Mwisho wa utawala wa chama cha siasa - CCM katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikuwa iwe wakati wa u Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete (2005 - 2010). Ukacheleweshwa kwa kitambo kidogo lakini maandalizi muhimu yakafanyika chini yake.
Kwa ulaghai na kwa udanganyifu wa kidola ktk uchaguzi mkuu wa 2015, wakaponea chupuchupu, wakaendelea kupumua.
Akamtengenezea njia Rais Hayati John P. Magufuli. Akaja na kauli za uharibifu na ubinafsi kama; "utawala wa CCM ya Magufuli" na "Tanzania ya Magufuli"
Huyu akaharibu mifumo ya utendaji ndani ya chama chake. Akaharibu pia mifumo ya utendaji ndani ya Serikali. Na kweli nchi hii ikawa "CCM na Tanzania ya Magufuli kwelikweli" isiyojali sheria wala katiba ya nchi.
Hakuweza kuelewa kuwa UOVU haujawahi kuishinda HAKI. Hakuwa kujua kuwa GIZA halijawahi kuitawala NURU.
Sasa tunaye mwanamama, Samia Suluhu Hassan aliyerithi mikoba ya uharibifu ya kichama na kiserikali ya Mwendazake John P. Magufuli.
Huyu ndiye alama ya mwisho ya anguko la Chama Cha Mapinduzi - CCM na utàwala ktk JMT. Ndiyo inaweza kuwa mwisho wa muungano laghai wa 1964 kati ya zilizokuwa nchi huru mbili za Tanganyika na Zanzibar.
Huyu atakuwa Rais wa kwanza mwanamke kutawala Tanzania na ndiye atakuwa Rais wa mwisho toka CCM kuiongoza Tanzania na ndiyo mwisho wa maisha ya Chama Cha Mapinduzi - CCM.
Alama za majira na nyakati ziko wazi sana kuhusu uthibitisho wa hoja hii:
1. KIFO CHA RAIS JOHN P. MAGUFULI
Sijadili kifo chake kilivyokuwa na sababu zake. Lakini ningependa kila mtu afahamu kuwa si cha bahati mbaya. Ni "call" muhimu, kwamba, tuko mwisho na Tanzania na Watanzania wanakwenda kuanza MAJIRA na NYAKATI mpya kabisa katika nchi yao.
Mwenye akili na asome na kufahamu haya.
2. UJIO WA RAIS WA JMT MWANAMKE
Si kawaida. Hakujiandaa. Hakudhani kuwa atakuwa. Haijalishi tunalionaje. Lakini ni tukio lenye kusudi maalumu ktk utawala wa nchi hii. Hakukubalika kwa kirahisi na kwa haraka ndani ya "deep state" na ndani ya CCM kwa sababu ya "conflict of interests" kati ya makundi mbalimbali.
Hawakumwona kuwa anaweza. Zipo sababu nyingine kama nitakavyoeleza hapa chini.Haya hayakutokea kwa bahati mbaya. Lipo kusudi na linakwenda kutimizwa sawia kitambo si kirefu.
3. UDHAIFU WA KATIBA YA JMT KUHUSU TRANSITION OF POWER IWAPO RAIS ALIYEKO MADARAKANI ANAKUFA AU KUKOSA UWEZO WA KUONGOZA NCHI:
Unaanza na upatikanaji wa "mgombea mwenza" ambaye automatic huwa Rais wa nchi mara litokeapo tukio la kifo au incumbent president kushindwa kutimiza wajibu wake kama inavyoelezwa na katiba ya JMT ya 1977.
Ukweli wa hili umethibitishwa na kifo cha John P. Magufuli na harakati za nani awe Rais badala yake. Udhaifu huu wa kikatiba siyo wa bahati mbaya. Ni ili kusudi la Mungu litimie na litatimia.
4. TANZANIA BARA KUONGOZWA NA RAIS MZANZIBARI WA UPANDE WA PILI WA MUUNGANO:
Hili linaweza na siku zote huonekana kuwa mwiko kuandikwa na kusemwa. Lakini ili tupone, ni sharti lijadiliwe kwa UKWELI na UWAZI. Hili haliko sawa. Halijakaa sawa. Haliatendei haki Watanganyika.
Na kiuhalisia, chanzo chake ni ASILI YA MUUNGANO mwenyewe. Kwamba, muungano kati ya nchi huru hizi mbili Tanganyika na Zanzibar, asili yake si watu au wananchi wenyewe. Huu ni muungano ulioasisiwa na viongozi kwa manufaa ya kisiasa ya viongozi wenyewe.
Ndani ya Chama kinachoongoza serikali (CCM) hawakubaliani na hili. Nje ya CCM wengi wetu, hatukubaliani na hili...
Tanganyika (Tanzania Bara) ina population kubwa sana ya karibu au zaidi ya watu 60,000,000. Zanzibar sehemu ya pili ya Muungano ina population ya watu wasiozidi 2,000,000.
Kuwa na kiongozi mkuu wa nchi kutoka Zanzibar halafu atawale Tanganyika, it is absolutely not right and unacceptable.
Unaweza kulazimisha na kudanganya watu kwa nyakati fulani. Lakini haiwezi kuwa hivyo nyakati zote.
Sababu hii ndiyo ilitaka kuleta mtafuruku wa kutaka kuvunjwa kwa katiba ya JMT na kisha muungano kwa baadhi ya Watanganyika ndani ya serikali na CCM kutaka kukataa kumpa u Rais mama Samia S. Hassan sawasawa na katiba inavyoelekeza.
Hii ni ishara (signal) muhimu ya udhaifu wa Muungano huu na unaithibitisha hoja hii sawia.
Sasa hili haliko kwa bàhati mbaya. Lipo kwa kusudi maalumu tangu wakati ule ili kutimizwa kwa mwisho wa majira na nyakati hizi na kuanza majira na nyakati mpya za utawala wa nchi hii.
5. KUIBUKA KWA KASI TENA YA AJABU KWA SAUTI ZA UPINZANI:
Kufa kwa Magufuli hakukutokea tu kwa sababu alistahili kufa. Lakini ilikuwa lazima afe ili haya yatokee. Mwendazake Magufuli aliandaa na kutengeneza upinzani na huu ndiyo kisu kibaya. Huyu mama hawezi kukabiliana na wimbi la kelele hizi za mabadiliko na akabaki salama bila yeye kuanguka anguko kuu.
Wasichofahamu CCM ni kuwa upinzani huu ni wa aina yake. Haujawahi kuwepo tangu mwaka 1992. Unaanzia ndani ya CCM yenyewe na kushika kasi huku nje. Utabiri wa Nyerere J. K miaka karibu 30 iliyopita unatimia mdogo mdogo.
Hili halikuja kwa bahati mbaya. Linakuja ili kusudi la mabadiliko ya kiutwala wa nchi litimie.
CCM INAWEZA KUCHELEWESHA KWA KITAMBO KIDOGO MWISHO WAKE:
Nawashangaa ni kwanini wanapingana na kelele za harakati za mabadiliko ya katiba ya JMT ya 1977. Kwa hili, hawa ndugu zetu mtu aweza kusema bila shaka yoyote kuwa hawana akili, busara wala maarifa
Ndo kusema kuwa, wanaweza kulainisha wimbi la kelele za madai ya KATIBA MPYA YA WANANCHI kwa kukubali kwanza kufanya amendments kadhaa ili ku accommodate baadhi ya sensitive issues kulingana na mahitaji ya nyakati na majira.
Kushupaza shingo na kujaribu ku - opt "violence means" ili kuzima sauti hizi za kudai mabadiliko ya kiuongozi na utawala wa nchi hii, ni ku - speed anguko lao na bado wanalolikataa sasa likafanyika wakiwa nje.
Bado wako ndani. Watumie kikamilifu kanuni ya GIVE and TAKE. Wakubali kubaki na kidogo na pia kupoteza kidogo. Kama wanataka yawe yao yote, wakae tayari kupoteza yote.
Hapana japo unaelekea kidogo ,anguko la ccm bado kidogo ila chadema watapata wabunge wengi kwa 2025 na jimbo moja karibu na magu kama unaenda mara kabla hujavuka msoma litaenda chadema.
Ukiona hivo ifikapo 2035 ccm itapumzika na haitainuka tena.
lakini iko hvo tu kwa sababu yeye ajaye kuanzia huo mda ni mtawala wa taifa na dunia nzima ambaye siri zote za Mungu na biblia yaani neno la mungu limefunuliwa kwake
Na tuyaonayo hayo basi tujue mtu huyo atakuja kufufuka baada ya siku tatu akisha kuzikwa kwa heshima kama mkuu wa nchi lakini yote hayo ili majira yabadilike na watu wote turudi kwa mungu ,
yeye ndo anatuletea uzima wa milele kwa kizazi hiki na kijacho,
Mapito yake ni kama inavyosema isaya 53
Yaani mtu wa huzuni nyingi ,ajuaye sikitiko na hana uzuri mpaka tumtamani ,aliyevumilia maneno mabaya na watu waliomtendea mabaya akiwajibu kwa kuwaombea na kumwachia Mungu lakini yeye ataleta haki yote duniani juu ya watawala
na danieli 2,39 yaani ataupata ubunge theni atakuwa mkuu wa nchi na dunia yote kama alivyo ahidiwa na Mungu kwa neno la danieli lile la sanamu ya mfalme nebukadneza huku akiongozwa na roho wa Mungu kuujua mda wote wa majira ya utimilifu wa kutabiriwa kwake mwaka 2012 akirishudia kwa wenzake sehemu mbalimbali na kuhusu fimbo ya Kristo yeye ndo kapewa na akiwashuhudia wenzake juu ya unabii wake alivyotabiriwa na utimilifu wa neno hilo huku akiwashuhudia wenzke darasani.
,Ana nguvu alizopewa na Mungu kwa neno la kristo kama inavyosema timotheo 1,1.12-19.
Ni yule ambaye bahati bukuku anamuongelea kwenye wimbo wake wa NANI AITIKISE tz na DUNIA AU NABII ALIYETABILI KIFO CHA MAGUFULI ALIVYOSEMA KUHUSU KUSUDI LA KUFA MAGUFULI yaani ili akitwae kiti hicho kidogo na badae kile kiti kikuu baada ya miaka 10 yaani ni ahadi kutoka kwa Mungu mkuu kusudi dunia irudi kwa Mungu.
Yote hayo yamefunuliwa kwake kabla na kote ameyasema tena kapitia mapito hayo magumu ya kuwa kinyume na watu wenzake yaani aibu sana usoni kwake yaani kaibeba lawama yote kutoka kwa watu wengi Kama alivyotabiriwa huko nyuma.
Kwa sasa kaimarika na uwezo wa kimungu kapewa na yeye ndiye aliyenenwa na kitabu cha yohana kuhusu ahadi ya Mungu baada ya kristo masihi wa israel kuwepo kwetu ila katoka kwa Mungu na kristo Kamwachia njia zake zote na atanena yale ya kristo , atayanena ya watu wote wa dunia yote kutoka kwa Mungu na YEYE ANEKUJA ILI TURUDI KWA MUNGU.
MUNGU NI PENDO.
Well come 2035, dunia haina mwisho ila majira yatabadilika baada ya kufufuka kwake.