Acehood
JF-Expert Member
- Oct 1, 2018
- 1,700
- 2,904
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika moja ya utekelezaji wa ratiba yake ngumu huko nchini Urusi aliulizwa swali na moja ya muendeshaji wa majadiliano (moderator) kwamba;
Tanzania inataka kupanua wigo wa biashara kati ya Tanzania na Urusi, wakati huohuo kuna vikwazo hasa vya kiuchumi alivyowekewa Urusi kimataifa. Swali la muendesha majadiliano lilikuwa;
"ni kwa namna gani Serikali ya Tanzania ikiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan itaweza kukwepa na kufanikisha lengo la kuongeza ukubwa na ufanisi wa mahusiano ya kiuchumi kati ya Urusi na Tanzania ikiwa kuna vikwazo (restrictions) tayari ambavyo amewekewa Urusi vinavyomzuia kufanya shughuli za kiuchumi na mataifa mengine kwa uhuru?".
Rais Samia Suluhu Hassan alijibu "Tanzania haiko kwenye vikwazo" akimaanisha kwamba Tanzania haijawekewa vikwazo vyovyote.
Kwa kawaida hili jibu la Rais Samia Suluhu Hassan halikujibu swali la muendesha majadiliano moja kwa moja, bali limejibu swali la muendesha majadiliano kwa namna nyingine.
Ni jibu ambalo limeonyesha ukomavu wa Rais wa Tanzania kidiplomasia na katika siasa za ulimwengu (Geopolitics).
Kama Rais wa nchi (Head of State) kuna maswali ya kujibu moja kwa moja na kuna maswali ya kujibu kwa namna tofauti.
Lile swali la muendesha majadiliano lilikuwa la hatari na mtego kwa diplomasia ya nchi yetu na Rais wa Tanzania 🇹🇿 aliweza kulijibu kiufasaha zaidi kulingana na nafasi yake yeye kama Rais wa nchi.
Leo raia wa kawaida nikiulizwa lile swali nitalijibu kama nafanya mtihani wa darasani, lakini to a diplomat ni swali risk sana na lenye mtego mkubwa.
Kusema ukweli Rais ameonyesha ukomavu kwenye hilo.
Na Rais yeyote kuanzia Vladimir Putin, Donald Trump na wengineo lazima wangekwepa kujibu lile swali moja kwa moja.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
#uzalendokwanza🇹🇿