Kwanza kabisa haijajulikana kama Sherehe hizi yeye ndiye atakuwa mgeni Rasmi au nayo itapita kimya kimya kama ilivyokuwa jana Sherehe za Muungano kwa sababu ya kuomboleza Msiba Mkubwa wa Jiwe.
Rais Samia ameamua kutojitenganisha na Hayati JPM - Mpango Kazi wa Mwaka 2020-2021 umejadiliwa lakini hakuna dalili kabisa kama kutakuwa na nyongeza ya mshahara. Rais Samia kaanza vizuri na hata kutamka kuwa kutakuwa na nyongeza ya mshahara. Wafanyakazi wanasubiri - hata hivyo mijadala ya bungeni na Serikali ilivyojionesha katika Mpango kazi ni hamna kabisa suala la kupanda mishahara. Hii ni ajabu ingine ambayo Rais Samia anataka kuionesha na kuonesha wazi wazi kuwa atakuwa anapelekeshwa na Spika Ndugai.
Spika Ndugai ni mjanja sana - anaenda kumtumbukiza Samia kwenye shimo - chuki kwa Samia itaanzia Mei Mosi. Ilipaswa kabisa baada ya Samia kuchukua URais asimamishe ule Mpango wa Serikali aupitie upya kwa kutumia wateuzi wake na kisha ndiyo upelekwe bungeni - yeye inavyoonekana ni kama amaeamua uende ulivyo. Huu Mpango Kazi na Mwelekeo wa Bajeti sio wa Samia ni wa Mtangulizi wake.
Kwa nini hakuufanyia hata review kidogo tu - Mwaka jana JPM alishusha kodi kwenye mishahara angalau kwa asilimia moja (1) lakini Mwaka huu baada ya kuwa ameshashinda Uchaguzi hicho hakikuwekwa kabisa. Yaani ni balaaa! Mama Samia hivi kwa nini umewaacha hawa watu kama akina Ndumbaro wa Utumishi na Msaidizi wake - huyu Waziri wa Utumishi naye kaingia lakini halioni hili kabisa.
Ninashangaa sana Bajeti za Wizara zinaendelea kujadiliwa zikiwa hazina kabisa projection ya nyongeza za mishahara - hivi kwa nini mnataka kumwangamiza huyu Mama kwa kuanza kuchukiwa mapema mapema hivi. JPM alikuwa anasema atakuja kufanya nyongeza kubwa - hamna kitu kama hicho duniani. Nyongeza kubwa ya mshahahara - say zaidi ya asilimia 50 huashiria kudorora kwa uchumi. Nyongeza hupaswa kwa wafanyakazi waliopo kwenye nchi wanazolipwa vizuri huwa haizidi asilimia sita (6%). JPM alichokuwa anasubiriwa kukifanya kama kweli ingekuwa ni kudororesha uchumi wa Tanzania zaidi au kuendeleza uwongo wa waziwazi na huku akitumia ubabe na ukandamizaji kutuongoza.
Rais Samia tafadhali achana na akina Ndugai - Ndugai atakuangusha - kundi lake la kutumia ubabe - yaani ile Sukuma Gang ipo na imeanza kushamiri zaidi. Mama pls pls jitenge na Ndugai. Huyu staili ya uongozi wake ni hiyo ya kibabe. Fikiria tu wewe kwa makini inakuwaje mpaka leo akina Halima Mdee na Kampani yake bado wapo bungeni?
Huo ndiyo mtihani wako wa kwanza - ulipaswa uanzie hapo - elekeza mbunge wako aanzishe hoja ya kutokuwa na Imani na Spika Ndugai kwa kulazimisha Halima and Gang kuwa wabunge. Ikibidi unda Tume ya kufanya uchunguzi kwa jambo hili. Una mamlaka hayo Rais wangu. JPM alijisahau sana na kakuzingatia misingi ya demokrasia hata kdg - ndiyo maana watu hawaogopi hata kumpa jina la Mwendazake - na ni kweli kabisa aende zake kule! Wewe jitofautishe na hawa watu - kama usipofanya hivyo kwa kweli hata hizi chokochoko za kutaka uongoze mara moja zitakuwepo sana.
Kwa kuanza hebu toa maelekezo ya nyongeza hata asilimia mbili tu kwa watumishi hawa waliosota miaka sita (just 2%) uone morari ya kazi na nchi itavyochangamka. Huwezi kuwatenganisha watumishi hawa na wananchi waliokuwa wakisemwa na JPM kuwa ni wanyonge au walalahoi. Kumbuka familia zetu WaTanzania ni extended so tupo nao humo humo. Usifuate kinachojadiliwa bungeni ni haramu kabisa. Hilo ni limpango la JPM na wewe sio JPM hata ukitaka kujing'ang'aniza hivyo wewe si yeye - kwa hili mwache ameshaenda zake pls!
NB. Kwa kushauri zaidi Hayati Magufuli alikuwa kabla ya Mei Mosi anakutana na viongozi wa wafanyakazi wanaweka mambo sawa - JPM alifanya hivyo miaka yake mitatu ya mwanzo akawaacha wafanye watakalo. Wewe pia unataka kufanya hivyo hivyo kutoitisha vikao na vyama kujadili maslahi yao. Viongozi wa vyama nao siku hizi wamejaa hofu tu utafikiri JPM bado yupo hawasemi hata tu kupongeza ahadi yako ya kuongeza mshahara. Wanapimia tu kwa sababu walishanunuliwa na JPM - sisi tunawaangalia tu - mwaka huu hasira zimetufika shingoni.
Hayati Magufuli alitudharau sana - sina shaka wewe angalau utaleta nafuu. Kuwa makini na Bunge! (tena sio bunge lote - ni wale Sukuma Gang tu). Mahakama umeshamaliza kazi - tayari kuna mabadiliko makubwa - hata Jaji Kiongozi Feleshi tayari kishatoa mwelekeo wa utendaji haki Mahakamani.