mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 19,981
- 35,581
Kutoka kwenye clip fupi ya mtanzania mwenzetu Bwana Saimon Sirikwa anayefanya kazi kwenye sector ya utalii nimejifunza mambo machache ambayo nadhani tunayapuuzia au hatutaoni japo ni muhimu
Kwanza, serikali haijawatumia kabisa hili kundi la hawa watu wanaokutana na watalii moja kwa moja na kuongea nao. Hawa watu ni muhimu kuliko tunavyodhani
Pili, hakuna elimu au maelekezo maalumu waliyonayo au wanayopatiwa na serikali yatakayowasaidia kutoa huduma yenye vigezo vinavyotakiwa kwa wageni wanaokutana nao. Wanajiongeza wenyewe kwa njaa zao tuu
Tatu, hakuna mifumo ya kufuatilia na kuhakikisha kwamba hili kundi linafanya kile kinachotakiwa, kilicho sahihi au wanatoa huduma inavyotakiwa wanapokuwa na watalii. Yaani hawa wanaweza hata kutumika vibaya na watu wenye nia mbaya
Nne, hakuna mfumo wa kupata feedback toka kwa hili kundi, feedback zitakazosaidia kuongeza thamani kwenye sekta ya utalii. Tukumbuke Feedback kutoka field ni muhimu kuliko zile tunazopokea tukiwa kwenye AC maofisini
Tano, hili kundi ni kubwa na linafanya kazi kubwa pia tena sana lakini halipewi Ile nafasi wala thamani kwenye Ile chain nzima ya utalii. Tunaweza kuwatumia hawa watu ku add value kwenye utalii wetu kirahisi sana kuliko tunavyowachukulia.
Mnaweza kumsikiliza bwana Saimon zaidi hapa kupata mengine ya muhimu
Login • Instagram
Ni muhimu sasa wakatazamwa na kupewa seminars, miongozo na hata motisha. Tunatumia makundi mbalimbali kukuza sekta ya utalii lakini hili kundi likipewa elimu rasmi, mbinu na motisha kunaweza kuwa na faida kubwa pia kwa nchi yetu
Nawatakia mapumziko mema ya MeiMosi