali kupitia taasisi ya wizara ya mawasiliano kwa kushirikiana na Msanii Nandy, hapo sikutaja mechi ya Simba na Yanga na mengineyo mengi Ninachojiuliza, Waziri wa afya unasubiri nini kutoa tamko na agizo la kulazimisha kufuata hizi protocols, najiuliza Wizara ya mambo ya ndani kupitia Jeshi la Polisi, Wizara ya usafirishaji kupitia Latra, Wizara ya Utamaduni na Michezo, manispaa na halmashauri mbalimbali, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya kupitia TAMISEMI na taasisi nyingine wenye dhamana na wanaohusika na matukio yanayokusanya watanzania WANASUBIRI NINI. MBONA WAO NAO WANAHUSIKA KATIKA KUKUSANYA WATU NA KUACHA HUU UGONJWA UENEE KWA KASI. Mbona mambo ni kama Mwaka jana na juzi , mbona kama hakuna tofauti na baada ya kupima mapapai?
Kama Tumetangaziwa tatizo lipo basi tuwe serious kuanzia Serikali hasa Wizara ya Afya, taasisi za serikali na zisizo za kiserikali pamoja na sisi wananchi wenyewe. Naweza mimi nikajidistance lakini vipi jamii yetu?
SERIKALI IACHE KURUKARUKA , INABIDI KUENFORCE BAADHI YA POLICIES NOW, ELSE ITAKUWA INAENDELEA KUSHIRIKI KUTUSAMBAZIA GONJWA HILI