Rais Samia Suluhu apokea andiko la ombi la Tanzania, Kenya na Uganda kuwa Mwenyeji wa AFCON 2027

Naomba Mungu ombi lisikubaliwe ili tuikwepe aibu ya taa za uwanjani kuzimika na mpira kusimamia kwa masaa 2 huku dunia ikituangalia
 
Sasa timu washiriki si huwa wana free entry sasa kama nchi tatu tunaomba kwa pamoja maana yake yani kenya Tanzania na Uganda ziingie free tu kwenye afcon..hii mbona kama itagomewa na caf
 
Acha ujinga wako hapa wewe, kwani wanaoendaga kuitazama ligi kuu na kujaza uwanja wa mkapa huwa unawalipia wewe viingilio? Huwa unawasafirisha wewe?
 
Acheni siasa kwenye mambo tusiyo na uwezo nayo!

Kiwanja kimoja tu chenye hadhi hiyo ya AFCON halafu mbwembwe kibao!
Ndio maana ya joint bid... Nchi 3 kila moja ikiwa na viwanja 2 hivyo ni viwanja 6. Vinatosha kabisa ku-host AFCON. Tanzania tayari tuna uwanja mmoja wenye hadhi
 
Wakatavyolipigia debe hili jambo

Ngojeni muone

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…