Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

Ni kama kusema ukikosea kifungu fulani cha kesi yako mahakamani jaji atakuonea huruma kwa sababu anajua ni kosa la kibinadamu. Ukiwa kiongozi (ukosee kwa kujua au kutojua) condemnation ni ileile na kiongozi inabidi alijue hili kabla hajapata nafasi ya kuwa kiongozi, ili ilitokea akakosea asitegemee umma utamsamehe kwa sababu kukosea ni ubindamu. Ni kama legal maxim inayosema 'judges like Caesar's wife must be beyond suspicion' - i.e. 'those holding public positions should avoid even the appearance of wrongdoing'.
 
Mkuu Telesphory Magobe T , nakuunga mkono ndio maana nimesema mkubwa ni jalala!, kila kosa atalaumiwa yeye hata kama mkosaji halisi sii yeye bali ni wasaidizi wake, na nikasema ukiwa kiongozi lazima uwe na ngozi ngumu!, ila kwetu sisi wana jf, tusimsakame, kumshutumu na kumlaumu kwa makosa ambayo sio yake.
P
 
Asante mkuu. Kwa mtazamo wangu, Kumsakama Rais hata kwa jf ni sawa, kwa sababu na yeye atajua wapi 'subordinates' wake hawakuwajibika kiasi cha kutosha. Kwa vile hawezi kufanya Kila kitu peke yake lazima mambo mengi a'delegate', na anaposakamwa anapata kujua wapi kuna tatizo, wakati tukinyamaza na kupiga makofi matatizo yanayosababishwa na watu wengine yataendelea kushamiri na hali hiyo itaipa serikali yetu sifa ya kutokuwa makini/kutoaminika machoni pa mataifa na viongozi na watu mbalimbali.
 

HBD Rais Samia
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…