Naomba sana, tena sana; tusishangilie kabla ya kujua utendaji wa wateule wapya. Tuwe na subira, pengine nao wana maovu yao, hao si malaika! Tukumbuke hata tengua-teua ya Magufuli tulishangilia sana na ufisadi ukaendelea kama kawaida TAMISEMI, Benki Kuu, bandarini na kwingineko kwingi.
Usifurahie uteuzi, furahia ufanisi wa mtu baada ya kuanza kazi. Tutulie wakati huu Rais anapanga safu yake ya awamu ya 6, muhula wake wa kwanza. This is my early warning and a benefit of any doubt!
Kisayansi, ufuatiliaji na tathmini (M&E) hufanyika baada ya vitendo (actions) na/au utekelezaji (implementation), siyo baada ya appointment!
Narudia tena, kwa sasa tusije tukashangilia, tukahukumu, tukahofu au tukawa na matarajio makubwa; tuvute subira, matendo yaseme, si maneno matamu ya jukwaani au uteuzi.