Samia alijitengenezea tatizo mwenyewe bila kujua, sasa hilo tatizo alilojitengenezea ndio linaanza kumtafuna, amesababisha aonekane anawakilisha kikundi cha mafisadi wachache wanaoitafuna nchi kwa dharau.
Alipoingia madarakani akaanza kuwaondoa waliokuwa watendaji wa Magufuli, huku akiwarudisha wale waliotemwa na Magufuli. Sidhani kama alipata muda wa kutosha kujua sababu zilizomfanya Magufuli awatose kwenye serikali yake.
Binafsi, naona aliamua kufanya vile akiamini atakuwa salama kwa kuzungukwa na kundi la marafiki zake, au watoto wao, akasahau baadhi ya hao wana kashfa zinazowazonga muda wote, huku utendaji wao ukiwa mbovu.
Sasa ameanza kuvuna alichopanda, ameanza kazi ya kuwaombea msamaha kwa viburi vyao, kwa kujua au kutokujua, ametengeneza picha kwa watanzania wanaona vile anavyokibeba kikundi cha wachache.
Nao wanakikundi kwa kutambua udhaifu wake, wanachofanya ni kumsifia 24 hours ili kujihakikishia usalama wa ofisi zao, wala sio kwa utendaji wao serikalini ambao kwa kiasi kikubwa hauridhishi.