Rais Samia Suluhu amedhamiria kuodoa utegemezi wa ngano kutoka nje

Rais Samia Suluhu amedhamiria kuodoa utegemezi wa ngano kutoka nje

Getrude Mollel

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2022
Posts
270
Reaction score
362
Tanzania imeandaa mkakati kabambe wa kuondoa kabisa utegemezi wa zao wa ngano kutoka nje ambapo malengo yaliyowekwa hadi ni kufikia uzalishaji wa tani milioni moja ifikapoi 2025.

Tanzania huagiza ngano kwa wingi kutoka Urusi na Ukreini ambapo kutokana vita katika nchi hizo, kumepelekea uhaba wa zao hilo kwa kiasi kikubwa sana katika nchi nyingi ikiwemo Tanzania.

Ni hatua gani zimechukuliwa na serikali ya Rais Samia Suluhu kuondoa kadhia hiyo?

Kuongeza eneo la uzalishaji
Mwaka 2020/21 Tanznia ilizalisha tani 70,288 za ngano kwenye eneo la hekta 100,000 huku uhitaji wa ngano kwenye soko la ndani ukiwa ni tani milioni moja. Hivyo basi, Tanzania imeazimia kuongeza eneo hadi hekta 400,000 ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 300 ya eneo lilioongezwa ambapo inatazamiwa, eneo hilo kuweza kuzalisha tani milioni moja ifikapo 2025.

Kutumia mbegu za kisasa zenye matokeo makubwa
Tani 210 za mbegu za kisasa kutoka Zambia zimeagizwa ili kusambazwa kwa wakulima nchi.

Utafiti
Bajeti ya Kilimo 2022/23 serikali imetenga milioni 750 kwa ajili ya utafiti kwenye mazao ikiwemo ngano. Tanzania Agriculture Research Institute (TARI) imeshakusanya mbegu 11 nchi nzima kwa ajili ya kufanya tafiti ili kubaini mbegu gani ni bora na ishauriwe kupandwa kwa wingi. Tari tayari imefanikiwa kuwafikia wakulima 6000 nchi nzima.

Ujenzi wa viwanda
Kutokana na kutokuwa na miundombinu imara ya kutunzia zao la ngano baada ya kuvunwa na kupelekea kuhabika kwa zao hilo, Tsh. Bil 20.5 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vitatu kwa ajili ya kuchakata ngano. Viwanda hivyo vitajengwa Mbeya, Mwanza na Dar es Salaam.

wheat_0.jpg
 
Back
Top Bottom