Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wake wa kwanza Ikulu. Gerson Msigwa atolewa Ikulu, Dotto James ahamishwa. TPA, TCRA na TRA zapata wakuu wapya

Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wake wa kwanza Ikulu. Gerson Msigwa atolewa Ikulu, Dotto James ahamishwa. TPA, TCRA na TRA zapata wakuu wapya

Huyu kijana hapana.
Uzoefu wake mkubwa ni UVCCM!
Hili ni furushi la samadi ya mbolea mbichi.
Zama hizi mpya, bado mama Samia anakwenda kuokoteza makada wa CCM ambao wengi wao ni mitindio wa ubongo!
Jamaa kasoma project planning and community development....hana background yoyote ya mafuta na gasi wala madini...kwanza hajawahi kuajiriwa zaidi ya kuwa kada wa UVCCM.
 
Hatimaye Mataragio karudishwa tena kwenye nafasi yake, hongera mama Samia umetenda vyema...

Mamoderator wa JF muwe mnaachia nyuzi zenye afya zisimame kivyake, sio mnafuta futa tu au kuunga nyuzi...
 
Mama anayumbishwa sana haiwezekani apelekewe majina naye asaini tu kuna shida mahali kwenye recruitment team yake...
Ila na uhakika kwa kiasi fulani kajifunza kitu.
Yeye ndio mkuu, macho yote kwake, akiboronga sio wateuzi wake bali ni yeye! Awe mwangalifu sana na anaowategemea kwenye haya mambo.
 
Acheni udini jamani.
Mlitaka Mh. Samia ateuwe waislaam tupu nfo mfurahi
Hakuna mdini ila penye haki ionekane haki mm si muislamu ila ninapoona kuna sehemu inafanyika dhuluma lazima isemwe hakuna haki ya 80% to 20% hata kidogo tena kwa nyakati hizi ambazo wote ni wasomi rabda wangesema hawa hawajasoma hapo sawa lakini wamesoma nini kinazuia sasa?
 
Tanzania kuna fitna na majungu Sana. Yaani unatengenezewa kashfa mpaka watu wanaamini ni kweli. Kumbe chuki binafsi tu. Mimi nilishafanyiwa fitna, nikatengenezewa chuki ambayo ilisababisha Mimi kupoteza mali yangu yote. Mpaka SASA imeathiri hali yangu ya uchumi na maisha.
WATU WAELEWE RAISI NI TAASIS. HAWEZ KUFANYA KAZI KWA MIHEMKO AMA TAARIFA ZA MITANDAONI. MH. RAISI ANA TAARIFA SAHIHI KUMUHUSU DOTTO KULIKO MTU YEYOTE YULE. RAISI HAWEZ PANGIWA KUFANYA TEUZI ZAKE NA WHISTLE BLOWERS.
Kweli kabisa.
 
Mkurugenzi wa TPDC ni nafasi kubwa na nyeti sana. Mteule hakustahili hata unaibu ukurugenzi. Siasa zisitutumbukize shimoni.
Amtafutie UDas utamfaa zaidi apambane huko kwanza TPDC ni kampuni kubwa yenye kubeba interest za nchi sio nafasi za ukada....jamaa anaenda kupambana na kampuni kubwa kama TOTAL, EXXON, BP , SHELL ambayo yameniaamarusha.
 
Bandari pia inataka mkurugenzi ambaye anajua masuala ya bandari na biashara za meli.
Hii nayo ni sekta nyeti na inahusika sehemu kubwa kuingiza pato la taifa.
 
Wasaidizi wa Rais jitahidini kumpa Mama taarifa sahihi kuepuka usumbufu huu wa kutengua kabla ya kuapisha
 
Bandari pia inataka mkurugenzi ambaye anajua masuala ya bandari na biashara za meli.
Hii nayo ni sekta nyeti na inahusika sehemu kubwa kuingiza pato la taifa.
Kwani Erick Hamis amesoma nini baada ya degree ya kwanza? Najua degree yake ya kwanza ni Sociology ila huenda alijiendeleza na degree nyingine maana amekuwa pia banker na insurer kwa muda kabla ya mambo ya usafiri wa majini.
 
Ndugu Rais amefanya uamuzi sahihi na wa wakati kumrejesha mbobezi Dr. James Mataragio TPDC. Chini ya Dr. Mataragio, sekta muhimu ya Petroli, mafuta na gesi ipo mikono salama.

Serikali iendelee kupokea maoni kutoka kwa raia wake, kwa maana, hakuna mwenye haki miliki ya ukweli.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Naomba sana, tena sana; tusishangilie kabla ya kujua utendaji wa wateule wapya. Tuwe na subira, pengine nao wana maovu yao, hao si malaika! Tukumbuke hata tengua-teua ya Magufuli tulishangilia sana na ufisadi ukaendelea kama kawaida TAMISEMI, Benki Kuu, bandarini na kwingineko kwingi.

Usifurahie uteuzi, furahia ufanisi wa mtu baada ya kuanza kazi. Tutulie wakati huu Rais anapanga safu yake ya awamu ya 6, muhula wake wa kwanza. This is my early warning and a benefit of any doubt!

Kisayansi, ufuatiliaji na tathmini (M&E) hufanyika baada ya vitendo (actions) na/au utekelezaji (implementation), siyo baada ya appointment!

Narudia tena, kwa sasa tusije tukashangilia, tukahukumu, tukahofu au tukawa na matarajio makubwa; tuvute subira, matendo yaseme, si maneno matamu ya jukwaani au uteuzi.
 
Back
Top Bottom