Rais Samia: Serikali yenu ni sikivu, tutaangalia njia nzuri tunayoweza kufanya ili kikokotoo kisilete maneno mengi

Rais Samia: Serikali yenu ni sikivu, tutaangalia njia nzuri tunayoweza kufanya ili kikokotoo kisilete maneno mengi

Mbunge anayeendelea na ubunge asilipwe kwa mkupuo, mkupuo uwe kwa wale tu walioshindwa uchaguzi. Hawa wengine waendelee kutunziwa kama inavyofanyika kwa watumishi wa umma.
Hata wanaoishia njiani wasubiri wafike miaka 60
 
Bado jamii nayo na waganyakazi wana shida why do they not have the power to accuse?

Why kila kinachopitishwa hunong'ona chini chini wkt kila idara inayoathirika ina watu wajiitao mawakili wasomi?
 
Akizungumzia kuhusu malalamiko yaliyopo kwenye kikokotoo katika ufunguzi wa Kikao kazi cha Maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi, Oysterbay, leo Septemba 4, 2023, Rais Samia amesema Serikali inafanyia kazi suala hilo na itaangalia njia nzuri ili kuondoa maneno mengi.

"Tupo tunakifanyia kazi na kuona jinsi tutakavyoenda vizuri kwa sababu masuala ya kikokotoo haya si tu matakwa ya Serikali kutaka kuja na kikokotoo, ni hali ya uchumi na hali ya mifuko yenu ilivyo. Ni hali ya mifuko ilivyo. Tukisema kila anayetoka boom lako hilo hapo, boom lako hilo hapo, miaka 2 tu mifuko ile imekauka." Amesema Rais Samia.

Ameongeza, "Tuliweka hivi ili kuweka sustainability ya mfuko, sasa kwa sababu imepigiwa kelele sana sio tu na jeshi la polisi lakini na wengine, tutakwenda kuangalia sababu tunasema siku zote Serikali yenu ni sikivu. Tutakwenda tuangalie njia nzuri tunayoweza kufanya ili kikokotoo kisilete maneno mengi"
Kiukweli suala la pensheni limepitwa na wakati na ni legal pyramid scheme.
 
Tatizo la kikokotoo ni zao la viongozi wabovu, wala rushwa, waoga, na wazandiki wa vyama vya wafanyakazi wakiongozwa na TUCTA baba lao. Police wao walishaona kikokotoo hiki ni kimeo ila hawakuwa na sehem tu ya kusemea kutokana na nature ya kazi yao km ilivyo kwa Jw. Ila hawa wafanyakazi wengine wenye vyama vya wafanyakazi ukiwauliza juu ya kikokotoo utaskia wakisema "hayo ni maoni ya wafanyakazi, walikubali wenyewe na wao kuwasilisha kwa serikali". Ni viongozi wa hovyo hovyo hivi hawapo kuwatetea wafanyakazi bali kutunisha matumbo yao.

Ona sasa jana police wamepata tu nafasi kidogo wakafunguka mbele ya rais na rais katoa neno. Lakini hao viongozi wa vyama vya wafanyakazi ni kujichekesha tu kwenye hafla wanazokaribishwa.
 
Back
Top Bottom