Rais Samia Suluhu Hassan: Alama ya mwisho ya anguko la Utawala wa CCM, Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan: Alama ya mwisho ya anguko la Utawala wa CCM, Tanzania

Mkuu matusi, kubagaza ndio mchango unaoweza kuutoa?. Mnnandika sana utumbo bila kufanya utafiti wa kuweza kufahamu tunaenda wapi.

China Urusi, Vietnam, Japan Singapore, Laos na nchi nyingi zingine zilizo kuwa za kijamaa zimebadilishwaje.

Mkubwa wewe huwezi ku-cross utabaki mpinzani na CCM watabaki kwao na hautokuwa na ukakasi. Wakati huo ukifika hautakuwa na maneno uliyo nayo leo.
Tanzania sio mali ya CCM bali ni mali ya Watanzania wenyewe, endelea kumtia moyo rais wa mwisho kutoka CCM, ila wananchi wanachukua nchi yao waliyopewa na Mungu, CCM ni ngome ya ibilisi itaangushwa na mwenye mamlaka mwenyewe.
 
😄🤣🤣🤣🤣CHADEMA hawataki kusikia ukweli huu.
Hivyi kwenye wenyeviti vya vyama vyao wameng'ang'ania ukiwapa Ikulu si watafia happy Kama kupe.
Ndio maana hatutawapa nchi kamwe. Chadema wanachotakiwa kujua ni kwamba watanzania wa sasa sio wale wa mwaka 2000, ambapo watu walikuwa wanapakizwa kwenye mafuso kwenda jangwani au kidongo chekundu kumuona Lipumba badala ya kwenda kusikiliza sera za chama.
 
Very weak Governance and power of transitional politics. But good to remain with current eyesight you have. You need to synthesis your political transition analysis for it to show the way forward.
We have two ways in order to move forward...

1. The sixty years reign of CCM politics for this beautiful nation has to go down the grave....

This is the natural principle, that each beginning has its end. No one resists the natural principle goes unpunished...!

Foolishly and unknowingly its consequences, you are resisting the nature depending on human power and conscience...

2. The ruling CCM party and Madam President of URT ndugu, Samia Suluhu Hassan can a little bit make delayment for this to happen soon...

Unfortunately for them is that, they are totally obsessed with what they eat, drink and enjoy today while their tomorrow is no where to be seen..!!

It's sorrowful that the fire is burning towards their entrance. Who can save them...?

Hopefully, you got me..

NB:
For reference, you can read again and again my main topic...
 
Kuna harufu/upepo wa mabadiliko ya kisiasa hapa Afrika mashariki.
Uganda wameshamchoka mu7, Kenya mzee Jomo aliacha warithi watatu na Uhuru ndio anamalizia hivyo, Burundi inaitegemea ccm, Kagame hatakuwa na option atakapojikuta amezungukwa na majirani wageni kabisa, DRC sijui lakini lazima itapata effect kwa kiasi fulani, n.k.
Muingiliano wa mataifa ya Afrika na mataifa yenye nguvu ulimwenguni nao upo katika hali ya mabadiliko.
 
Kuna harufu/upepo wa mabadiliko ya kisiasa hapa Afrika mashariki.
Uganda wameshamchoka mu7, Kenya mzee Jomo aliacha warithi watatu na Uhuru ndio anamalizia hivyo, Burundi inaitegemea ccm, Kagame hatakuwa na option atakapojikuta amezungukwa na majirani wageni kabisa, DRC sijui lakini lazima itapata effect kwa kiasi fulani, n.k.
Muingiliano wa mataifa ya Afrika na mataifa yenye nguvu ulimwenguni nao upo katika hali ya mabadiliko.
Heri yako wewe unayaona mambo katika jicho angavu la tatu...

Shauri lao ambao bado wanatumia macho mawili yaleyale ya toka mwaka 1961 au 1964 kuzitazama siasa za dunia ya Leo...

Hawa ufahamu wao umefunikwa na EGO na PRIDE zao zenye kufisha na kuangamiza...
 
The devil is always a liar...!

Who the hell do you think you are to say these words..?

Shameful ending is coming for you. You will surely swallow these words...
Mlipanga kuitafuna nchi, matokeo yake nchi imewatafuna nyie. Mwenyekiti kameza hela zote zilizochangishwa kwenye kampeni. Je tukiwapa nchi hazina itasalimika kweli?

2528007_20200919_173148.jpg
 
Kufa CCM siyo leo kama wapinzani wenyewe was hivyo, hoja matusi tu, mara tuandamane. WaTZ walishajifunza kwenye mataifa yanayofanya siasa za nguvunguvu wakaona matokeo yake hivyo hawawezi kujiingiza kwenye siasa za matusi na maneno makali.
Asante kwa maoni yako..

Lakini ni wazi kuwa, huna uhakika au hujui kabisa usemalo...

Na ni kwa sababu hujui historia na siasa za dunia ya leo...

Bado unayatazama mambo katika jicho la "utamaduni wa mazoea" ya kusikia au kuambiwa...

Yatazame mambo ktk jicho la tatu tena likiwa angavu, utaona mambo ya ajabu sana yatakayobadilisha ufahamu wako...
 
Mlipanga kuitafuna nchi, matokeo yake nchi imewatafuna nyie. Mwenyekiti kameza hela zote zilizochangishwa kwenye kampeni. Je tukiwapa nchi hazina itasalimika kweli?

View attachment 1843222
Kumbe wewe ni mtoto kwelikweli...

Huwezi kujadili hii mada...

Mimi siko interested kutazama au kuangalia komedi..

Asante
 
Tungekuwa na upinzani makini hayo unayofikiria labda yangewezekana. Lakini kwa bahati mbaya hatuna chama cha upinzani wala mpinzani wa kweli.

Sabodo alimkabidhi mwenyekiti wa chadema mamilioni ya shilingi ili ajenge ofisi za chama na kuchimba visima katika maeneo mbali mbali ya nchi, kwa lengo la kuwavuta watu wajiunge na chama lakini matokeo yake mwenyekiti akatumia mamilioni yale kwenda kula bata na wema sepetu dubai, na aliporudi kutokana na nguvu alizonazo ndan ya chama hakuna mtu aliefungua kinywa chake kumuuliza chochote kuhusiana na mamilioni aliyotafuna.

Kama hiyo haitoshi mwenyekiti na genge lake wakaja na plan ya kuwachangisha wabunge kila mwezi. Wabunge wakachangia chama kwa kipindi cha miaka mitano lkn mpaka leo hawajui hela hizo zimekwenda wapi na hapo hatujazungumzia ruzuku ya chama iliyokuwa inapokea wakati wa utawala wa Kikwete na Magufuli, hela za michango wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, bado misaada ya mamilioni kutoka kwa wafadhili wa chama kule ulaya.

Zote hizi zinatafunwa na mwenyekiti pamoj na genge lake la kumtetea hapa mitandaoni ili kufunika mabaya yake na ya chama kwa ujumla. Lipumba, Zito na Mbatia hawa ndo tunawatumia tutakavyo kudhoofisha upinzani nchini. Kifupi hakuna upinzani wa kuitoa CCM madarakan labda miaka 40 ijayo. Baada ya hawa wenyeviti wachumia matumbo kustaafu siasa au kutoka kweny nafasi zao.
Chama cha Ukoo kichukue nchi, uliona wapi....
 
Zanzibar na Tanganyika ni nchi moja..toeni kauli zenu za utenganishi kwa kuchuchumilia madarakaa...hakuna kitu kama hichoo..huu muungano ni wa moja kwa moja..wala msitegemee chochoteee...hayo madaraka mnayoyalilia hamtakaa muyapatee hakikaa
Sijaelewa ni kitu gani kumekufanya ung'ake...

Halafu mimi siko huko unakofikiria wewe...

Sijawahi kutamani madaraka ya uongozi na nchi...

Mimi ni raia wa kawaida sana ambaye sijulikani CCM, CHADEMA au chama chochote cha siasa zaidi ya hapa JF...

Tunajadili mstakabali wa nchi yetu. Na harakati zetu tunazifanya kwa mwavuli wa "undercover". Huwezi kutujua kwa sura, lakini tupo...

Katika kujadili huwezi kukwepa kuitaja CCM , Rais Samia Hassan na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar...
 
Mkuu acha tujipe muda ili hio siku ikifika wote tushuhudie utabiri wako.... Mungu atupe umri mrefu wa kwetu na wa Babu zetu ili tushuhudie hayo ulosema.

Nitaomba mnikumbushe.

Asante
 
Labda tujaribu kufahamu mambo mawili muhimu...

1. Ally H. Mwinyi (Mzanzibari) 1985 - 1995 akiwa Rais wa JMT takribani miongo mitatu (miaka 30) iliyopita, uelewa na ufahamu wa kizazi kile ni tofauti na uelewa na ufahamu wa kizazi cha sasa. Hiki ni kizazi kilichokuwa gizani. Kiliamini chochote cha kuambiwa na viongozi kina Nyerere J K....

Kizazi cha leo (kina sisi) ni cha kuhoji maswali magumu ya WHY? WHEN? HOW? nk. Ukishindwa kutoa majibu sahihi, hawawezi kukuacha, watakuwa na wewe mpaka utoe majibu sahihi ya maswali yao na waridhike. Vinginevyo, ukiishi kwa ulaghai na udanganyifu, viongozi wajiandae kuwashiwa moto...!!

Hiki ni kizazi cha maendeleo ya teknolojia ya habari. Hiki ni kizazi cha dot.com. Kinaona kila kinachoendelea ktk nchi yao na huko duniani..

2. Nimejadili utawala wa Samia Suluhu Hassan na hatima ya CCM katika context pana nikijaribu kumfungua macho ya msomaji aone mwisho wa dola ya CCM unavyoonekana kwa karibu ukija....

Upole au busara za Rais Samia Suluhu hazina uhusiano na anguko la CCM na hizo kamwe haziwezi kuuzuia mwisho huo...

Wakati umeshawadia. Samia Suluhu yupo hapo kutimiza kusudi bila kujali ana haiba gani...

I am speaking boldly with full authority, kuwa kusudi la mwisho wa CCM ni lazima litimie na litatimia kitambo kifupi kijacho....

Rais Samia Suluhu Hassan is just a tool or an instrument for making sure that the prophecy is fulfilled..!!
Katika hali ya kawaida,kama Magufuli angeongoza vizuri,watanzania bara wasingekubali kabisa kuongozwa na raisi mzanzibari. Wengi tulijua Mwinyi alikuwa wa mwisho.

Kwa bahati mbaya,Magufuli alikuwa mtawala mbaya ambaye amesababisha watanzania bara wamchukulie Samia kama mkombozi. Kutokana na hofu ya masalia ya Magufuli serikalini,watanzania wengi,wako tayari kuongozwa na wazanzibar,i angalau kwa sasa,mpaka watakapoamini kwamba masalia ya Magufuli yamemalizika serikalini ili nchi isirudi kwenye utawala wa hovyo wa awamu ya Magufuli.
 
Mwisho wa utawala wa chama cha siasa - CCM katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikuwa iwe wakati wa u Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete (2005 - 2010). Ukacheleweshwa kwa kitambo kidogo lakini maandalizi muhimu yakafanyika chini yake.

Kwa ulaghai na kwa udanganyifu wa kidola ktk uchaguzi mkuu wa 2015, wakaponea chupuchupu, wakaendelea kupumua.

Akamtengenezea njia Rais Hayati John P. Magufuli. Akaja na kauli za uharibifu na ubinafsi kama; "utawala wa CCM ya Magufuli" na "Tanzania ya Magufuli"

Huyu akaharibu mifumo ya utendaji ndani ya chama chake. Akaharibu pia mifumo ya utendaji ndani ya Serikali. Na kweli nchi hii ikawa "CCM na Tanzania ya Magufuli kwelikweli" isiyojali sheria wala katiba ya nchi.

Hakuweza kuelewa kuwa UOVU haujawahi kuishinda HAKI. Hakuwa kujua kuwa GIZA halijawahi kuitawala NURU.

Sasa tunaye mwanamama, Samia Suluhu Hassan aliyerithi mikoba ya uharibifu ya kichama na kiserikali ya Mwendazake John P. Magufuli.

Huyu ndiye alama ya mwisho ya anguko la Chama Cha Mapinduzi - CCM na utàwala ktk JMT. Ndiyo inaweza kuwa mwisho wa muungano laghai wa 1964 kati ya zilizokuwa nchi huru mbili za Tanganyika na Zanzibar.

Huyu atakuwa Rais wa kwanza mwanamke kutawala Tanzania na ndiye atakuwa Rais wa mwisho toka CCM kuiongoza Tanzania na ndiyo mwisho wa maisha ya Chama Cha Mapinduzi - CCM.

Alama za majira na nyakati ziko wazi sana kuhusu uthibitisho wa hoja hii:

1. KIFO CHA RAIS JOHN P. MAGUFULI

Sijadili kifo chake kilivyokuwa na sababu zake. Lakini ningependa kila mtu afahamu kuwa si cha bahati mbaya. Ni "call" muhimu, kwamba, tuko mwisho na Tanzania na Watanzania wanakwenda kuanza MAJIRA na NYAKATI mpya kabisa katika nchi yao.

Mwenye akili na asome na kufahamu haya.

2. UJIO WA RAIS WA JMT MWANAMKE

Si kawaida. Hakujiandaa. Hakudhani kuwa atakuwa. Haijalishi tunalionaje. Lakini ni tukio lenye kusudi maalumu ktk utawala wa nchi hii. Hakukubalika kwa kirahisi na kwa haraka ndani ya "deep state" na ndani ya CCM kwa sababu ya "conflict of interests" kati ya makundi mbalimbali.

Hawakumwona kuwa anaweza. Zipo sababu nyingine kama nitakavyoeleza hapa chini.Haya hayakutokea kwa bahati mbaya. Lipo kusudi na linakwenda kutimizwa sawia kitambo si kirefu.

3. UDHAIFU WA KATIBA YA JMT KUHUSU TRANSITION OF POWER IWAPO RAIS ALIYEKO MADARAKANI ANAKUFA AU KUKOSA UWEZO WA KUONGOZA NCHI:

Unaanza na upatikanaji wa "mgombea mwenza" ambaye automatic huwa Rais wa nchi mara litokeapo tukio la kifo au incumbent president kushindwa kutimiza wajibu wake kama inavyoelezwa na katiba ya JMT ya 1977.

Ukweli wa hili umethibitishwa na kifo cha John P. Magufuli na harakati za nani awe Rais badala yake. Udhaifu huu wa kikatiba siyo wa bahati mbaya. Ni ili kusudi la Mungu litimie na litatimia.

4. TANZANIA BARA KUONGOZWA NA RAIS MZANZIBARI WA UPANDE WA PILI WA MUUNGANO:

Hili linaweza na siku zote huonekana kuwa mwiko kuandikwa na kusemwa. Lakini ili tupone, ni sharti lijadiliwe kwa UKWELI na UWAZI. Hili haliko sawa. Halijakaa sawa. Haliatendei haki Watanganyika.

Na kiuhalisia, chanzo chake ni ASILI YA MUUNGANO mwenyewe. Kwamba, muungano kati ya nchi huru hizi mbili Tanganyika na Zanzibar, asili yake si watu au wananchi wenyewe. Huu ni muungano ulioasisiwa na viongozi kwa manufaa ya kisiasa ya viongozi wenyewe.

Ndani ya Chama kinachoongoza serikali (CCM) hawakubaliani na hili. Nje ya CCM wengi wetu, hatukubaliani na hili...

Tanganyika (Tanzania Bara) ina population kubwa sana ya karibu au zaidi ya watu 60,000,000. Zanzibar sehemu ya pili ya Muungano ina population ya watu wasiozidi 2,000,000.

Kuwa na kiongozi mkuu wa nchi kutoka Zanzibar halafu atawale Tanganyika, it is absolutely not right and unacceptable.

Unaweza kulazimisha na kudanganya watu kwa nyakati fulani. Lakini haiwezi kuwa hivyo nyakati zote.

Sababu hii ndiyo ilitaka kuleta mtafuruku wa kutaka kuvunjwa kwa katiba ya JMT na kisha muungano kwa baadhi ya Watanganyika ndani ya serikali na CCM kutaka kukataa kumpa u Rais mama Samia S. Hassan sawasawa na katiba inavyoelekeza.

Hii ni ishara (signal) muhimu ya udhaifu wa Muungano huu na unaithibitisha hoja hii sawia.

Sasa hili haliko kwa bàhati mbaya. Lipo kwa kusudi maalumu tangu wakati ule ili kutimizwa kwa mwisho wa majira na nyakati hizi na kuanza majira na nyakati mpya za utawala wa nchi hii.

5. KUIBUKA KWA KASI TENA YA AJABU KWA SAUTI ZA UPINZANI:

Kufa kwa Magufuli hakukutokea tu kwa sababu alistahili kufa. Lakini ilikuwa lazima afe ili haya yatokee. Mwendazake Magufuli aliandaa na kutengeneza upinzani na huu ndiyo kisu kibaya. Huyu mama hawezi kukabiliana na wimbi la kelele hizi za mabadiliko na akabaki salama bila yeye kuanguka anguko kuu.

Wasichofahamu CCM ni kuwa upinzani huu ni wa aina yake. Haujawahi kuwepo tangu mwaka 1992. Unaanzia ndani ya CCM yenyewe na kushika kasi huku nje. Utabiri wa Nyerere J. K miaka karibu 30 iliyopita unatimia mdogo mdogo.

Hili halikuja kwa bahati mbaya. Linakuja ili kusudi la mabadiliko ya kiutwala wa nchi litimie.

CCM INAWEZA KUCHELEWESHA KWA KITAMBO KIDOGO MWISHO WAKE:

Nawashangaa ni kwanini wanapingana na kelele za harakati za mabadiliko ya katiba ya JMT ya 1977. Kwa hili, hawa ndugu zetu mtu aweza kusema bila shaka yoyote kuwa hawana akili, busara wala maarifa

Ndo kusema kuwa, wanaweza kulainisha wimbi la kelele za madai ya KATIBA MPYA YA WANANCHI kwa kukubali kwanza kufanya amendments kadhaa ili ku accommodate baadhi ya sensitive issues kulingana na mahitaji ya nyakati na majira.

Kushupaza shingo na kujaribu ku - opt "violence means" ili kuzima sauti hizi za kudai mabadiliko ya kiuongozi na utawala wa nchi hii, ni ku - speed anguko lao na bado wanalolikataa sasa likafanyika wakiwa nje.

Bado wako ndani. Watumie kikamilifu kanuni ya GIVE and TAKE. Wakubali kubaki na kidogo na pia kupoteza kidogo. Kama wanataka yawe yao yote, wakae tayari kupoteza yote.
Uko sahihi. "Social and political reforms are in making. Behold".
 
Umejaza pumba tu, sioni wa kuitoa CCM kwa sasa.Kwa Vyama vilivyoko sasa hakuna, vyama vilivyojaa wahuni, wabinafsi na wakabila kama mbowe,zitto, mbatia na lipumba ndio viitoe CCM? Acha kuchekesha wewe
 
Kwa hiyo mkuu unaamini kabisa aliyekuwa anaizamisha CCM ni JPM na ndio ilikuwa inaelekea kufa ?

Nope. Maana takwimu tu zinakataa. Kipindi cha JPM wapinzani wamepungua na upinzani ulipoa kabisa. Ushahidi ni bunge la sasa.
Kwa siasa za kigaidi za jpm ulitarajia matokeo gani?

Unadhani unaweza kuendesha utawala wa aina ya Magufuli na watu wakatulia na kukuacha ufanye upendavyo. Lilikuwa ni suala la muda tu.. .. hatimae uasi ungetamaliki kila kona.

Kwa hiyo,wewe unaona jpm aliimarisha CCM? Kama huo ndio mtazamo wako ni vigumu kukuelewesha ukaelewa!
 
Back
Top Bottom