Doctor Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,089
- 2,725
"Mkiambiwa kwamba Mwenyekiti wa CCM na Rais wenu Samia ni mwuaji waambie ni kweli bila hofu. Ninaua Sisimizi wenye nguvu hasi ya Upinzani dhidi ya serikali ya CCM, ninaua Sisimizi waletao umasikini, ninaua Sisimizi wenye mambo hasi ya kuturudisha nyuma kiuchumi, ninaua Sisimizi waletao giza lilinalotanda kwenye uso wa nchi yetu, kweli ninaua sisimizi lakini sijawahi kuua mtu. ” (paraphrased) - - Kauli ya Rais Samia, Songea, Ruvuma, 28 Sep 2024
Tarehe 28 Sep 2024, akiwa mjini Songea, mkoani Ruvuma, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alihutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa CCM na kusema maneno hayo hapo juu.
Tamko lake linakuja siku chache baada ya utekaji, utesaji na mauaji ya kikomandoo ya Mohamed Ally Kibao yaliyotekelezwa na wahusika waliobeba silaha za kijeshi kwa mujibu wa mashuhuda.
Ni tamko linalokuja wakati ambapo, kwa mujibu wa taarifa ya TLS, kuna orodha ya watu wapatao 80 ambao wametoweka na hawajulikani waliko, baadhi wakiwa wamechukuliwa na Wahusika waliojitambulisha kuwa ni mapolisi.
Ni katika mazingira haya Rais Samia ameamua kucheza na "unyumbulifu" wa maana ya neno "muuaji. "
Neno hili linaloweza kumaanisha muuaji wa mtu, muuaji wa Sisimizi, muuaji wa mende, muuaji wa umaskini na kadhalika.
Anatumia utata huu kuwahamisha wasikilizaji kutoka kwenye tuhuma kuu yaani tuhuma kwamba "Rais Samia ni muuaji wa watu wanwoikosoa Ccm na Serikali yake"
Hata hivyo hajafanikiwa. Mazingira tuliyomo leo yanaashiria wazi kuwa Rais Samia ametofautisha maneno "Sisimizi" na "watu" kama mkakati wake wa propaganda dhidi ya wakosaji wa serikali yake.
Ni kama ambavyo maneno "mende" na "watu" yalitofautishwa huko Rwanda miaka ya 1990 katika vurugu za kundi moja dhidi ya kundi jingine (mass violence) ili kufanikisha dhana ya "wao" dhidi "yetu"
Katika kanuni za propaganda mkakati huu unaitwa "dehumanisation".
Rafiki yangu mmoja anasema yafuatayo kuhusu kanuni hii:
"Perpetrators of mass violence often appear to deny the humanity of their victims. Theoretical treatments of this topic suggest such dehumanization facilitates violence by disengaging moral restraints against harming fellow humans"
Hivyo ni sahihi kuhitimisha kuwa Rais Samia alitumia neno Sisimizi kama silaha ya kipropaganda.
Na kwa kweli limebeba maana ambayo inamtia hatiani Rais Samia.
Na likiendelea kutumika katika mtazamo huo linaweza kuleta maafa makubwa sana hapa Tanzania.
Historia inaonyesha kuwa huko Rwanda Wahutu waliwaua Watusi kwa sababu walitumia mkakati wa dehumanisation kuwabatiza Watusi jina baya la MENDE.
Hivyo ikawa rahisi kwa wahutu kutekeleza mauaji ya halaiki ya Watusi kwa kuwa wauaji walijawa na ujasiri wa "HAPA TUKO TUNAUA MENDE TU"
Aidha Waarabu na Wazungu waliokuwa wachuuzi wa biashara ya watumwa weusi hapa Afrika waliwabatiza Wabantu majina mabaya kama vile "nyani", "sokwe," na "nguruwe" na kwa sababu hii ikawa rahisi kwao kuwapiga bei Waafrika hawa katika masoko ya watumwa kwa sababu ya ujasiri kwamba "HAWA NI NYANI TU."
Kwa sababu hizi namwalika Rais Samia na wasaidizi wake kujielekeza kwenye mada ya msingi kwa faida ya Taifa.
Na mada kuu ni hii hapa:
Je, nguvu ya hoja iliyo hasi dhidi ya madudu ya Ccm na Serikali yake inawafanya wakosoaji husika kupoteza hadhi ya utu wao hadi watekwe, wateswe, wasiginwe kama "Sisimizi" na hatimaye kuuliwa na milli yao kuharibiwa kwa kumwagiwa tindikali kama tukio la Mohamed Ally Kibao linavyothibitisha?
Je, kwa mujibu wa katiba ambayo SAMIA aliapa kulinda, ni halali kwa mtu yeyote kueneza itikadi, sera na mipango ya serikali kwa kutumia itikadi ya JAMBIA LA MTUME MOHAMED isemayo kuwa "kila mtu aliye kinyume chetu ni kafiri anayestahili adhabu ya kuchinjwa kwa upanga hadi kufa"?
Na je, kwa nini Samia na wasaidizi wake wanashindwa kuona kwamba sisi Waafrika tulipokubali kuwa na Rais Mwarabu tulikuwa tunajua ukweli kuwa mataifa yote ya kiarabu yanaikataa democracy na kukumbatia autocracy, lakini tukaamua kwamba tumpe, benefit of doubt, kwa kumkabidhi kamba ya urais ili ajinyonge mwenyewe, kama akitaka?
Kwa kukiri kwa mdomo wake kwamba yeye ni muuaji wa Sisimizi wanaomnyima usingizi tayari Rais Samia amekataa urais kwa maneno na matendo yake mwenyewe.
Ameamua kujinyonga mwenyewe kwa kamba hadi kufa!
RIP Samia Suluhu Hassan!
CCM mkimaliza matanga anzeni kuandaa mgombea irais mwingine!
Nakala kwa:
1. Mary Chatanda,
Mwenyekiti UWT Taifa,
Tanzania
(Aione kwenye faili)
2. Dk. Emanuel Nchimbi,
Katibu Mkuu CCM
(Aione kwenye faili)