Rais Samia Suluhu Hassan: Alama ya mwisho ya anguko la Utawala wa CCM, Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan: Alama ya mwisho ya anguko la Utawala wa CCM, Tanzania

Mwisho wa utawala wa chama cha siasa - CCM katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikuwa iwe wakati wa u Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete (2005 - 2010). Ukacheleweshwa kwa kitambo kidogo lakini maandalizi muhimu yakafanyika chini yake.

Kwa ulaghai na kwa udanganyifu wa kidola ktk uchaguzi mkuu wa 2015, wakaponea chupuchupu, wakaendelea kupumua.

Akamtengenezea njia Rais Hayati John P. Magufuli. Akaja na kauli za uharibifu na ubinafsi kama; "utawala wa CCM ya Magufuli" na "Tanzania ya Magufuli"

Huyu akaharibu mifumo ya utendaji ndani ya chama chake. Akaharibu pia mifumo ya utendaji ndani ya Serikali. Na kweli nchi hii ikawa "CCM na Tanzania ya Magufuli kwelikweli" isiyojali sheria wala katiba ya nchi.

Hakuweza kuelewa kuwa UOVU haujawahi kuishinda HAKI. Hakuwa kujua kuwa GIZA halijawahi kuitawala NURU.

Sasa tunaye mwanamama, Samia Suluhu Hassan aliyerithi mikoba ya uharibifu ya kichama na kiserikali ya Mwendazake John P. Magufuli.

Huyu ndiye alama ya mwisho ya anguko la Chama Cha Mapinduzi - CCM na utàwala ktk JMT. Ndiyo inaweza kuwa mwisho wa muungano laghai wa 1964 kati ya zilizokuwa nchi huru mbili za Tanganyika na Zanzibar.

Huyu atakuwa Rais wa kwanza mwanamke kutawala Tanzania na ndiye atakuwa Rais wa mwisho toka CCM kuiongoza Tanzania na ndiyo mwisho wa maisha ya Chama Cha Mapinduzi - CCM.

Alama za majira na nyakati ziko wazi sana kuhusu uthibitisho wa hoja hii:

1. KIFO CHA RAIS JOHN P. MAGUFULI

Sijadili kifo chake kilivyokuwa na sababu zake. Lakini ningependa kila mtu afahamu kuwa si cha bahati mbaya. Ni "call" muhimu, kwamba, tuko mwisho na Tanzania na Watanzania wanakwenda kuanza MAJIRA na NYAKATI mpya kabisa katika nchi yao.

Mwenye akili na asome na kufahamu haya.

2. UJIO WA RAIS WA JMT MWANAMKE

Si kawaida. Hakujiandaa. Hakudhani kuwa atakuwa. Haijalishi tunalionaje. Lakini ni tukio lenye kusudi maalumu ktk utawala wa nchi hii. Hakukubalika kwa kirahisi na kwa haraka ndani ya "deep state" na ndani ya CCM kwa sababu ya "conflict of interests" kati ya makundi mbalimbali.

Hawakumwona kuwa anaweza. Zipo sababu nyingine kama nitakavyoeleza hapa chini.Haya hayakutokea kwa bahati mbaya. Lipo kusudi na linakwenda kutimizwa sawia kitambo si kirefu.

3. UDHAIFU WA KATIBA YA JMT KUHUSU TRANSITION OF POWER IWAPO RAIS ALIYEKO MADARAKANI ANAKUFA AU KUKOSA UWEZO WA KUONGOZA NCHI:

Unaanza na upatikanaji wa "mgombea mwenza" ambaye automatic huwa Rais wa nchi mara litokeapo tukio la kifo au incumbent president kushindwa kutimiza wajibu wake kama inavyoelezwa na katiba ya JMT ya 1977.

Ukweli wa hili umethibitishwa na kifo cha John P. Magufuli na harakati za nani awe Rais badala yake. Udhaifu huu wa kikatiba siyo wa bahati mbaya. Ni ili kusudi la Mungu litimie na litatimia.

4. TANZANIA BARA KUONGOZWA NA RAIS MZANZIBARI WA UPANDE WA PILI WA MUUNGANO:

Hili linaweza na siku zote huonekana kuwa mwiko kuandikwa na kusemwa. Lakini ili tupone, ni sharti lijadiliwe kwa UKWELI na UWAZI. Hili haliko sawa. Halijakaa sawa. Haliatendei haki Watanganyika.

Na kiuhalisia, chanzo chake ni ASILI YA MUUNGANO mwenyewe. Kwamba, muungano kati ya nchi huru hizi mbili Tanganyika na Zanzibar, asili yake si watu au wananchi wenyewe. Huu ni muungano ulioasisiwa na viongozi kwa manufaa ya kisiasa ya viongozi wenyewe.

Ndani ya Chama kinachoongoza serikali (CCM) hawakubaliani na hili. Nje ya CCM wengi wetu, hatukubaliani na hili...

Tanganyika (Tanzania Bara) ina population kubwa sana ya karibu au zaidi ya watu 60,000,000. Zanzibar sehemu ya pili ya Muungano ina population ya watu wasiozidi 2,000,000.

Kuwa na kiongozi mkuu wa nchi kutoka Zanzibar halafu atawale Tanganyika, it is absolutely not right and unacceptable.

Unaweza kulazimisha na kudanganya watu kwa nyakati fulani. Lakini haiwezi kuwa hivyo nyakati zote.

Sababu hii ndiyo ilitaka kuleta mtafuruku wa kutaka kuvunjwa kwa katiba ya JMT na kisha muungano kwa baadhi ya Watanganyika ndani ya serikali na CCM kutaka kukataa kumpa u Rais mama Samia S. Hassan sawasawa na katiba inavyoelekeza.

Hii ni ishara (signal) muhimu ya udhaifu wa Muungano huu na unaithibitisha hoja hii sawia.

Sasa hili haliko kwa bàhati mbaya. Lipo kwa kusudi maalumu tangu wakati ule ili kutimizwa kwa mwisho wa majira na nyakati hizi na kuanza majira na nyakati mpya za utawala wa nchi hii.

5. KUIBUKA KWA KASI TENA YA AJABU KWA SAUTI ZA UPINZANI:

Kufa kwa Magufuli hakukutokea tu kwa sababu alistahili kufa. Lakini ilikuwa lazima afe ili haya yatokee. Mwendazake Magufuli aliandaa na kutengeneza upinzani na huu ndiyo kisu kibaya. Huyu mama hawezi kukabiliana na wimbi la kelele hizi za mabadiliko na akabaki salama bila yeye kuanguka anguko kuu.

Wasichofahamu CCM ni kuwa upinzani huu ni wa aina yake. Haujawahi kuwepo tangu mwaka 1992. Unaanzia ndani ya CCM yenyewe na kushika kasi huku nje. Utabiri wa Nyerere J. K miaka karibu 30 iliyopita unatimia mdogo mdogo.

Hili halikuja kwa bahati mbaya. Linakuja ili kusudi la mabadiliko ya kiutwala wa nchi litimie.

CCM INAWEZA KUCHELEWESHA KWA KITAMBO KIDOGO MWISHO WAKE:

Nawashangaa ni kwanini wanapingana na kelele za harakati za mabadiliko ya katiba ya JMT ya 1977. Kwa hili, hawa ndugu zetu mtu aweza kusema bila shaka yoyote kuwa hawana akili, busara wala maarifa.

Ndo kusema kuwa, wanaweza kulainisha wimbi la kelele za madai ya KATIBA MPYA YA WANANCHI kwa kukubali kwanza kufanya amendments kadhaa ili ku accommodate baadhi ya sensitive issues kulingana na mahitaji ya nyakati na majira.

Kushupaza shingo na kujaribu ku - opt "violence means" ili kuzima sauti hizi za kudai mabadiliko ya kiuongozi na utawala wa nchi hii, ni ku - speed anguko lao na bado wanalolikataa sasa likafanyika wakiwa nje.

Bado wako ndani. Watumie kikamilifu kanuni ya GIVE and TAKE. Wakubali kubaki na kidogo na pia kupoteza kidogo. Kama wanataka yawe yao yote, wakae tayari kupoteza yote.
Very weak Governance and power of transitional politics. But good to remain with current eyesight you have. You need to synthesis your political transition analysis for it to show the way forward.
 
Nakushauri haya mtu mzima wewe, kuwa;
1. Katika mijadala jitahidi sana kusoma au kusikiliza kwa makini yatokayo kwa wenzako kabla kujibu iwe kwa maandushi au mdomo. Usijaribu kuwa insensitive and dilusional for no reasons...

2. Soma katikati ya mistari tena andiko langu kuu ili upate mantiki au logic ya nilichojadili. Nimejua kuwa hukusoma au umesoma lakini hukuelewa kwa hiki ulichoandika hapa...

3. Dhana na mantiki (logic) nzima ya andiko langu imejikita katika mambo makuu mawili

å Samia Suluhu Hassan alama kuu ya anguko la utawala wa CCM baada ya miaka 60 tangu uhuru wa wa Tanganyika 1961

å Nikajaribu kujenga hoja yangu ya anguko hili kwa kuhusianisha na udhaifu wa Muungano wa 1964 kati ya nchi za Tanganyika na Zanzibar..

4. Huu ni mtazamo wangu, maoni yangu kwa kuzungatia mazingira na kinachoendelea ktk nchi yetu. Wewe sasa kama mzee uliyekomaa, badala ujenge hoja yako kunikosoa, unarusha matusi ya kitoto na kunishauri eti nikasome ujinga wa CIVICS ya Form 2 sekondari...

Kwa hili tu lime - expose weakness yako kubwa kabisa...

Sasa nimeelewa kuwa, kumbe elimu yako wewe ni ile uliyokaririshwa form 2 na unakutumia kukariri kwako katika maisha halisi...

Nakushauri achana na hiyo. Tumia hicho kidogo sana ulichokipata sekondari kuhoji ili update ufahamu zaidi...!!
Huna hoja Ila una mkusanyiko wa maneno tu uliyoyaweka pamoja.
 
Umezungumzia mengi ila hilo la mzanzibar kuitawala Tanganyika ni fikirishi zaidi, najua huwa wanampachika mzanzibar kwenye nafasi ya VP kama kielelezo cha kudumisha huu muungano, lakini kwa nini na kule Zanzibar asiwepo mtanganyika kwenye moja ya nafasi za juu serikalini ili kudumisha huo muungano?

Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania JPM, kinaweza kuwaamsha CCM next time waone kumbe inawezekana "kumpachika" kwao mzanzibar kama VP ipo siku anaweza akaja kuwa Rais accidentally bila wao kujiandaa na kusababisha misuguano ndani ya chama chao, kama wana akili watajifunza kwenye hili, na zaidi ukizingatia tofauti kubwa ya population iliyopo kati yetu na Znz.
Sasa Tanganyika inatawaliwa na Zanzibar, yote hayo yamesababishwa na katiba dhaifu iliyoandaliwa na CCM yenyewe kulinda maslahi yao
 
CCM haiwezi kuanguka kirahisi hivyo, Hilo sahau kabisa. Tena sahau sana.

CCM ni mfumo wa utawala wa nchi. CCM sio tu ni chama bali ni nchi pia. Hili kila siku kumbuka nakuomba sana.

Ki deal na CCM hakuhitajiki akili ndogo namna hv, bali akili kubwa mno.

CCM sio wepesi hivyo. Na hv sasa ndo tupo kwenye harakati za kudai reform ya chama ndo kabisa, wapinzani watapoteana mazima
Wazee ndiyo mizizi ya ccm.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kuitoa CCM madarakani ni ndoto za mchana. Wapinzani wana hoja nyepesi sana na wananchi wa kawaida ambao ndio majority hawajawahi kuwaelewa na wala hawawaungi mkono. Upinzani una nguvu mtandaoni na sio ndani ya jamii. Ninazo facts katika hili.

Namna pekee ya CCM kutoka madarakani ni Mgogoro wa ndani ya chama wa wenyewe kwa wenyewe, tena msuguano mkali utakofanya ipasuke vipande vipande.

Hata hivyo kutokana na CCM kuweka msingi imara tangu kuasisiwa mpaka leo kuwa taasisi kubwa yenye nguvu, hivyo dhana ya mgogoro utakaopelekea ipasuke inakuwa ndogo. Rejea Lowassa na Membe walivyojaribu kuivimbia CCM.

Hii ni kwa sababu hakuna aliye mkubwa ndani ya chama kama lilivyo jina la CCM. Na hakuna chama Afrika nzima kinachoheshimu katiba yake, miongozo na kanuni kama CCM.

CCM haina mwenyewe kama vilivyo vyama vya msimu. Ndio maana kiongozi mstaafu wa CCM anaheshimu uongozi uliopo hata kama aliwahi kuwa Mwenyekiti. Hii inaonesha ukomavu wa CCM.

Sikisifii sana chama tawala lakini nimejifunza mengi kwenye chama tokea nikiwa mtoto na nakifananisha na kanisa katoliki. Ni sawa na kifikiri kanisa katoliki litadhoofishwa na makanisa ya kilokole yanayoibuka yenye kumsujudu mtu mmoja (kiongozi mwanzilishi) kwa tegemeo la kuiangusha Roman empire ambayo ni taasisi iliyoshamiri kila kona.

Mleta post amka kumekucha. Ndoto za mchana sio nzuri. CCM haiwezi kung'oka kwa nadharia zako mfu.

Wrong premise. CCM haitegemei kueleweka na wananchi; inasimikwa madarakani na vyombo vya dola na taasisi zake, period. Ushindi wa CCM kwenye uchaguzi huamuliwa na mwenyekiti wa chama hicho. CCM ina uwezo hata wa kulipanga Bunge inavyotaka kama ilivyofanya Oktoba 2020 kwa kuogopa nguvu kubwa ya upinzani kisiasa.

Right kuhusu mgogoro ndani ya chama lakini wrong again kulinganisha enzi za Lowassa/Membe na za Magufuli/SSH. Magufuli alifanya MAMBO huko ccm. Alipindua status quo na kujenga himaya yake binafsi inayotisha sana. Tunaona dhahiri jinsi SSH anavyojitahidi “kunyata” katika mwendo wake kuepuka kutibua “legacy” ya mwendazake huku akijenga taswira ya “kurekebisha mambo”.

Hivyo, tumaini kuu la CCM dhidi ya “unabii” wa mleta mada ni kuhakikisha kelele za legacy ya JPM zinazimika mapema na mizigo mizito aliyolitwisha taifa inatuliwa mapema bila kuzidi kuumiza system na wananchi. Real mkingamo. Yetu macho.
 
CCM hii haina tofauti na Bokoharam, CCM hii ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala.
JamiiForums-1778114462.jpg
 
CCM hii haina tofauti na Bokoharam, CCM hii ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala.View attachment 1843097
Nasikia pia huwa wanawakamata na kuwaminya kwa pliers makende ya wapinzani wao, yaani hii ccm ni sawa na wale ma NAZI wa ujerumani walioangukia pua enzi zile, nabii kesha tabiri kuwa huwa mama ndiye rais wa mwisho kutoka CCM [emoji3][emoji3]
 
kama shetani alianguka itakuwa ccm? Uongo haujawahi kuushinda ukweli hata mara moja!
Kijana naomba nikusaidie ili kesho yako iwe ya mwanga na pia ujue unapigana na nani kisiasa.
Hii itakusaidia huenda michango yako inayofuata ikiwa ya kielimu ni sio ushabiki maandazi.

CCM IMEKAA KIVIPI .
Baada ya 2015 chama wamekigeuza kuwa National movement na siyo Chama.
CCM = Serikali kuu, Serikali za Mitaaa, Vyombo vyote vya Usalama, Jamii yote ya kipato vha Chini, wakulima, wachimba madini na sector zote za nchi za kiuchumi , kisiasa na kiutawala.

Eneo pekee ambalo hawajalishika ni wafanyabiasha na kwa hili 45% wako upande wao.

Wanachokitaka na wamejaribu na wanaelekea kufanikiwa ni kufanya CCM iwe NATIONAL CONSCIENTE

(A national consciousness is a shared sense of national identity and a shared understanding that a people group shares a common ethnic/linguistic/cultural/ economic/education background.
a rise in national consciousness has been the first step towards the creation of a nation)

ukiipinga CCM unatikisa sukari kwenye kikombe chá chai, kwa hiyo inazidi CCM kunoga.

Na hii ndio maana naamini viongozi wa sasa hivi wa vyama vya upinzani vyote hawana uwezo wanaodai wanao kufanya mabadiliko.

Mwanachama wa chama cha upinzani yupo kwa kuiimarisha CCM na aliyepo CCM yupo kwa kuimarisha CCM.

Inatakiwa muda mrefu nikuchambulie michango mitatu au minne ili uweze kuelewa vizuri.
Ndio maana vijana wa upinzani wanachanganywa CCM na vijana wa CCM wanaendelea kuwa CCM.

Hii ni operation ni ya miaka 25 , ambayo ni generation moja. Baada ya hapo ama upinzani au CCM vyote vita fanana tuu na upinzani hautokuwa tishio kwa CCM na vile vile CCM háito kuwa kikwazo kwa upinzani. wote CCM na Upinzani watakuwa wanacheza, wanapika na kula sahani moja..
 
Wrong premise. CCM haitegemei kueleweka na wananchi; inasimikwa madarakani na vyombo vya dola na taasisi zake, period. Ushindi wa CCM kwenye uchaguzi huamuliwa na mwenyekiti wa chama hicho. CCM ina uwezo hata wa kulipanga Bunge inavyotaka kama ilivyofanya Oktoba 2020 kwa kuogopa nguvu kubwa ya upinzani kisiasa.

Right kuhusu mgogoro ndani ya chama lakini wrong again kulinganisha enzi za Lowassa/Membe na za Magufuli/SSH. Magufuli alifanya MAMBO huko ccm. Alipindua status quo na kujenga himaya yake binafsi inayotisha sana. Tunaona dhahiri jinsi SSH anavyojitahidi “kunyata” katika mwendo wake kuepuka kutibua “legacy” ya mwendazake huku akijenga taswira ya “kurekebisha mambo”.

Hivyo, tumaini kuu la CCM dhidi ya “unabii” wa mleta mada ni kuhakikisha kelele za legacy ya JPM zinazimika mapema na mizigo mizito aliyolitwisha taifa inatuliwa mapema bila kuzidi kuumiza system na wananchi. Real mkingamo. Yetu macho.
Kwa hiyo mkuu unaamini kabisa aliyekuwa anaizamisha CCM ni JPM na ndio ilikuwa inaelekea kufa ?

Nope. Maana takwimu tu zinakataa. Kipindi cha JPM wapinzani wamepungua na upinzani ulipoa kabisa. Ushahidi ni bunge la sasa.
 
Umezungumzia mengi ila hilo la mzanzibar kuitawala Tanganyika ni fikirishi zaidi, najua huwa wanampachika mzanzibar kwenye nafasi ya VP kama kielelezo cha kudumisha huu muungano, lakini kwa nini na kule Zanzibar asiwepo mtanganyika kwenye moja ya nafasi za juu serikalini ili kudumisha huo muungano?

Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania JPM, kinaweza kuwaamsha CCM next time waone kumbe inawezekana "kumpachika" kwao mzanzibar kama VP ipo siku anaweza akaja kuwa Rais accidentally bila wao kujiandaa na kusababisha misuguano ndani ya chama chao, kama wana akili watajifunza kwenye hili, na zaidi ukizingatia tofauti kubwa ya population iliyopo kati yetu na Znz.
 
Kwa hiyo mkuu unaamini kabisa aliyekuwa anaizamisha CCM ni JPM na ndio ilikuwa inaelekea kufa ?

Nope. Maana takwimu tu zinakataa. Kipindi cha JPM wapinzani wamepungua na upinzani ulipoa kabisa. Ushahidi ni bunge la sasa.
Hizo takwimu zako ni figisu figisu Za vyombo vya dola. Tuliona mabegi badala kubeba nguo yakibeba kura feki
 
Kufa CCM siyo leo kama wapinzani wenyewe was hivyo, hoja matusi tu, mara tuandamane. WaTZ walishajifunza kwenye mataifa yanayofanya siasa za nguvunguvu wakaona matokeo yake hivyo hawawezi kujiingiza kwenye siasa za matusi na maneno makali.
 
Kijana naomba nikusaidie ili kesho yako iwe ya mwanga na pia ujue unapigana na nani kisiasa.
Hii itakusaidia huenda michango yako inayofuata ikiwa ya kielimu ni sio ushabiki maandazi.

CCM IMEKAA KIVIPI .
Baada ya 2015 chama wamekigeuza kuwa National movement na siyo Chama.
CCM = Serikali kuu, Serikali za Mitaaa, Vyombo vyote vya Usalama, Jamii yote ya kipato vha Chini, wakulima, wachimba madini na sector zote za nchi za kiuchumi , kisiasa na kiutawala.

Eneo pekee ambalo hawajalishika ni wafanyabiasha na kwa hili 45% wako upande wao.

Wanachokitaka na wamejaribu na wanaelekea kufanikiwa ni kufanya CCM iwe NATIONAL CONSCIENTE

(A national consciousness is a shared sense of national identity and a shared understanding that a people group shares a common ethnic/linguistic/cultural/ economic/education background.
a rise in national consciousness has been the first step towards the creation of a nation)

ukiipinga CCM unatikisa sukari kwenye kikombe chá chai, kwa hiyo inazidi CCM inanoga.

Na hii ndio maana naamini viongozi wa sasa hivi wa vyama vya upinzani vyote hawana uwezo wanaodai wanao kufanya mabadiliko.

Mwanachama wa chama cha upinzani yupo kwa kuiimarisha CCM na aliyepo CCM yupo kwa kuimarisha CCM.

Inatakiwa muda mrefu nikuchambulie michango mitatu au minne ili uweze kuelewa.
Ndio maana vijana wa upinzani wanachanganywa CCM na vijana wa CCM wanaendelea kuwa CCM.
Una mawazo mgando ndugu, ungejua kuwa kila lenye mwanzo halikosi mwisho usinge bwabwaja hapa na ushauri wako wa kisukuma.

Tulia bwashee hii vita ya kuiondoa CCM sio ya wapinzani bali ni vita ya Mungu mwenyewe ambaye alionyesha ubabe wake kwa kumwondoa huyo JPM wenu ambaye mlijitapa kuwa mtampa ridhaa awe rais wa milele shenzi nyie

Sasa huyo Mungu aliyemwondoa Magufuri atawaondoa mafala wote ccm wanaodhani kuwa utawala ni mali yao

Time will tell
 
Suluhisho ni majimbo mawili ya kiutawala ya Tanganyika na Zanzibar chini ya Rais mmoja wa Jamuhuri.Kila jimbo linakuwa na waziri mkuu wake au Gavana, bunge lake lenyewe, mfumo wa mahakama zake na mahakama kuu za Rufaa na Katiba za kitaifa.
Hii hoja KUNTU sana. Hongera kwa kuiona hili. Kuwa na nchi moja na Rais moja ndo suluhisho la kweli. Then Tanganyika ikawa na Gavana au PM na Zanzibar ikawa na Gavana au PM.
 
Una mawazo mgando ndugu, ungejua kuwa kila lenye mwanzo halikosi mwisho usinge bwabwaja hapa na ushauri wako wa kisukuma.

Tulia bwashee hii vita ya kuiondoa CCM sio ya wapinzani bali ni vita ya Mungu mwenyewe ambaye alionyesha ubabe wake kwa kumwondoa huyo JPM wenu ambaye mlijitapa kuwa mtampa ridhaa awe rais wa milele shenzi nyie

Sasa huyo Mungu aliyemwondoa Magufuri atawaondoa mafala wote ccm wanaodhani kuwa utawala ni mali yao

Time will tell
Mkuu matusi, kubagaza ndio mchango unaoweza kuutoa?. Mnnandika sana utumbo bila kufanya utafiti wa kuweza kufahamu tunaenda wapi.

China Urusi, Vietnam, Japan Singapore, Laos na nchi nyingi zingine zilizo kuwa za kijamaa zimebadilishwaje.

Mkubwa wewe huwezi ku-cross utabaki mpinzani na CCM watabaki kwao na hautokuwa na ukakasi. Wakati huo ukifika hautakuwa na maneno uliyo nayo leo.
 
Kijana naomba nikusaidie ili kesho yako iwe ya mwanga na pia ujue unapigana na nani kisiasa.
Hii itakusaidia huenda michango yako inayofuata ikiwa ya kielimu ni sio ushabiki maandazi.

CCM IMEKAA KIVIPI .
Baada ya 2015 chama wamekigeuza kuwa National movement na siyo Chama.
CCM = Serikali kuu, Serikali za Mitaaa, Vyombo vyote vya Usalama, Jamii yote ya kipato vha Chini, wakulima, wachimba madini na sector zote za nchi za kiuchumi , kisiasa na kiutawala.

Eneo pekee ambalo hawajalishika ni wafanyabiasha na kwa hili 45% wako upande wao.

Wanachokitaka na wamejaribu na wanaelekea kufanikiwa ni kufanya CCM iwe NATIONAL CONSCIENTE

(A national consciousness is a shared sense of national identity and a shared understanding that a people group shares a common ethnic/linguistic/cultural/ economic/education background.
a rise in national consciousness has been the first step towards the creation of a nation)

ukiipinga CCM unatikisa sukari kwenye kikombe chá chai, kwa hiyo inazidi CCM kunoga.

Na hii ndio maana naamini viongozi wa sasa hivi wa vyama vya upinzani vyote hawana uwezo wanaodai wanao kufanya mabadiliko.

Mwanachama wa chama cha upinzani yupo kwa kuiimarisha CCM na aliyepo CCM yupo kwa kuimarisha CCM.

Inatakiwa muda mrefu nikuchambulie michango mitatu au minne ili uweze kuelewa vizuri.
Ndio maana vijana wa upinzani wanachanganywa CCM na vijana wa CCM wanaendelea kuwa CCM.

Hii ni operation ni ya miaka 25 , ambayo ni generation moja. Baada ya hapo ama upinzani au CCM vyote vita fanana tuu na upinzani hautokuwa tishio kwa CCM na vile vile CCM háito kuwa kikwazo kwa upinzani. wote CCM na Upinzani watakuwa wanacheza, wanapika na kula sahani moja..
CCM ingalikubalika Pemba kwa mtindo huo. Na kila uchaguzi inazidi kuuwa watu. Uchaguzi uliopita wamekodi askari wa Burundi.
 
Back
Top Bottom