Rais Samia: Sio na kigazeti chako mara uandike Samia hivi mara vile, vingine vya uongo vingine vya ukweli

Tatizo wengine wanaandika upotoshaji makusudi. Kazi kuharibu tu
Wakipotosha kwa makusudi bila facts, then sheria ifuate mkondo wake. Lakini sio sahihi kuwatisha watu na kutaka waogope kurusha madongo heavy kwa kile kinachoitwa “heshima ya kiafrika”
 
Acha upuuzi.

Muachiwe mseme.....mpaka muharibu

Hakuna uhuru huo.

Tena mumshukuru sana alie waumba.
 
Wakipotosha kwa makusudi bila facts, then sheria ifuate mkondo wake. Lakini sio sahihi kuwatisha watu na kutaka waogope kurusha madongo heavy kwa kile kinachoitwa “heshima ya kiafrika”
Umenikumbusha, "heshima ya kiafrika" ndo inatuponza

Tunaachia Mali zetu: ardhi, madini, wanyama bure kabisa kwa wageni kwa majina ya "ukarimu wa kiafrika" na "heshima ya kiafrika"

Wakati ilitakiwa tuvifanye hivyo vitu viweze kutukwamua kiuchumi
 
Wakipotosha kwa makusudi bila facts, then sheria ifuate mkondo wake. Lakini sio sahihi kuwatisha watu na kutaka waogope kurusha madongo heavy kwa kile kinachoitwa “heshima ya kiafrika”
Kisheria utafungiwa, eenh vipi ukichafuliwa kwa uchafu wa rangi za mafuta na sabuni ya kukusafishia ya magadi unadhan utaeleweka kuwa wewe ni smart.?

Unaonaje ukitukanwa mbele ya hadhira kisha mkosa wako akakufuata private kukuomba radhi?
 
Shida ya mmbongo kupewa uhuru wa kufungua bakuli lake atakavyo ndio hii!
 
Mama ameanza kujisahau. Sasa minamuonya, ile njia alipita mtangulizi wake na yeye ataipita haraka sana
 
Asifikie kiwango cha jiwe cha watu kupotezwa
Namuelewa and it was much expected.

Ukiwa na power you become jealous of it to the extent of using every means available to protect it.
 
Watawala wanapenda sana kuuamanisha umma vyombo vya habari visivyochukua mrengo wa serikali vinatoa habari za uongo na uzushi.
Vyombo vya habari muda mwingine vinakosa weledi.kwanini wasiandike habari za kweli? Uzushi na uongo wakati mwingine unaviondolea credibility vyombo hivyo.
 
Vitu vingine tuwe wakweli, hivi Mbowe na wafuasi wake wako tayari kumuona Msigwa, Heche ua Sugu akizungumzia uenyekiti wa Mbowe? Wana Uhuru wa kusema Mbowe uenyekiti wako umekaa muda mrefu? Tunaomba tubadiri katiba ya CHADEMA mwenyekiti upumzike?

Au ndo MWAMBA TUVUSHE?
 
Your???
 
Vyombo vya habari muda mwingine vinakosa weledi.kwanini wasiandike habari za kweli? Uzushi na uongo wakati mwingine unaviondolea credibility vyombo hivyo.
Mtu kama Kubenea ni bingwa sana wa kuchonga vijitaarifa halafu anaita vya uchunguzi.

Sasa hivi naona ndiye mhariri wa Raia Mwema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…