Rais Samia Suluhu Hassan ashiriki Mkutano wa 12 wa Baraza la Taifa la Biashara

Rais Samia Suluhu Hassan ashiriki Mkutano wa 12 wa Baraza la Taifa la Biashara

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Saa 4:00 Asubuhi tutawaletea Kile kinachojiri moja kwa moja ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan atashiriki Mkutano wa 12 wa Baraza la Taifa la Biashara.



========

Angelina Ngarura(Mwenyekiti Sekta Binafsi):

  • Tunampongeza Waziri Nchemba kwa kukemea Rushwa kwenye taasisi ya TRA hasa kitengo cha ukadiriaji Kodi. Swala hili lilikuwa ni kero na lilivunja moyo wafanyabiashara
  • Mheshimiwa Rais, leo hatufikirii tena kwa mabavu lakini kodi zinakusanywa
    - Leo hatufanyi kwa maguvu kwenye uwekezaji, umeanza kuboresha mazuri ya mazingira, wawekezaji wa ndani na wa nje wanakuja kuwekeza
  • Hatuzungumzii uhusiano wa sekta binafsi na sekta ya Umma bali tunakaa pamoja kwenye meza ya mazungumzo kujadili namna ya kuboresha sera na sheria
    -Mheshimiwa Rais, utaona hata leo mawaziri wamekaa na sekta binafsi kwenye meza moja wanajadiliana
    Mheshimiwa Rais, umebadilisha kabisa Formation ya mambo
    -Kwa mainjinia watakuwa wanafahamu maana na umuhimu wa 'expansion joint' kwenye majengo. Wafanyabiashara wana utulivu, wanafikiria kukuza biashara, kuongeza ajira na kulipa kodi zako.

Hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan

Nakushukuru Balozi Katanga kunikaribisha kuongea na hadhara hii, ukumbi umejaa kwelikweli. Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kazi iendelee.

Nawashukuru wajumbe wote wa baraza la Taifa la biashara kwa kuhudhuria mkutano wa 12 wa baraza la Taifa la biashara. Baraza hili lina wajumbe 50, 25 wanatika sekta ya uuma na 25 wanatoka sekta binafsi hata hivyo katika kupanua wigo wa majadiliano tumealika wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka kwenye mikoa na sehemu mbalimbali kama wale wawekezaji mlio waona na pia mabalozi ili waweze kuchukua na kutupa msukumo unaostahiki ni imani yangu uwepo wenu utaongeza tija katika mkutano huu.

Hii ni mara yangu ya kwanza kushuriki mkutano huu tangu kuchukua dhamana ya kuliongoza taifa hili na mkutano huu ulifanya miaka mitatu nyuma na wapo ambao walikuwa wajumbe wa baraza hili na leo hawapo tena kama John Magufuli, Kijazi, Mengi, Shamte nk Hivyo tusimame dakika 1 kuwaombea dua....... Mwenyezi Mungu Rahimu Azipumzishe Roho zao mahali pema peponi Amen.

Wajumbe wa mkutano huu nimeshukuru mwenyekiti wa baraza la biashara kwa salamu zake za pongezi kwa yale ambayo amaesema tumeanza kuyashughulikia, Aidha namshukuru kwa ahadi yake kuwa sekta binafsi ipo tayari kufanya kazi kwa bidii na uadilifu, kwa niaba ya serikali nasema asenteni sana.

Sekta binafsi ni muhimili mkubwa wa maendeleo katika nchi na kwa maneno mengine ni injini ya kukuza uchumi katika nchi na kwa hakika katika dunia ya leo hakuna taiga linaloweza kujinasua bila kufanya kazi na sekta binafsi na kwa kuzingatia hilo mwaka 2001 serikali yetu iliamua kuanzisha baraza la taifa la sekta binasfi lengo likiwa ni kuweka majadilino na makubaliano baina ya sekta binafsi na serikali ili kuondoa kutokuamiana kati ya sekta binafsi na serikali na ninyi ni mashahidi mambo mengi yamejadiliwa.

Mafanikio mengine ni kunazihswa kwa mabaraza ya mikoa na wilaya na baraza hili limeweza kuondoa kutokuaminiana na mambo mengi yamejadiliwa nitoe wito wa kuendelezwa kwa baraza ili na pia kuyapa uhai mabaraza ya mikoa na wilaya ili nayo yaweze kufanya kazi na baraza la taifa liweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Kupitia baraza hili kumeundwa mabaraza ya wanawake peke yao, nami nimejitolea kuwa mlezi wa mabaraza ya wanawake na lengo ni lile lile kuwainua wanawake.

Changamoto nyingi zimetajwa hapa na kama nilivyosema kuwa hapa kuna wasaidizi wangu watanisaidia kuyafanyia kazi na kama ambavyo mwenyekiti alivyosema kuwa changamoto nyingi tumeanza kuzifanyia kazi. Naambazo bazo naahidi kuzifanya kazi. Kwa swala la mabenki tumefanya kazi nzuri ya kuwaongezea mitaji na tutaendelea kuongeza mitaji kwa bank za wakulima na bank.

Na eneo lingine ni eneo la utalii tutakwenda kuliwekea mkazo kwa kuwa limeathirika na janga la korona na sekta ya utalii itakwenda sambamba na sekta ya usafirisha kwa kuwa zinakwenda sambamba. Kazi yangu ilikuwa ni kufungua mkutano na Mwenyekiti kashaweka ajenda kwenye meza, Maswala ya local content tutakwenda kulishughulikia kwa kuwa niswala muhimi kweli lakini litahitaji kungalia na swala la uchumi na tutafanya pamoja na ninyi.

Mwasala ya pre inspection ni wafanyabiashara nyinyinyinyi mlipiga kelekele serikali ikasikiliza na sasa kuna kelele tenabasi tukaa tuone tena wapi panapotuchoma na ndio faida ya majadiliano. Mambo ni mengi na tutayajadili na sasa tupo au tumeingia kwenye wimbi la nne la mapinduzi ya viwanda na wimbi hili limengukia Afrika na kuna mambo ya Teknolojia.

Lengo ni kufanya mazingira ya biashara yawe mazuri na kukuza uchumi wa taifa letu, nitamke rasmi kuwa mkutano huu umefunguliwa na sasa nimepo tayari kwenda kukaa kama mwenyekiti na kuna kitu nilikuwa sijakisema hapa kuhusu bandari ya Bagamoyo ni kuwa tunakwenda kufanya mazungumzo na hii ni pamoja na Mchuchuma na Liganga nazo nimesema serikali ifanye uchunguzi tuone tunafanya nini ili mradi uweze kuendea tuone serikali itajitoa ngapi na mwekezaji ngapi ili mradi uweze kuendelea hiyo ni pampja na mradi wa Bandari ya Bagamoyo pia chuma imepanda bei hivyo ni wakati sahihi wa Tanzania kuchangamka .
 
Naona tasac leo wanalo wametajwa kuhusu kufanya clearing badala kusimamia wadau.

TBS nao wametajwa ...swala la' inspection destination linakufa sasa. Maana magari yankuja mabovu.

Wakandarasi nao wapewe contract mambo ya force account yafe.




....tungojee majumuisho ya mama SSH
 
ongezeni ufanisi kwanza kwenye Bandari ya DSM, Tunataka kuona utendaji wa kisasa na wenye kasi ndipo tufikirie bandari ya Bagamoyo,

nyie mnashindwa kuweka ufanisi ktk bandari ya DSM ndio maana mnasababisha msongamano!!
unongea zaidi kuliko kutenda, yaaani viongozi wetu waongeaji zaidi kuliko utendaji.

si maanishi kuwa bandari ya Bagamoyo isijengwe au haina umuhimu la hasha! ila najiuliza tu kwa nini tujiongezee mzigo wakati bandari ya Dsm pekee bado hatujafanikiwa kuiendesha kwa viwango vinavyo takiwa, wizi na ubadhirifu unajitokeza kila mara sasa tunataka kujenga bandari ya b.moyo ili kuendeleza wizi au?

tunatakiwa kwanza tuimarishe na tuzibe myanya.
Mwenyekiti wa sekta binafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Mama Samia Suluhu amesema wamemeanza Mazungumzo ya kufufua Mradi wa Bandari ya Bagamoyo uliokua umesimama.
Amesema hayo katika mkutano na 12 wa Baraza la Taifa la biashara.

“Kuhusu mradi wa Bagamoyo, niwape habari njema kwamba tumeshaanza mazungumzo ya kufufua mradi wote wa Bagamoyo, tunakwenda kuanza mazungumzo na Taasisi ambayo ilikuja kwa ajili ya mradi huo kwa lengo la kuufungua kwa faida ya Taifa letu” @SuluhuSamia


View attachment 1830556
 

Attachments

  • IMG_20210626_113943.jpg
    IMG_20210626_113943.jpg
    27 KB · Views: 1
Wakati akiongea na Baraza La Wafanyabiashara Samia Amesema Kwamba Mazungumzo ya Kufufua Ujenzi Yanaendelea Na Wako Kwenye Mazungumzo. Ni Kwamba Hayati Kuukataa Huo Mradi Hakuwa Sahihi?
Screenshot_20210626-114109.jpg
 
Wacha sasa tubaki watazamaji tu wa hii issue.

Magu aliamua kivyake, na Mama nae kaja kivyake, ila wote wanaendeleza usiri wa mikataba.

CCM sssa ndio muone na mjifunze kwa vitendo kuwa Katiba mpya ni muhimu, na kwamba ili nchi isonge mbele, hatuhitaji strong people bali strong institutions na katiba iliyo bora na zaidi watawala wanaoheshimu utawala wa sheria.
 
Wakati akiongea na Baraza La Wafanyabiashara Samia Amesema Kwamba Mazungumzo ya Kufufua Ujenzi Yanaendelea Na Wako Kwenye Mazungumzo. Ni Kwamba Hayati Kuukataa Huo Mradi Hakuwa Sahihi?View attachment 1830552
Hakuwa Malaika jiulize kwa nini ilisemwa mkataba ni mbovu lakini hakuonesha kwa maandishi zaidi ya kusema tu ni mbovu na huu nao hatujui uhalisia wake ukoje maana yote yanafanana
 
Hakuwa Malaika jiulize kwa nini ilisemwa mkataba ni mbovu lakini hakuonesha kwa maandishi zaidi ya kusema tu ni mbovu na huu nao hatujui uhalisia wake ukoje maana yote yanafanana
Kwa Hyo Huyu Ataaonesha Huo Mkataba Ulivyo Mzuri??
 
Kwa watu wanaowaza mbali nchi inatakiwa kuwa na bandari hata kwa kila mkoa ambao una bahari

Angalia nchi zinazotuzunguka zaidi ya watu million 300 je miaka 20 ijayo population yao itakuwa kiasi gani je tutaweza kuwahudumia kwa bandari hizi?

Jibu ni hapana issue sio kupinga mradi issue hapa ni kupeleka mkataba bungeni upitiwe na wanasheria tuangalie maslahi yetu kama nchi.

Tuache kuwaza kupigwa tu ila tuboreshe mradi wenyewe na kuweka mahitaji yetu.
 
Kwa watu wanaowaza mbali nchi inatakiwa kuwa na bandari hata kwa kila mkoa ambao una bahari

Angalia nchi zinazotuzunguka zaidi ya watu million 300 je miaka 20 ijayo population yao itakuwa kiasi gani je tutaweza kuwahudumia kwa bandari hizi?

Jibu ni hapana issue sio kupinga mradi issue hapa ni kupeleka mkataba bungeni upitiwe na wanasheria tuangalie maslahi yetu kama nchi.

Tuache kuwaza kupigwa tu
Yes Hilo Ndio Jambo La Msingi Mkuu
 
Bandari ya Dar kwaheri, Mtwara na Tanga adios,

Kwaheri Tanzania karibu mkoloni.
 
Inawezekana hakuwa sahihi maana naye hakuweka wazi mkataba.

Huu si wakati wa kupigania mawazo ya hayati au legacy, ni wakati wa kupigania maslahi ya nchi.

Jambo sahihi la kuuliza ni huo mkataba wa bagamoyo utakuwa siri?
 
Back
Top Bottom