Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huwaletea hizi makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa". Makala ya leo ni wito wa ustaarabu kwa Rais Samia, rais Samia Suluhu, sio malaika, ni binadamu kama binaadamu wengine wote na anaweza kukosea kama binaadamu wengine wote, kwa kufanya makosa ya kibinaadamu, hivyo nashauri, tusimfanyie nongwa, tusikalie kumlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa madogo madogo kabisa ya kawaida ya kibinaadamu, kwasababu binadamu wote huwa tunakosea, na hakuna mkamilifu.
Ila pale ambapo rais Samia amefanya makosa ambayo sio ya kwake, yale makosa ya kukoseshwa na wasaidizi wake au vyombo vyake, yakiwemo vyombo vya uteuzi vyenye jukumu la kufanya vetting, kwa baadhi ya watu wa hovyo hovyo kukwaa uteuzi, sio sawa, sio haki kumlaumu na kumshutumu mteuzi tuu yaani Rais Samia, nashauri kwanza, tumuonyeshe Mama Samia kuwa amechomekewa mabomu, kisha tumuonyeshe hayo makosa na makorokocho ya baadhi ya wateule wake walivyo wa hovyo, kisha tu project the consequences za kuwa na viongozi mabomu, kisha tumvumilie kwa tumpe muda wa kutosha kuwa atarekebisha mwenyewe yale makosa madogo madogo with time.
Tukiona ameambiwa makosa yake au makosa ya wateule wake, tukimkosoa kwa a constructive criticism tukamuonyesha the right thing to do, na kuonyesha madudu ya wateule wake, na yeye akiwaona bado wanamfaa, tuheshimu maamuzi yake, tusimpangie kwa jinsi ile ile ambayo hatukumpangia mtangulizi wake, lakini kwa sababu tutakuwa tumeainisha the consequences, hizo consequences zikija kutokea, tunakuwa hatuna jinsi, bali kumtundika msalabani!.
Declaration of Interest
Humu jf, kumezuka mtindo, ukisifia tuu jambo lolote zuri la viongozi wetu, unanyooshewa vidole kuwa unausaka uteuzi wa u-DC, na ukikosoa lolote, unanyooshewa kidole cha hizo ni hasira za kuukosa uteuzi!.
Naomba ku decrare interest, mimi Pascal Mayalla nikisifia, sisifii ili kuutafuta uteuzi, wowote wa nafasi yoyote, wanaosifia kwa ajili ya kutafuta uteuzi, kazi yao itakuwa ni kusifia tuu mwanzo mwisho na kamwe hutawasikia wakikosoa lolote!.
Mimi husifu tuu pale penye kustahili sifa na hukosoa kwenye makosa, ila ukosoaji wangu ni constructive cricitisim, nikikosoa naonyesha kosa, hapo hapo sio tuu nashauri nini cha kufanya, kurekebisha makosa, pia hutoa couscous statement ya the consequences if ushauri hautafuata, nini kitatokea!, hivyo ushauri ukipuuzwa likatokea la kutokea, unakuwa hauna jinsi, ni kumtundika msalabani kwa spana za kutosha!.
Mimi kwa shughuli zangu za PPR, nachangia fedha za kiasi cha kutosha kuwalipa mishahara ya mwaka mzima RC, DC na Mkurugenzi!, sasa mtu kama huyu, autafute u DC wa nini?!. Japo kwa sasa, nakiri kupigika sana lakini kwa mtu kama mimi, kitu ninachokihitaji kwa Mama, ni kuendelea tuu kuboresha mazingira ya biashara, PPR irudishe zile tenda zake, tumsaidie Mama, kumlipia mishahara ya ma RC, ma DC na Wakurugenzi wake!.
Japo mkubwa ni jalala, na ukiwa kiongozi ni lazima uwe na ngozi ngumu, lakini tusimsakame saana Mamaa kwa makosa ambayo sio makosa yake bali ni anakuwa ameshauriwa vibaya na wasaidizi wake!.
Pili, Rais Samia sio malaika ni binadamu tuu, kama binaadamu wengine wote, hivyo na yeye kama binadamu, anaweza kukosea kama, binadamu wengine wowote, hivyo anapokosea anahitaji kusaidiwa kwa kukosolewa kwa lugha ya kistaarabu, staha na heshima kwa kumuonyeshea kosa, ushauri wa kurekebisha, namna bora zaidi ya kulifanya hilo jambo, na the consequences of mapuuza endapo atapuuzia!.
Pia tujenge tabia ya uvumilivu wa kuyavumilia makosa madogo madogo ya kibinaadamu, to err is a human nature!.
Nakiri kupandisha bandiko kufuatia kelele nyingi za shutuma, lawama, kumsakama Mama Samia kwenye uteuzi wa baadhi ya watu. Mfano ni bandiko hili
Ni Albert Msando. Look at him. Wamekosekana kabisa watu wenye maadili na wanaojiheshimu mpaka kupelekea huyu ateuliwe? What was he doing there? Fingering her? What the hell is wrong with you Samia? Do you just flip a coin when picking these people? Do you conduct any background checks on...
www.jamiiforums.com
Mkuu Nyani Ngabu, kwanza naunga mkono hoja ya vetting, Mama amepelekewa makorokocho, na yeye bila kujua ni makorokocho, akateua tu.
Kuna baadhi ya makorokocho hayo, sababu ya uteuzi wao ni mchango wao kwa CCM, Msando amefanya kazi mzuri iliyotukuka kwenye ile kamati ya mali za CCM.
Hayo makorokocho na Gigy ni personal private matter akiwa under influence of alcohol. Kuvuja kwa hizo video ni kuingilia privacy zake, kama tutapekenyeua privacy za kila mtu kwa kutumia a hidden camera, hakuna msafi, na hakuna atakayebaki !.
Mwisho, with due respect, umetumia lugha kali mno na very harsh kwa mtu gentle kama Mama Samia.
Maneno kama
"What the hell is wrong with you Samia?"
"Shameful! Repulsive! Disgusting!"
"shame on you Samia! Are you proud of appointees like this?"
"Are you that morally bankrupt? You don’t care? Don’t give a damn?"
are unclalled for kwa mtu mwenye sifa kama za Mama Samia, wote tunajua vetting hafanyi yeye, yeye analetewa tuu majina, hivyo maneno makali haya, hayamstahili, mtu mwema, mpole, mstaarabu, mwelewa, mnyenyekevu kama Mama Samia.
Na kwa kuongezea, tofauti kubwa ya mwanaume na mwanamke sio physiological on sex tuu ya being male and female, bali ni psychological, men thinks, women feels, ukimtukana mwanaume kwa maneno makali hata matusi, mwanaume can take it na isiwe a big deal, kwasababu ana ngozi ngumu, lakini kwa mwanamke, it's not, wanawake wana ngozi laini, hivyo naomba usiyalize yale macho, laini, legevu, ukayarowesha kwa machozi, utatuumiza wengi!. Please lets spare this lovely lady kwenye baadhi ya mambo.
Hitimisho
Kama ambavyo hatukumpangia Magufuli, nashauri pia tusimpangie Samia, tuepuke matukano, lugha za machukizo, ukali kebehi, kubagaza, tuendelee kumkosoa kwa lugha ya heshima, staha, kistaarabu kwa nia ya kujenga, huku tukikosoa constructively kwa nia ya kujenga huku tukishauri, the right thing to do.
Ni kama kusema ukikosea kifungu fulani cha kesi yako mahakamani jaji atakuonea huruma kwa sababu anajua ni kosa la kibinadamu. Ukiwa kiongozi (ukosee kwa kujua au kutojua) condemnation ni ileile na kiongozi inabidi alijue hili kabla hajapata nafasi ya kuwa kiongozi, ili ilitokea akakosea asitegemee umma utamsamehe kwa sababu kukosea ni ubindamu. Ni kama legal maxim inayosema 'judges like Caesar's wife must be beyond suspicion' - i.e. 'those holding public positions should avoid even the appearance of wrongdoing'.
Ni kama kusema ukikosea kifungu fulani cha kesi yako mahakamani jaji atakuonea huruma kwa sababu anajua ni kosa la kibinadamu. Ukiwa kiongozi (ukosee kwa kujua au kutojua) condemnation ni ileile na kiongozi inabidi alijue hili kabla hajapata nafasi ya kuwa kiongozi, ili ilitokea akakosea asitegemee umma utamsamehe kwa sababu kukosea ni ubindamu. Ni kama legal maxim inayosema 'judges like Caesar's wife must be beyond suspicion' - i.e. 'those holding public positions should avoid even the appearance of wrongdoing'.
Mkuu Telesphory Magobe T , nakuunga mkono ndio maana nimesema mkubwa ni jalala!, kila kosa atalaumiwa yeye hata kama mkosaji halisi sii yeye bali ni wasaidizi wake, na nikasema ukiwa kiongozi lazima uwe na ngozi ngumu!, ila kwetu sisi wana jf, tusimsakame, kumshutumu na kumlaumu kwa makosa ambayo sio yake.
P
Mkuu Telesphory Magobe T , nakuunga mkono ndio maana nimesema mkubwa ni jalala!, kila kosa atalaumiwa yeye hata kama mkosaji halisi sii yeye bali ni wasaidizi wake, na nikasema ukiwa kiongozi lazima uwe na ngozi ngumu!, ila kwetu sisi wana jf, tusimsakame, kumshutumu na kumlaumu kwa makosa ambayo sio yake.
P
Asante mkuu. Kwa mtazamo wangu, Kumsakama Rais hata kwa jf ni sawa, kwa sababu na yeye atajua wapi 'subordinates' wake hawakuwajibika kiasi cha kutosha. Kwa vile hawezi kufanya Kila kitu peke yake lazima mambo mengi a'delegate', na anaposakamwa anapata kujua wapi kuna tatizo, wakati tukinyamaza na kupiga makofi matatizo yanayosababishwa na watu wengine yataendelea kushamiri na hali hiyo itaipa serikali yetu sifa ya kutokuwa makini/kutoaminika machoni pa mataifa na viongozi na watu mbalimbali.
Zawadi yangu kwa Birthday ya Mama nilipanga kumpa wiki ya mwisho ya October 2025,
Ili zawadi hii iwe na manufaa kwake, nikisubiri mpaka hiyo 2025, it might be a bit too little too late, kuna ubaya hiyo zawadi, kutolewa mapema mwaka huu ili iweze kutumika mwaka kesho?.
Zawadi yenyewe ni Salaam tuu za Birthday zenye ki parcel fulani!
HBD Mhe. Rais Samia kwa kutimiza miaka 64!, nakupongeza sana na kukuombea afya njema!.
Mwakani 2025 utakuwa unatimiza umri wa miaka 65 na 2030 utakuwa na umri wa miaka 70, hivyo zawadi yangu ya pekee kwako ni HII na kukusisitizia, sio lazima kuizingatia saana kivile, ila ni muhimu kuisikiliza na kujisikilizia kama na wewe pia uliambiwa kama nilivyoambiwa mimi, kwasababu yule YEYE, sometimes ana tabia na mtindo wa kuwaambia watu wake, kupitia kwa watu wengine!, hivyo just listen and try to make sense of this, a think about it, if makes any sense to you, ikitokea it doesn't make any sense to you, then dismiss it as just another set of crap!.
Ila ikitokea na wewe pia uliambiwa, but you are not very sure kama ni YEYE au ni yeye, then don't take a chance!, usipuuze!, maana hicho kitu chenyewe, is nothing compared!.
If this being the case, then tunakuomba sana sana sana, ututekelezee haya mambo tunayokulilia nayo tangu umeingia kwenye usukani, tekeleza tuu yale yaliyomo ndani ya uwezo wako, maana kusubiria post 2025, it might be too little too late!. Please Mama!.
Na ikitokea wewe hujaambiwa mpaka 2025 inaingia na hujawahi kuambiwa na mtu mwingine yeyote, then ipuuze HII itakuwa sio sauti yake YEYE bali itakuwa ni sauti ya yeye tuu ambaye sio YEYE!.
Hivyo endelea na ule mpango wako wa 2025!, na Watanzania wanaolitakia mema taifa letu hili, wote tutakuwa Tuko nyuma yako,
Tuko pamoja nawe,
Tuko nawe!.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.