#COVID19 Rais Samia: Silazimishi watu kupata chanjo, kila mtu ni mkubwa ana akili yake

#COVID19 Rais Samia: Silazimishi watu kupata chanjo, kila mtu ni mkubwa ana akili yake

Niko na mama Samia!
.
Kila mtu na akili zake, wewe kama unataka chanjo peleka takle zako kawatengee wakupige chanjo kimya kimya
Chanjo ni takoni? Ccm ccm ccm, wanaharibu watu akili sana, ona huyu sasa.
 
Kila mtu si mkubwa huku ni kujivua uwajibikaji tu.

Si aseme tu kuwa yuko kwenye kusimamisha uchumi wake kwanza?

Corona ipo na inachukua maisha ya watu maana yake nini? Au ndiyo tunayoiona kutuongezea mzigo wa tozo na kodi zaidi?

Takwimu kama walivyo ainishwa wataalamu ziko wapi?

Aache kutufanya mazwazwa kama Jumbe Brown au zandrano
🤣🤣Mh.Rais ameshauri kitaalamu baada ya kushauriwa na Wataalamu wake....

Kinyume chake mkuu Brazaj amekuja na maneno yasiyo ya "KIPOPOMA" kutusema sisi "mazwazwa"....🤣
 
🤣🤣Mh.Rais ameshauri kitaalamu baada ya kushauriwa na Wataalamu wake....

Kinyume chake mkuu Brazaj amekuja na maneno yasiyo ya "KIPOPOMA" kutusema sisi "mazwazwa"....🤣

'.... amekuja na maneno yasiyo ya "KIPOPOMA" ...'

😀😀😀
 
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa Zinga, Bagamoyo amesema halazimishi watu kupata Chanjo dhidi ya COVID-19 akieleza, "Kila mtu ni mkubwa ana akili yake. Vituo vipo ukijihisi unataka kwenda nenda, ukiona bado hutaki ni wewe na maamuzi yako"

Amesisitiza "Tusidanganyane, COVID-19 ipo na inachukua maisha ya watu wetu. Sikwambii ukichanja hutopata, ukipata haina maumivu makubwa"
Gwajima ww ni msema kwel Mung yu pamoja na ww ,, rest in peace John pombe magufuri
 
Sasa ndugai kwann anataka kumuadhibu gwajima Kama Ni hiari
Kosa lake ni kuenda kinyume na matakwa ya serikali, govt inataka watu wachanjwe alafu wewe upo tofauti hutaki kuchanjwa sawa, na unashawishi watu wasichanjwe kwa maneno ya uongo
 
Tatizo hii chanjo ina magumashi mengi, mabeberu wanatengeneza chaka lao la kupiga hela.....vipi yale matrilioni waliyopewa na mabeberu kuhamasisha chanjo dhidi ya uviko watayatapika, au ndo nitolee hiyo.
 
Kila mtu si mkubwa huku ni kujivua uwajibikaji tu.

Si aseme tu kuwa yuko kwenye kusimamisha uchumi wake kwanza?

Corona ipo na inachukua maisha ya watu maana yake nini? Au ndiyo tunayoiona kutuongezea mzigo wa tozo na kodi zaidi?

Takwimu kama walivyo ainishwa wataalamu ziko wapi?

Aache kutufanya mazwazwa kama Jumbe Brown au zandrano
 
Sasa kusema hulazimishwi ndio nini? Kitu kama kina madhara halafu unakaa kimya na wewe ndio kiongozi hiyo maana yake nini? Wewe ni kiongozi wa aina gani sasa unashindwa kuchumbulia wananchi wako lililo baya na lililo jema na ukawashauri accordingly? Huu ni udhaifu wa hali ya juu!!
Kuongoza watanzania kazi sana.
 
Wabongo bana mlitaka awaambie msichanje kama yule marehemu wenu alivyowaaminisha corona haipo?
 
Alitaka awachape viboko wote wanaokataa na kuwadunga kwa nguvu. Mtanzania bana haridhiki kwa lolote
Aisee kuwaongoza watanzania inahitaji uwe na roho kama ya paka vile.
 
Kuwa basi rais ili ulazimishe watu unachokitaka. Una elements zote za dikteta!
Rais yuko sahihi! Kila mtu ni mtu mzima. Achague aonavyo vyema.
Kama hupendi, kunywa maji endelea na kazi. Kama una mashaka jifungie ndani utakuwa salama!
Yeye ni Rais, anadhamana ya kulinda raia wake, tangu lini mchungaji akaona Simba mbele halafu anawaambia Kondoo kwamba kila mtu aamue kuendelea na Safari au kurudi nyuma? Nini maana ya kuwa kiongozi?! Ni kiongozi wa namna gani huyu?!!!
 
Back
Top Bottom