Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Akizungumza wakati anazindua jengo la ofisi y mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Rais Samia amewataka viongozi wa Halmashauri hiyo kutumia jengo hilo kurahisisha kufanya kazi zao kwa sababu miundombinu ni mizuri na pia aliwataka watumishi watoe huduma nzuri kwa wananchi.
Samia aliongeza kwa kusema:
“Niwatake Watendaji kusimamia miradi na Watendaji ni pamoja na Madiwani, muendelee kuweka nguvu kusimamia miradi ili yale yanayowakera Wananchi yaweze kuondoka, utumishi wetu Mimi na Nyinyi kuhudumia Wanachi, sisi ni Watumishi wa Wananchi na si Mabwana wa Wananchi, si watawala wa Wananchi, sisi ni Watumishi kwa Wananchi, ndio maana Serikali inashusha fedha nyingi ili zifanyiwe kazi Wananchi hawa waondoshewe shida zao”