Asalaam Aleykum Wasomaji wa JFs.
Kwanza nitoe pongezi za awali kwa Mh Samia Suluhu kwa namna alivyoanza kuongoza nchi yetu ambayo kwa namna moja ama nyingine ilikuwa unapoteza mwelekeo chini ya mtangulizi wake hayati Baba Dr John Josefu Magufuli.
Nasema pongezi za awali kwa kuwa ameonesha hatua za mwanzo za kuleta mabadiliko ktk utendaji kazi, kwa kuwa ni mapema sana kujihakikishia kile anachofanya sasa kama kitaendelea kwa misingi hii hii.
Tukirudi nyuma kidogo wakati wa kampeni za uchaguzi nyote ni mashahidi kuwa Mh Tundu Lissu aliendesha kampeni zake mwaka jana 2020 huku akiwa hana chombo chochote cha habari cha nchi hii hasa mashrika makubwa na ya serikali kutangaza habari zake. Hata hivyo mikutano yake ilizizima kwa wingi wa watanzania walionogewa na kauli mbiu ya Uhuru, haki, demokrasia na maendeleo ya watu. Mada hii ilipendeza sana. Aliifafanua kwa umahiri na umakini mkubwa hata mwananchi wa kawaida wa hali ya chini kabisa akaielewa. Hali ile iliwashangaza wengi hata wapinzani wake wa kisiasa.
Baada ya kuchukua Kiti cha Urais Mh Samia Suluhu Hasani tar 19 Machi 2021 kwa mujibu wa katiba ya nchi alifanya Hotuba ya kwanza bungeni Tar 22 april 2021. Moja ya mambo aliyosistiza ni pamoja na kudumisha uhuru, haki na kuleta maendeleo kwa watu.
Matukio yaliyodhihirisha dhamira yake yalitokea kama ifuatavyo.
1. Siku ya kupokea ripoti ya CAG alisema na kuwaasa TRA kuhakikisha wanakusanya kodi ya haki na kuacha kubambikia makodi ya uongo na kweli. Hapa wahanga ikiwa ni wafanya biashara waliikuwa hawaungi mkono sera za hayati.
2. Siku hiyo hiyo Ripoti ya CAG Mh Samia Suluhu aliagiza DPP na Mahakama kuhakikisha watu wenye kesi zisizo na kichwa wala miguu zenye dosari za kubambikiza ziachwe mara moja au zifanyiwe mchakato na kuisha haraka.
3. Wakti akiwa Bungeni aliagiza wabunge waachane na vihoja na viroja vya kupayuka payuka na kudemka na badala yake wafanye kazi kuisimamia serikali ili kuwaletea maendeleo watu.
4. Samia amesikika akikiri kuwa mifukoni mwa wananchi hakuna pesa na dhamira yake ni kuhakikisha anakuza njia za uchumi.
5. Mh Samia Suluhu amesikika jana ktk kikao chake na wazee wa Dar es salaam kuwa atahakikisha nchi inakuwa ya kidemikrasia na kwamba mtu akipata haki basi haki yake aipate na si vinginevyo( kupora na kuiba kura byebye)
6. Lakini si hivyo tu kauli na matendo yake yanaashiria nia njema aliyonayo kurekebisha makosa yaliyofanywa na mtangulizi wake.
7. Leo tumepokea taarida ya kufurahisha kwamba BASATA wamesimamisha utekelezaji wa kanuni za kibabe na kikabaila zilizokuwa zinadidimiza uhuru wa maoni kwa njia ya muziki na tungo mbali mbali kwa wasanii. haya si mambo ya kuacha yapite bila kuyapongeza.
8. Kubwa zaidi Ktk kulinda haki ya kuishi na afya kwa watanzania, jambo amabalo mtangulizi wake alipinga na kwa nguvu zote, leo Mh Rais ameonekana na viongozi mbali mbali wa kitaifa wakiwa na Full Face mask kujikinga na Covid 19.
Hii inanipa fikra kuwa kumbe Mh Rais alivutiwa na Sera za TL wakati wa kampeni sasa amepata fursa ya kutuongoza na anaitekeleza kwa 100%.
wale mliotoa mapovu na kutukana kwamba Chadema sisi ndio tunaoeneza uvumi wa Covid-19 mpaka mishipa ya shingo ikawatoka mnasemaje leo mnapoona Safu nzima ya Ikulu na Waziri Mkuu wako ktk mwonekano huu??
Rais Mstaaf JK aliwahi kusema .....Zakuambiwa....Changanya na zako. Kweli Mama anachanganya