Rais Samia Suluhu Hassan ashiriki Mkutano wa 12 wa Baraza la Taifa la Biashara

Rais Samia Suluhu Hassan ashiriki Mkutano wa 12 wa Baraza la Taifa la Biashara

Huyu Mama anafanya Vitu Kwa Kufuraisha Watu, anataka Kuonekana hakubaliani na Mawazo ya Mtangulizi Wake. Angalia Hata Mradi wa Ujenzi Wa Kimara-kibaha Ni kama Umebuma Kabisa, Mradi Wa Hyo Barabara umekufa
Haya subiri huo mradi mtakuja kulia kama ilivyo gesi ya mtwara maana najua hapo mama hana uwezo wa kujisimammia anachokiamini atasikiliza watu especially msoga haitamwacha salama. Mama mara liganga na mchuchuma anataka pia waanze na amesema hata madini yakiwa kwenye hifadhi wachimbwe anaharaka gani huyu mama?
 
Huyu subiri huo mradi mtakuja kulia kama ilivyo gesi ya mtwara maana najua hapo mama hana uwezo wa kujisimammia anachokiamini atasikiliza watu especially msoga haitamacha salama. Mama mara liganga na mchuchuma anataka pia waanze na amesema hata madini yakiwa kwenye hifadhi wachimbwe anaharaka gani huyu mama?
Mama hana msimamo, atakavyoambiwa na wazee wa madili mdivyo atavyofanya
 
Haya subiri huo mradi mtakuja kulia kama ilivyo gesi ya mtwara maana najua hapo mama hana uwezo wa kujisimammia anachokiamini atasikiliza watu especially msoga haitamacha salama. Mama mara liganga na mchuchuma anataka pia waanze na amesema hata madini yakiwa kwenye hifadhi wachimbwe anaharaka gani huyu mama?
Mkuu Kimsingi lazima tubadilike kifikra na ndipo tutaweza kujenga mifumo iliyoimara na taasisi zilizo bora.
 
Huyu Mama anafanya Vitu Kwa Kufuraisha Watu, anataka Kuonekana hakubaliani na Mawazo ya Mtangulizi Wake. Angalia Hata Mradi wa Ujenzi Wa Kimara-kibaha Ni kama Umebuma Kabisa, Mradi Wa Hyo Barabara umekufa
Hajakosea, hata Magufuli hakukubaliana na mambo mengi yabKikwete, hivyo hiyo spirit inaendelea
 
Kwa Hyo Huyu Ataaonesha Huo Mkataba Ulivyo Mzuri??
Anayo nafasi ya kurekebisha makosa au dosari za mkataba lkn aepuke mkataba aliousema Magufuli kuwa wachina wataimiliki bandari kwa miongo kadhaa, bali uwe terms za win win
 
Kazi iendelee..
trumpsmirk.png
 
I'm confused... Naomba darasa. What has changed?
Kwanini tumlaum Samia kujifanyia mambo ilhal watangulizi wake nao walijifanyia na kuacha ya watangulizi wao?
Anzia Mwinyi, BM, JK na JPM wote walijifanyia mambo yao.
Kuepuka hili tudai katiba vinginevyo kwa utamaduni usio rasmi wa kujifanyia mambo utadumu miaka mingi
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hakuwa Malaika jiulize kwa nini ilisemwa mkataba ni mbovu lakini hakuonesha kwa maandishi zaidi ya kusema tu ni mbovu na huu nao hatujui uhalisia wake ukoje maana yote yanafanana
Kwa sasa hakuna mkataba,ila mama kasema wanajadiliana upya
 
Mawazo ya kijinga sana haya. Yaani bandari zife kwa kuongeza bandari? Mkataba uwekwe wazi tuone content kama zina maslahi bandari ijengwe, kama hauna maslahi urekebishwe uwe na maslahi kwetu bandari ijengwe. Ya dar es salaam pia na nyingine ziboreshwe. Tuachane na kukariri na woga wa kupigwa tu. Ss sio mafala wala wanyonge.
Mkuu kusubiri mkataba uwekwe wazi ili ondoa mkuu kimsingi utashi kama kaagiza watu wakajadiliane sina hakika kama tutafaidika na uo mradi, Uzuri wa Magufuli alikuwa mfatiliaji na mama mwenyewe alikiri kuwa yule alikuwa na uwezo wa pekee ila Mama akajisema yeye ni mtu wakucheza na ghaph tu zimepanda zimeshuka basi..! Kwa maana hi mama ni mtu anaesubiri watu wamchoree aletewe mezani asaini basi.

Uadilifu kwenye nchi yetu ni zero na ndiyo maana Magufuli alikuwa anakulanao sahani moja, sio ajabu katika nchi yetu watu ambao wameambiwa wakajadiliane na ao wawekezaji wakapelekwa ughaibuni na hiyo kampuni, kule wakala bata wakaonyeshwa mifano ya bandari kama hizo huko Dubai wakapewa maipad na kulazwa mahotel makubwa na mwisho wa siku wakala posho zakutosha toka kwaiyo kampuni na wakasaini mambo yaende bila kujali maslahi ya taifa ni kawaida tu kitu kama hiki kilikuwa awamu ya 4.

Mradi wa Julius Nyerere Hydroelectric power usingejengwa kama Magu angekuwa mlaini usingefanyika cos aliwapa watanzania kazi wafanye tafiti athari gani zitatokana na ile project na watoe mapendekezo jinsi gani tufanye kuovercome hizo impact ila ajabu ya watanzania wale walishauri eneo la mradi hapatakiwi kudobdokewa ata tone la oil na choo kiwe km 10 toka eneo la mradi unapotekelezwa..! Hawa ndiyo watanzania.
 
Saa 4:00 Asubuhi tutawaletea Kile kinachojiri moja kwa moja ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan atashiriki Mkutano wa 12 wa Baraza la Taifa la Biashara.



========

Angelina Ngarura(Mwenyekiti Sekta Binafsi):

  • Tunampongeza Waziri Nchemba kwa kukemea Rushwa kwenye taasisi ya TRA hasa kitengo cha ukadiriaji Kodi. Swala hili lilikuwa ni kero na lilivunja moyo wafanyabiashara
  • Mheshimiwa Rais, leo hatufikirii tena kwa mabavu lakini kodi zinakusanywa
    - Leo hatufanyi kwa maguvu kwenye uwekezaji, umeanza kuboresha mazuri ya mazingira, wawekezaji wa ndani na wa nje wanakuja kuwekeza
  • Hatuzungumzii uhusiano wa sekta binafsi na sekta ya Umma bali tunakaa pamoja kwenye meza ya mazungumzo kujadili namna ya kuboresha sera na sheria
    -Mheshimiwa Rais, utaona hata leo mawaziri wamekaa na sekta binafsi kwenye meza moja wanajadiliana
    Mheshimiwa Rais, umebadilisha kabisa Formation ya mambo
    -Kwa mainjinia watakuwa wanafahamu maana na umuhimu wa 'expansion joint' kwenye majengo. Wafanyabiashara wana utulivu, wanafikiria kukuza biashara, kuongeza ajira na kulipa kodi zako.

Hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan

Nakushukuru Balozi Katanga kunikaribisha kuongea na hadhara hii, ukumbi umejaa kwelikweli. Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kazi iendelee.

Nawashukuru wajumbe wote wa baraza la Taifa la biashara kwa kuhudhuria mkutano wa 12 wa baraza la Taifa la biashara. Baraza hili lina wajumbe 50, 25 wanatika sekta ya uuma na 25 wanatoka sekta binafsi hata hivyo katika kupanua wigo wa majadiliano tumealika wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka kwenye mikoa na sehemu mbalimbali kama wale wawekezaji mlio waona na pia mabalozi ili waweze kuchukua na kutupa msukumo unaostahiki ni imani yangu uwepo wenu utaongeza tija katika mkutano huu.

Hii ni mara yangu ya kwanza kushuriki mkutano huu tangu kuchukua dhamana ya kuliongoza taifa hili na mkutano huu ulifanya miaka mitatu nyuma na wapo ambao walikuwa wajumbe wa baraza hili na leo hawapo tena kama John Magufuli, Kijazi, Mengi, Shamte nk Hivyo tusimame dakika 1 kuwaombea dua....... Mwenyezi Mungu Rahimu Azipumzishe Roho zao mahali pema peponi Amen.

Wajumbe wa mkutano huu nimeshukuru mwenyekiti wa baraza la biashara kwa salamu zake za pongezi kwa yale ambayo amaesema tumeanza kuyashughulikia, Aidha namshukuru kwa ahadi yake kuwa sekta binafsi ipo tayari kufanya kazi kwa bidii na uadilifu, kwa niaba ya serikali nasema asenteni sana.

Sekta binafsi ni muhimili mkubwa wa maendeleo katika nchi na kwa maneno mengine ni injini ya kukuza uchumi katika nchi na kwa hakika katika dunia ya leo hakuna taiga linaloweza kujinasua bila kufanya kazi na sekta binafsi na kwa kuzingatia hilo mwaka 2001 serikali yetu iliamua kuanzisha baraza la taifa la sekta binasfi lengo likiwa ni kuweka majadilino na makubaliano baina ya sekta binafsi na serikali ili kuondoa kutokuamiana kati ya sekta binafsi na serikali na ninyi ni mashahidi mambo mengi yamejadiliwa.

Mafanikio mengine ni kunazihswa kwa mabaraza ya mikoa na wilaya na baraza hili limeweza kuondoa kutokuaminiana na mambo mengi yamejadiliwa nitoe wito wa kuendelezwa kwa baraza ili na pia kuyapa uhai mabaraza ya mikoa na wilaya ili nayo yaweze kufanya kazi na baraza la taifa liweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Kupitia baraza hili kumeundwa mabaraza ya wanawake peke yao, nami nimejitolea kuwa mlezi wa mabaraza ya wanawake na lengo ni lile lile kuwainua wanawake.

Changamoto nyingi zimetajwa hapa na kama nilivyosema kuwa hapa kuna wasaidizi wangu watanisaidia kuyafanyia kazi na kama ambavyo mwenyekiti alivyosema kuwa changamoto nyingi tumeanza kuzifanyia kazi. Naambazo bazo naahidi kuzifanya kazi. Kwa swala la mabenki tumefanya kazi nzuri ya kuwaongezea mitaji na tutaendelea kuongeza mitaji kwa bank za wakulima na bank.

Na eneo lingine ni eneo la utalii tutakwenda kuliwekea mkazo kwa kuwa limeathirika na janga la korona na sekta ya utalii itakwenda sambamba na sekta ya usafirisha kwa kuwa zinakwenda sambamba. Kazi yangu ilikuwa ni kufungua mkutano na Mwenyekiti kashaweka ajenda kwenye meza, Maswala ya local content tutakwenda kulishughulikia kwa kuwa niswala muhimi kweli lakini litahitaji kungalia na swala la uchumi na tutafanya pamoja na ninyi.

Mwasala ya pre inspection ni wafanyabiashara nyinyinyinyi mlipiga kelekele serikali ikasikiliza na sasa kuna kelele tenabasi tukaa tuone tena wapi panapotuchoma na ndio faida ya majadiliano. Mambo ni mengi na tutayajadili na sasa tupo au tumeingia kwenye wimbi la nne la mapinduzi ya viwanda na wimbi hili limengukia Afrika na kuna mambo ya Teknolojia.

Lengo ni kufanya mazingira ya biashara yawe mazuri na kukuza uchumi wa taifa letu, nitamke rasmi kuwa mkutano huu umefunguliwa na sasa nimepo tayari kwenda kukaa kama mwenyekiti na kuna kitu nilikuwa sijakisema hapa kuhusu bandari ya Bagamoyo ni kuwa tunakwenda kufanya mazungumzo na hii ni pamoja na Mchuchuma na Liganga nazo nimesema serikali ifanye uchunguzi tuone tunafanya nini ili mradi uweze kuendea tuone serikali itajitoa ngapi na mwekezaji ngapi ili mradi uweze kuendelea hiyo ni pampja na mradi wa Bandari ya Bagamoyo pia chuma imepanda bei hivyo ni wakati sahihi wa Tanzania kuchangamka .

expansion Joint tena🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️
 
Unafiki unawasumbua.kinachokufanya usisimke ni nini?
Unafiki wa Nini Tena Ndugu yangu...mwenzio Nina hofu tu...nifariji kwa kunipa pole na siyo unavyofanya kunikejeli...
 
Mkuu kusubiri mkataba uwekwe wazi ili ondoa mkuu kimsingi utashi kama kaagiza watu wakajadiliane sina hakika kama tutafaidika na uo mradi, Uzuri wa Magufuli alikuwa mfatiliaji na mama mwenyewe alikiri kuwa yule alikuwa na uwezo wa pekee ila Mama akajisema yeye ni mtu wakucheza na ghaph tu zimepanda zimeshuka basi..! Kwa maana hi mama ni mtu anaesubiri watu wamchoree aletewe mezani asaini basi.

Uadilifu kwenye nchi yetu ni zero na ndiyo maana Magufuli alikuwa anakulanao sahani moja, sio ajabu katika nchi yetu watu ambao wameambiwa wakajadiliane na ao wawekezaji wakapelekwa ughaibuni na hiyo kampuni, kule wakala bata wakaonyeshwa mifano ya bandari kama hizo huko Dubai wakapewa maipad na kulazwa mahotel makubwa na mwisho wa siku wakala posho zakutosha toka kwaiyo kampuni na wakasaini mambo yaende bila kujali maslahi ya taifa ni kawaida tu kitu kama hiki kilikuwa awamu ya 4.

Mradi wa Julius Nyerere Hydroelectric power usingejengwa kama Magu angekuwa mlaini usingefanyika cos aliwapa watanzania kazi wafanye tafiti athari gani zitatokana na ile project na watoe mapendekezo jinsi gani tufanye kuovercome hizo impact ila ajabu ya watanzania wale walishauri eneo la mradi hapatakiwi kudobdokewa ata tone la oil na choo kiwe km 10 toka eneo la mradi unapotekelezwa..! Hawa ndiyo watanzania.
Mkataba uwekwe wazi tuone hayo aliyosema kama ni ya kweli. Jiwe alikuwa mwongo sana na mdanganyifu.
 
Back
Top Bottom