Rais Samia Suluhu akutana na Edward Lowassa

Rais Samia Suluhu akutana na Edward Lowassa

Mzee Lowasa, mzee wa hekima. Alienda CHADEMA bila ya kejeli kwa CCM, akarudi CCM bila ya kejeli kwa CHADEMA.

Aliambiwa anagombea Urais wakati yeye ni wa kufa wakati wowote, hakusema kitu zaidi ya, "maisha ya mwanadamu hupangwa na Mungu", na hakika Mungu kampangia aendelee kuishi, sawa na alivyopanga wengine watangulie ili yeye ashuhudie kuondoka kwao badala ya wao kushuhudia kuondoka kwake.

Pamoja na tofauti zozote zile, Lowasa could have been a better president than what we got in 2015.
 
Hii ndio taarifa mpya inayopatikana mitandaoni baada ya Rais kumtembelea Lowassa nyumbani kwake , bali haijulikani nini walichojadiliana .

UMESHATOKA MAHAKAMANI UMERUDI HUKU TENA?NAONA KULE LEO HAKUKALIKI USHAHIDI MURUWAAAAA KWA GAIDI UMEMMALIZA KABISA UKAONA BORA UJE URIPOTI YA MAMA YETU EEE???
 
Hii ndio taarifa mpya inayopatikana mitandaoni baada ya Rais kumtembelea Lowassa nyumbani kwake , bali haijulikani nini walichojadiliana .

Mzee Lowassa ni nguli wa siasa za Tanzania, mwenye nguvu na ushawishi ndani ya Chama tawala CCM na ndani ya Chama kikuu cha upinzani, yaani CHADEMA. Ni mwanasiasa mahiri Tanzania kuliko mwingine katika miaka ya karibuni. Prof Mwandosya aliwahi kumuelezea Lowassa kama mzee wa mipango, mwanasiasa makini ananiambia haraka kwamba aanzie wapi na amalizie wapi tena bila kutumia kauli za leo leo. Anajua atamke nini wakati husika na wapi akae kimya. Kama Rais kamtembelea bila shaka ni kwa kujua mchango wake nami namtakia Mungu wa Rehema amuimarishe mzee wa watu na wote wanaomtunza. My white hair!
 
kama ningekuwa na uwezo wa kurejeshea watu nguvu na uimara akawa kama mwanzo alivyo kuwa, basi kwakweli mtu wa kwanza angekuwa Mzee Lowasa.
Mzee Lowasa ni Mwanasiasa wa kuigwa na wanasiasa wengine.
 
Hii ndio taarifa mpya inayopatikana mitandaoni baada ya Rais kumtembelea Lowassa nyumbani kwake , bali haijulikani nini walichojadiliana .

Maigizo ya kupambana na Corona Tanzania ni kichekesho...wanashikana mikono,hakuna social distance,watatu akiwemo Hangaya hawajavaa barakoa,mmoja kavaa libarakoa Kama bakuli.
Kuigiza ni kazi ngumu waachieni akina Johari tu.
 
Maisha haya kweli Mungu hupanga wakati wanadamu huwaza tu...

Mzee Lowassa yupo vizuri kabisa, wakati waliokuwa wakimkejeli kwa mipush ups miaka ile sijui hata wapo wapi...
Kweli kabisa hata waliofurahia mpiga push up kutwaliwa,familia zao zinanyofolewa na Israel,Kaka mtu,mama mkwe😈😈
 
Kaa kwenye nyumba za tembe ukisubiri tshirt na kofia 2025
FB_IMG_1575390800494.jpg
 
Back
Top Bottom