SO UNAONA NI BORA YABJIWE ALIYEONYESHA MSIMAMO WAKE, MOJA KWA MOJA KUWA NATAKA NCHI TWENDE HIVI AU VILE?
Hapana, tunahitaji hoja zote zifanyiwe kazi, kwamba kwanini zitumiwe na kwamba kwanini zisitumiwe, hoja itakayoibuka na ushindi wote tuifuate. Sasa kuacha hoja zinaelea hewani halafu unasema tu anaeona anataka kuchanjwa achanjwe, asiyetaka aache, ni akili za kitoto sana, na ni aibu kutolewa na kiongozi wa nchi.
Watu wanauliza, side effects za hizo chanjo za muda mfupi, muda wa kati (5yrs) na za muda mrefu (10yrs) ni zipi? Badala ya kujibu hoja mtu anakwambia ukitaka kachanje, hutaki acha ufe! Jamani, tuna kiongozi tuna nini hapo?!
Watu wanauliza, chanjo ili iitwe chanjo, kwa mujibu wa hao waliopitisha hiyo wanayoita chanjo (CDC Marekani), inatakiwa iweze kufanya nini na nini, na je, hicho kilicholetwa, kinafanya hayo ili kiweze kukidhi hivyo vigezo vya kuitwa chanjo? Definition ya chanjo ya CDC ipo yeyote anaweza kuipata kwenye website yao, labda kama wabadilishe sasa hivi hiyo definition, na kwa yeye kusema kwamba haizuii kuambukizwa, kuugua na kufariki basi automatically inafeli kuingia kwenye category ya chanjo, sasa watu wanauliza hii kama si chanjo, basi ni nini mnachotaka kutuchoma?! Je ni dawa? Definition ya dawa ni ipi? Na hii inakidhi vya kuitwa dawa?
Binafsi nashangazwa na aina ya udhaifu tulionao katika uongozi, udhaifu kama huu tulikuwa nao awamu ya 4 tu, na sidhani kama itakuja kujirudia tena; hatutakubali.