Rais Samia Suluhu anafanya makubwa sekta ya usafiri wa anga

Rais Samia Suluhu anafanya makubwa sekta ya usafiri wa anga

Getrude Mollel

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2022
Posts
270
Reaction score
362
Katika mwaka wa fedha 2022/23 Serikali ya Rais Samia Suluhu imetenga Sh. 86.1bn/- kwa ajili ya ujenzi na marekebisho ya viwanja vya ndege mbalimbali nchi nzima.

Lengo ni kuboresha sekta ya usafiri wa anga na pia kuimarisha sekta ya utalii ambayo imekuwa ikichangia kiasi kikubwa sana cha fedha kwenye pato la Taifa.

Viwanja ambavyo vimepewa kipaumbele ni Kigoma, Mpanda, Songwe, Tabora, Arusha, Mtwara na Mwanza. Serikali haitoishia hapo, Waziri mwenye dhamana Mh. Makame Mbarawa amesema kwamba Serikali ya Rais Samia Suluhu itajenga na kukarabati viwanja vyote 58 nchi vilivyo chini ya Mamlaka ya viwanja vya ndege nchini (TAA)

Hata hivyo, katika bajeti ya 2022/23 Serikali imtenga bajeti ya Tsh 20.4bn/- kwa ajili ya Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Msalato jijini Dodoma, Makao Makuu ya Serikali.

Serikali ya Rais Samia Suluhu pia imetenga Sh. 356bn/- kwa ajili ya kuboresha Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ambapo hadi sasa shirika lina ndege mpya 11 huku tayari ikiwa ndege nyingine mpya 5 zimeagizwa ambapo zitafika mwanzoni mwa 2023.
 
Back
Top Bottom