Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wake wa kwanza Ikulu. Gerson Msigwa atolewa Ikulu, Dotto James ahamishwa. TPA, TCRA na TRA zapata wakuu wapya

Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wake wa kwanza Ikulu. Gerson Msigwa atolewa Ikulu, Dotto James ahamishwa. TPA, TCRA na TRA zapata wakuu wapya

Kama Mataragio hakutumbuliwa na Magufuli muda wote huo, basi ujue alikuwa ni mtu quality! Magufuli alikuwa ni mwepesi kufanya maamuzi, ila akishatulia na kufanya analysis akiona mtu aliyemtumbua alikuwa hana kosa basi alikuwa akimteua tena sehemu nyingine. Mataragio hakutumbuliwa hata kwa kesi moja yoyote ya harakaharaka!!

MKURUGENZI TPDC AACHIWA HURU NA MAHAKAMA​

August 19, 2019


Vigogo watano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC),akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo,James Mataragio wameachiwa huru leo August 19, 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP) kutokuwa na nia ya kuendelea na Mashitaka dhid yao.

Mataragio na wenzake walikuwa wakikabiliwa na shtaka moja la matumizi mabaya ya madaraka ambapo ilidaiwa kati ya Aprili 8, 2015 na Juni 3, 2016 walitenda kosa hilo wakiwa watumishi wa umma na waajiriwa wa TPDC.

Agosti 24, 2016 Bodi ya Wakurugenzi wa TPDC, ilimsimamisha Mkurugenzi huyo kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizokuwa zikimkabili .


Hata hivyo, Julai 22, 2019 Rais Magufuli aliielekeza wizara ya nishati kumrejesha ofisini katika wadhifa wake aliokuwa nao kabla ya kusimamishwa na kushtakiwa.

Wengine waliofutiwa mashtaka ni George Seni, aliyekuwa Kaimu Meneja wa Uvumbuzi; Welington Hudson, aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Utawala; Kelvin Komba, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mkondo wa Juu na Edwin Riwa aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Mipango

Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Saimoni amedai leo Jumatatu Agosti 19,2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Kelvin Mhina kuwa shauri hilo limekuja kwaajili ya kusikilizwa lakini Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameonyesha nia ya kutoendelea na kesi hiyo

DPP kwa niaba ya Jamuhuri amesema hakusudii kuendelea kuwashtaki washtakiwa hao katika kesi hiyo na akaomba iondolewe chini ya kifungu cha 91 (1) cha Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA) Sura ya 20. Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mhina aliwaachia huru washitakiwa hao chini ya sheria hiyo.
 
Mara 100 angewekwa sultan bashite pamoja na kuwa ni mjinga nambari wani mbinguni na ahera
 
Msaada tafadhali unaweza kuweka link tukatazama CV yake huyu Mkurugenzi mpya?
Nyie binadamu mnaoomba CV za watu hivi huwa mnaenda kuzifanyia nini?
CV ya mtu kuitazama inakusaidia nini katika maisha yako?
 
Tanzania kuna fitna na majungu Sana. Yaani unatengenezewa kashfa mpaka watu wanaamini ni kweli. Kumbe chuki binafsi tu. Mimi nilishafanyiwa fitna, nikatengenezewa chuki ambayo ilisababisha Mimi kupoteza mali yangu yote. Mpaka SASA imeathiri hali yangu ya uchumi na maisha.
WATU WAELEWE RAISI NI TAASIS. HAWEZ KUFANYA KAZI KWA MIHEMKO AMA TAARIFA ZA MITANDAONI. MH. RAISI ANA TAARIFA SAHIHI KUMUHUSU DOTTO KULIKO MTU YEYOTE YULE. RAISI HAWEZ PANGIWA KUFANYA TEUZI ZAKE NA WHISTLE BLOWERS.
Kumbuka hawa ni Viongozi wa Uma sio wa rais so kama wananchi hawamtaki au wanamshuku mtu... lazima ifanyike au mnadhani viongozi wana tu favour wananchi hata tuwaamini kila wanachofanya!

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Tanzania kuna fitna na majungu Sana. Yaani unatengenezewa kashfa mpaka watu wanaamini ni kweli. Kumbe chuki binafsi tu. Mimi nilishafanyiwa fitna, nikatengenezewa chuki ambayo ilisababisha Mimi kupoteza mali yangu yote. Mpaka SASA imeathiri hali yangu ya uchumi na maisha.
WATU WAELEWE RAISI NI TAASIS. HAWEZ KUFANYA KAZI KWA MIHEMKO AMA TAARIFA ZA MITANDAONI. MH. RAISI ANA TAARIFA SAHIHI KUMUHUSU DOTTO KULIKO MTU YEYOTE YULE. RAISI HAWEZ PANGIWA KUFANYA TEUZI ZAKE NA WHISTLE BLOWERS.
Kumbuka hawa ni Viongozi wa Uma sio wa rais so kama wananchi hawamtaki au wanamshuku mtu... lazima ifanyike au mnadhani viongozi wana tu favour wananchi hata tuwaamini kila wanachofanya!

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo nidyo njia sahihi.Haiwezekani mtu mmoja kuwa anawajua wote hao.
Hawa Wakurugenzi wa Mashirika ya umma inabidi waanxe kuomba kazi na kufanyiwa usaili.Au majina yawe yanapendekezwa na Bunge.
 
A
Kweli sijaona kipya kafanya reshuffle tu.
Amefanya kitu.
Amepunguza msongamano wa aina fulani, au niseme amepunguza SUFFOCATION iliyokuwa imeletwa na kikundi fulani.
Angalia waliotoka, au kuhamishwa, asili yao, au unasaba na "wapendwa"
KM Kusaya. "madawa ya kulevya" (Mz)
KM Mchembe. "out" (Mz)
KM Mwaluko. "out" (dada wa Kabudi)
KM Dotto. "uhamisho" (mpwa wa JPM)
KM Nyamhanga. "out" (Tanroads)
TPA Kakoko. "out" (Tanroads)
NSSF Erio. "out" (mpwa wa BWM)
Kikundi kilichokuwa kinaleta suffocation kinapungua polepole.
Bado suffocation ya Maprofesa.
Ni muhimu ipungue ili warudi kufanya kazi ya weledi wao, ambayo ni kufundisha Vyuo Vikuu.
 
Kapilimbi alipo hudumu ni sawa na TPDC?
Bandiko langu limejificha kidogo
Nilimaanisha kuwa hawa watu wa system cv zao hazieleweki,wakati mwingine ni very shallow
Naamini aliemuweka pale ana sababu nzito sana ambazo bahati mbaya hatuna nguvu ya kuzihoji
 
Waliomwambia Rais amfukuze Doto James mlale unono sio kwamba namkubali jamaa ila nazikubali strategies za Rais SSH

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki Rais wetu Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote [emoji7][emoji1241][emoji123]

Rest well our hero President John Pombe Magufuli [emoji885]
Your hero not me shubbbbbbat zako
 
Ameuacha kipenzi chako Gwajima kwenye afya[emoji3]. Endelea kunywa mtori nyama utazukuta chini.
Hotuba zake za mwanzo tu niliona mama atakuwa shida, alipomtoa Jaffo TAMISEMI ndio kabisa.

Hivi anafahamu nishati ni priority number 1 ya national security duniani. Huu utani wake mmbaya sana.
 
Kwa hiyo alikuwa ni Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu msemaji Mkuu wa Serikali?
Yes,mwanzo alikua msemaji mkuu,akapandishwa cheo kuwa katibu mkuu baada ya uchaguzi wa 2020,lakini akaambiwa ataendelea kuwa msemaji mkuu
Msigwa ndio amepanda cheo kwa kuwa msemaji mkuu
 
Subiri uchunguzi ukamilike.
Unadhani kutakuwa na jipya gani? ndio maana sisi wengine hatutamani ccm iendelee kuwepo mamlakani kingekuwa chama kingine angalau unaweza kufikiri tofauti Ila kwa ccm usipoteze muda wako unaweza kupata kiharusi maana unapotarajia kifanyike kitu cha maana kwa maslahi ya Nchi watu wanafanya kwa maslahi ya ccm

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Mama ashasema kuwa haangalii jina, mtu na ma CV yeye anaangalia utebdaji kazi wa mtu
 
Huyu kijana hapana.
Uzoefu wake mkubwa ni UVCCM!
Hili ni furushi la samadi ya mbolea mbichi.
Zama hizi mpya, bado mama Samia anakwenda kuokoteza makada wa CCM ambao wengi wao ni mitindio wa ubongo!
Mama kaingizwa mkenge.. nina imani ujumbe utamfikia.
 
Back
Top Bottom