tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi pasipo kuwachosha. Rais Dr Samia atajaribu kumuiga Magufuli lakini kamwe hataweza asilani hadi anaondoka madarakani. Wakati Dr Magufuli akiwa Rais aliusaidia sana mkoa wake wa Chato kimaendeleo na kiuchumi. Hili halihitaji utafiti kwani liko wazi kwa kila Mtanzania mwenye akili zilizotimia.
Baada ya Dr Samia kushika madaraka anajaribu kufuata nyayo za Magufuli lakini ameshindwa kuzifuata sawasawa. Tukumbuke Magufuli alipeleka Chato mbuga ya wanyama, uwanja wa ndege wa kimataifa, hospitali ya kanda, mabenki, ujenzi wa vivuko vya majini, ujenzi wa barabara kila kona ya Chato na mambo mengine kadha wa kadha. Mtu kwao.
Sasa wewe fikiria Magufuli kapeleka kwao mambo yote haya halafu Dr Samia (chifu Hangaya) yeye anapeleka akademi ya mpira na matamasha ya “Usiku wa mama Samia”. Hivi huyu Rais kweli ana uzalendo wa kutosha kwa watu wa Kizimkazi kama Magufuli alivyokuwa serious na Chato? Mimi tpaul nasema huyu mama hana uzalendo na mahali alipotoka.
Hafai kwa kula wala kwa kulumangia. Hivi anawaonaje au anawachukuliaje watu wa Kizimkazi kwa kuwapelekea matamasha na viwanja vya mpira wakati wazanzibar mambo ya mpira sio kipaumbele chao?
Mama aliwahi kusema yeye na Magufuli ni kitu kimoja. Iweje leo aende tofauti na Magufuli kama sio kukengeuka? Inasikitisha sana. Mtu kuwa pamoja na mtu sharti uwaji huo wa pamoja uhusishe matendo sio maneno matupu ambayo hayawezi kuvunja mfupa. Tafadhali sana Dr Rais Samia nakuomba uwaheshimishe wanaKizimkazi kama Magufuli alivyowaheshimisha wanaChato. Mdharau kwao ni mtumwa. Usiwe mtumwa Tanganyika ukasahau kwenu Zanzibar.
Nawasilisha.