kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 119
- 240
Mashabiki takribani 31,620 waliohudhuria mechi ya Ligi Kuu ya Soka ya Marekani na mamilioni zaidi duniani waliokuwa wakitazama “live” mechi ya Seattle Sounders dhidi ya Sporting Kansas City kupitia FOX TV na Apple TV, wamepata fursa ya kushuhudia Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania akienziwa katika tukio maalum kabla ya mechi hiyo kuanza mjini humo jana Jumapili Mei 7, 2023.
Mmiliki wa Seattle Sounders, Bilionea Adrian Hanauer, aliamua kutumia mechi hiyo kufanya tukio la kumpongeza Rais Samia kwa hatua zake za kutangaza utalii wa Tanzania hasa kupitia filamu ya Royal Tour. Kwa heshima hiyo, Hanauer jana alitumia mechi hiyo kukabidhi jezi maalum yenye jina la Rais Samia kwa Katibu Mkuu Wizara ya Utalii, Dkt. Hassan Abbasi na ujumbe wake na zaidi kutoa heshima kwa ujumbe wa Tanzania kupiga picha maalum na kikosi cha Sounders kabla ya kuanza kwa mechi hiyo muhimu.
Tukio hilo linakuja ikiwa ni siku chache tu baada ya juzi ambapo wamiliki wa Seattle Sounders walitoa fursa nyingine ya kuutangaza utalii wa Tanzania katika sehemu ya uwanja huo kwa kuionesha filamu ya “Tanzania; The Royal Tour” kwa wawakilishi wa makampuni makubwa duniani kama Google, Boeing, Starbucks, Amazon, Delta na Microsoft na ofisi ya Meya wa Seattle.