Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 1,015
- 2,493
Ukweli mchungu kwa Rais Samia, Serikali na chama-tawala CCM ni kwamba wananchi wamechoshwa mno na janga la ufisadi uliobadilika na kuwa utamaduni wa watendaji wa Serikali ya CCM.
Kitendo cha afisa wa umma TRA kukutwa na pesa taslimu nyumbani kwake 7bilioni ni ishara mbaya sana. Huyu ni mtumishi wa umma akiwa chini ya wizara ya fedha inayoongozwa na Dk. Mwigulu Nchemba. Hii ni ishara kwamba walioficha fedha majumbani kama huyu ni wengi sana.
Haya yanatokea katikati ya umma unaoshambuliwa na umasikini uliotopea. Hizi ni fedha zao past na shake yoyote. Hii ni aibu kwa waziri mwenye dhamana ambaye ni mteule wa Rais. Si kwamba umma mpana hususan vijana hawayaoni haya. Lakini wanasema huku vijiweni kwamba kama huwezi kumzuia mbwa wako kukera wapita njia na kuhatarisha maisha yao basi watashughulika na mwenye mbwa anayempa kiburi mbwa wake. Hiki ndicho kinachotokea Kenya.
Ni suala la muda tu lakini vijana wamechoka kuona na kusikia matukio ya ufisadi uliopindukia hapa Tanzania. Hata hao polisi tegemeo kuwalinda nao ni choka mbaya na silaha mabegani. Tuendelee kunywa mtori nyama tutazikuta chini zikiwa zimechacha zisizolika.
Ni wakati wa kila kijana kuamka na kutafakari mustakabali wa nchi yake. Ni wakati wa vijana kujadiliana na kuhimizana kuona kwamba hatima ya maisha yao sasa yako mikononi mwao na si Rais Samia, Serikali, au CCM.