Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wa mabalozi; wamo Hoyce Temu na Togolani Mavura

Noel, good job lad! Rais amechagua hapa.
 
Waliosomea diplomasia hawateuliwi ubalozi , wanateuliwa mamiss uchwara , CCM hakuna haja ya kusoma it's not what you know , but whom you know kijani kibichi oyeeeee .
 
23 May 2021

PRESIDENT SAMIA SULUHU HASSAN ATTENDING THE ONLINE MEETING WITH AFRICAN WOMEN LEADERS NETWORK

Source : michuzi tv

Balozi namba moja Mh. Samia Suluhu Hassan rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akishiriki mkutano wa kimataifa mtandaoni.

Kwa njia hii inaonesha balozi namba moja rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anahakikisha sera ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa ya Tanzania inapata msukumo chanya hivyo kuwatia moyo na kuwapa visheni balozi namba 2 waziri wa masuala ya nje Mh. Liberata Rutageruka Mulamula na mabalozi wengine wengi namba 3 waliopo ktk utumishi na hawa wengine walioteuliwa jana.

Kwa namna hiyo mabalozi wote wa Tanzania watakuwa wanafahamu Mh. Rais anataka kurejesha ushawishi wa Tanzania kimataifa na kuibeba vyema diplomasia ya kiuchumi.

 
Hapana watu walitoa mapovu iweje ateuliwa balozi na kupewa Ukatibu mkuu kiongozi kwani wewe unaishai sayari gani?
Labda ni hao uliowasoma ambao hawakuelewa hoja kuu na wewe ukabaki na hiyo hoja ya u Balozi. Kuwa balozi kila mtu aweza teuliwa, haina vigezo vyovyote vya watu kuhoji. Watu walihoji u Katibu Mkuu Kiongozi na ninajua hata wewe unajua kwa nini watu walihoji, lakini unakimbilia kwenye kichaka cha u Balozi ambako unaona unaweza kuwa na ya kujadili. Umeshaambiwa huko hakukua na shida, tujadili kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.
 
Rais Samia yupo vizuri akienda sambamba na dunia ya webinar na video conferences. Anatekeleza yale maneno aliyosema ikulu kwamba hatuwezi kufika popote kwa kwenda peke yetu ni lazima twende na wenzetu.

Hii miradi mikubwa anaweza kuimaliza mapema sana kwa njia hii ya kujichanganya na jamii za kimataifa.
 

Mh. Rais inaonekana haogopi mitandao wala teknolojia ya habari na mawasiliano, inatutia moyo kuona kama kiongozi wa nchi anatumia fursa zote iwe face-to-face ( tête-à-tête / head to head meeting) au kutipia TEHAMA kuifikia jumuiya ya kimataifa, wafanyabiashara na watu wa kawaida yote kwa manufaa ya nchi.

Kiongozi lazima uendane na kasi ya mabadiliko ya teknolojia iwe kwake binafsi au kwa kutumia wasaidizi wake.

Siyo kama wakati wa awamu ya tano full viongozi kukwepa jumuiya ya kimataifa kwa visingizio vingi vya kutopenda safari, kuogopa video-conferencing, Zoom meeting, kujiwekea vikwazo kwa kutotumia lugha rafiki ya kimataifa ya biashara na diplomasia ya Kiingereza n.k
 
Kuna baadhi ya matatizo ya kiuchumi utatuzi wake wakati wa awamu ya tano ulikuwa ndani ya mipaka ya uwezo wa uongozi wa juu wa nchi na pia yapo matatizo ambayo ni ya kidunia yenye kusumbua kila nchi.

Awamu ya sita ikipambana na kutatua yale matatizo yenye kuweza kutatulika inaweza kuifikisha mbali sana nchi kimaendeleo.

Hii njia ya kujichanganya kimataifa anayoitumia rais inatusaidia kupata ile positive image, ambayo yenyewe kama yenyewe ni mtaji tosha wa kukuza uchumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…