Rais Samia Suluhu Hassan: Alama ya mwisho ya anguko la Utawala wa CCM, Tanzania

" Watumie kikamilifu kanuni ya GIVE and TAKE. Wakubali kubaki na kidogo na pia kupoteza kidogo. Kama wanataka yawe yao yote, wakae tayari kupoteza yote."

Nakubaliana na maoni yako na hapa nataka nizungumzie hii aya ya mwisho,hapa kwenye Give and take ndio shida ya CCM,hawapo tayari kutoa kidogo na kubaki na kidogo na hili kosa alishalianzisha Mwendazake kwa kuiba uchaguzi mdogo na huu wa wabunge na uraisi kwa kupora majimbo yote ya upinzani.

Kosa lingine linaloenda kufanyika ni hili la kukataa katiba mpya na hapa wanadhani kwamba wenye shida na katiba mpya ni wapinzani kitu ambacho si kweli hapa lipo kundi kubwa sana hata humo CCM wapo.
Na hii katiba mpya si tu kwamba wanaikataa kwa sababu haina maana hapana,wanajua kabisa ni muhimu ila kwa sababu wanajua itaenda kufanya walichokumbatia kipungue mkononi mwao ndio maana wanatumia nguvu kubwa kuikataa.

Sasa hapa wanaosema kwamba CCM haifi wajiulize yafuatayo;
[emoji736]Nini kilimtisha mwendazake mpaka kaamua kupora uchaguzi mpaka watoto wakajua ameiba ?
[emoji736]Kwanini CCM inatumia nguvu kubwa hasa dola kubaki madarakani?
[emoji736]Nini kinasababisha Mama Samia aogope kuruhusu mikutano ya Kisiasa iendelee wakati yeye hagharamii chochote kwenye kwenye hio mikutano?

Ukiangalia vidokezo nilivyoweka hapo juu utaona kabisa ni 'Hofu' ndio iliyojaa kwenye mioyo ya CCM wakijua kabisa Mikutano ya Kisiasa itaamsha watu kifikra juu ya udhaifu wao,Pia itawaamsha hamasa ya watu kudai Katiba mpya kitu ambayo ikipatikana ni wazi kabisa watakuwa hawana chao maana nguvu yao kuu ipo kwenye Dola wala sio wananchi.

Mwisho kabisa,CCM wakubali au wakatae wao ndio wanaenda kupoteza katika hili,maana wapinzani wao hawana chochote cha kupoteza kwa sasa,
CCM ndio wamekumbatia vyote na wanashindana waendelee kubaki navyo na kwa sababu watu wameshaamua,hapa wanaenda kupoteza vyote,ni suala la muda tu watakuja kugundua walishachelewa na hawataamini kama ambavyo hawakuamini siku Magufuli alipopumzishwa kwa amani(kama anayo)huko Chato.
 
Ni time tu.... Kama USSR ilianguka .... Kwa nini isiwe CCM.
 
Hizo takwimu zako ni figisu figisu Za vyombo vya dola. Tuliona mabegi badala kubeba nguo yakibeba kura feki
Acha uongo. Mabegi majimbo yote nchi nzima? Sema ukweli wapinzani hawakuwa na sera wala ajenda mpya za kueleweka na wananchi.

Sera zao zilizowazolea umaarufu za Wizi, Ufisadi na Rushwa kwa viongozi na watumishi wa umma zilizikwa na JPM.

Pia aliwabana vilivyo hasa kukataza mikutano ya nje na maandamano yasiyo na kibali wala tija. Wakabaki wanatapatapa.
 
Well said,hawa jamaa wanajidanganya sana na kujipa tumaini lisilokuwepo.CCM is a "networking system of intelligence"
 
umeandika kwa kina sana ili kutaka kuaminisha wadau kwamba hisia zako na ndoto zako ni za kweli. Hizo zitabaki kuwa hisia zako na si lazima ziwe na ukweli wowote.
ninachofahamu mimi ni kwamba vyama vya upinzani nchi hii bado havijawekeza vya kutosha kuwa tayari kushika dola. Kelele za kutaka katiba mpya haziwezi kumbadirisha mpiga kura akupigieni kura ninyi badara ya ccm.
zile harakati za kweli za kuongeza wapiga kura kwa kushuka mpaka chini kabisa kufungua ofisi zenu mbona hazipo? Hapa usilete hoja ya kwamba JPM aliwazuia, kwa sasa hayupo japo bado anaendelea kuwaumiza sana( sijui sababu ni nini).
fanyeni harakati ambazo walio wengi watawaunga mkono na nguvu ya umma itaamua hata kama hakuna katiba mpya.
 
Magu in general was a good president naamini amefanya mazuri lakini vitendo vya utekaji, wanasiasa kufungwa kwa kesi zisizoeleweka na wengine kupigwa risasi, wizi wa kura na usalama wa Taifa kufanya chochote wanachotaka na kujifanya miungu mtu etc nchi ilikuwa inaelekea pabaya sana na magu hakukemea hayo kama alikuwa hausiki, nchi ilizaa mamtu kama Sabaya na Makonda..majitu ya ovyo kabisa
 
CCM bila wizi wa kura wasingekuwa wanaongoza nchi sasa hivi
 
Ni kwa sababu Hakuna jamaa yako aliuliwa Na vyombo vya dola wala kuumizwa
 
Asante sana kwa mchango wako mzuri...

Ndugu, yote yaliyokaa vibaya, yote wanayoyakataa CCM, yote yatafanyika/yatatokea...

Katiba mpy ya wananchi itaandikwa whether they (CCM) like it or not...

Tume Huru ya Uchaguzi itaanza kuundwa kwanza kati ya sasa na kabla ya mwaka 2025...

HOFU yao ni ya KWELI na ya DHATI kabisa. Na lazima wawe na HOFU kwa sababu miaka yote hii wametawala kilaghai na kwa udanganyifu mwingi...

Lakini kuwa na HOFU hakutawasaidia kwa sababu HOFU yao ni lazima iwe HALISI. Wanachokiogopa ni LAZIMA kiwapate...
 
Hawana ujanja hao walaghai
 
Nimesoma break news HAITI
 
CCM kuendelea kujiita mfumo ndiyo kutarahisha zaidi kifo chake kuliko kujitenga na dola.

2015 mpaka 2020 kilikuwa ni kipindi kilichoiua rasmi ccm.


Hakiishi kwa sera na ushawishi sasa kinaishi kwa kulindwa na dola.

Eleweni jambo moja muhimu dola haijawahi kushinda umma popote duniani pale yanapohitajika mageuzi ya kiutawala.
 
Hapana japo unaelekea kidogo ,anguko la ccm bado kidogo ila chadema watapata wabunge wengi kwa 2025 na jimbo moja karibu na magu kama unaenda mara kabla hujavuka msoma litaenda chadema.

Ukiona hivo ifikapo 2035 ccm itapumzika na haitainuka tena.

lakini iko hvo tu kwa sababu yeye ajaye kuanzia huo mda ni mtawala wa taifa na dunia nzima ambaye siri zote za Mungu na biblia yaani neno la mungu limefunuliwa kwake

Na tuyaonayo hayo basi tujue mtu huyo atakuja kufufuka baada ya siku tatu akisha kuzikwa kwa heshima kama mkuu wa nchi lakini yote hayo ili majira yabadilike na watu wote turudi kwa mungu ,

yeye ndo anatuletea uzima wa milele kwa kizazi hiki na kijacho,

Mapito yake ni kama inavyosema isaya 53
Yaani mtu wa huzuni nyingi ,ajuaye sikitiko na hana uzuri mpaka tumtamani ,aliyevumilia maneno mabaya na watu waliomtendea mabaya akiwajibu kwa kuwaombea na kumwachia Mungu lakini yeye ataleta haki yote duniani juu ya watawala

na danieli 2,39 yaani ataupata ubunge theni atakuwa mkuu wa nchi na dunia yote kama alivyo ahidiwa na Mungu kwa neno la danieli lile la sanamu ya mfalme nebukadneza huku akiongozwa na roho wa Mungu kuujua mda wote wa majira ya utimilifu wa kutabiriwa kwake mwaka 2012 akirishudia kwa wenzake sehemu mbalimbali na kuhusu fimbo ya Kristo yeye ndo kapewa na akiwashuhudia wenzake juu ya unabii wake alivyotabiriwa na utimilifu wa neno hilo huku akiwashuhudia wenzke darasani.

,Ana nguvu alizopewa na Mungu kwa neno la kristo kama inavyosema timotheo 1,1.12-19.

Ni yule ambaye bahati bukuku anamuongelea kwenye wimbo wake wa NANI AITIKISE tz na DUNIA AU NABII ALIYETABILI KIFO CHA MAGUFULI ALIVYOSEMA KUHUSU KUSUDI LA KUFA MAGUFULI yaani ili akitwae kiti hicho kidogo na badae kile kiti kikuu baada ya miaka 10 yaani ni ahadi kutoka kwa Mungu mkuu kusudi dunia irudi kwa Mungu.

Yote hayo yamefunuliwa kwake kabla na kote ameyasema tena kapitia mapito hayo magumu ya kuwa kinyume na watu wenzake yaani aibu sana usoni kwake yaani kaibeba lawama yote kutoka kwa watu wengi Kama alivyotabiriwa huko nyuma.

Kwa sasa kaimarika na uwezo wa kimungu kapewa na yeye ndiye aliyenenwa na kitabu cha yohana kuhusu ahadi ya Mungu baada ya kristo masihi wa israel kuwepo kwetu ila katoka kwa Mungu na kristo Kamwachia njia zake zote na atanena yale ya kristo , atayanena ya watu wote wa dunia yote kutoka kwa Mungu na YEYE ANEKUJA ILI TURUDI KWA MUNGU.
MUNGU NI PENDO.

Well come 2035, dunia haina mwisho ila majira yatabadilika baada ya kufufuka kwake.
 
Asante Sana. Nabii wa Bwana.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kuwa na kiongozi mkuu wa nchi kutoka Zanzibar halafu atawale Tanganyika, it is absolutely not right and unacceptable.
Ninyi watu waajabu sana, mkigeuka huku mnasema kabila lenye watu wengi halifai kuongoza Tanzania (yaani rais hasitoke huko) lakini mkitazama kule mnasema "kabila dogo" la wazanzibari halifai kuiongoza Tanzania. Tuwaeleweje ninyi??
 
Siku upinzani ukitaka kushinda siasa za
Ccm lazima Kwanzaa wajifunze kuisoma mifumo ya nchi yao Tanzania ipoje na namna yakukabiliana mayo. Mifumo Kama ya usalama na tume ya uchaguzi imefungamana na siasa za ccm,kutokuwa na maelewano na taasisi hizi mbili kuiangusha ccm ni vigumu. Karata mnazozicheza nikuweka utabiri usio weza kutokea yaan matumaini hewa.Inatakiwa mje na mbinu zakuweza kuweka sawa ushirikiano wenu na mifumo ya usalama WA nchi na tume ya uchaguzi maana taasisi hizi huathiri Sana matokeo ya uchaguzi.
Utawala hupatikana kwa kudhibiti kete kuu tatu 1.Kura za wapiga kura
2.Tume ya uchaguzi 3.vyombo vya Usalama
Ukiangalia kwa sasa haijulikani wapinzani wamefanikiwa kudhibiti kete hizi tatu kwa viwango gani?
Moja ya failures zilizojitokeza ni upinzani kuvurugana na vyombo vya usalama hata mkakati WA msajili WA vyama vya siasa kutaka kuwakutanisha wapinzani na polisi walisusa.

Taifa Lina mifumo yake yakujilinda kiutawala,kielimu,kiuchumi,kiusalama na kisiasa.Jifunzeni mifumo hiyo nakuifanya rafiki kwa kujipenyeza nakuwa center ya decision maker.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…