Rais Samia Suluhu kuzungumza na Wazee wa Dar es Salaam Ijumaa Mei 7, 2021

Rais Samia Suluhu kuzungumza na Wazee wa Dar es Salaam Ijumaa Mei 7, 2021

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho Ijumaa Mei 7, 2021 anatarajia kuzungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika mkutano utakaofanyika ukumbi wa Mlimani City na kuhusisha wazee takribani 900.

MATAGA andaeni mapovu tena maana Mama anaenda kuifungua nchi.
Hivi wazee huwa wapo Dar pekee?
 
Safi sana, Mheshimiwa rais, Sisi wazee wa DSM tunaomba Jiji Letu la Dar'es salaam ulirudishe liwe moja ila Uunde halmashauri moja ya Jiji kutoka wilaya Zote.

Haiwezekani Msasani, Mwenge, Kawe kusiwe jiji eti jiji liishie posta tu.

Kufuata model ya mwanza eti Halmashauri ya jiji iundwe na wilaya mbili tu haimake sense kwa DSM kwa sababu Mwanza ni kubwa ina rural area kubwa, kwa hiyo ni sahihi Jiji kuwa kwenye wilaya hizo mbili, Lakini DSM yetu kwa eneo ni Ndogo kwa hiyo Wilaya zote zinatosha na zina vigezo vya kuwa jiji moja.
 
Hiyo spika wenu hakosi kutunga hata Deni ili kumchafua mtu. Bado mnamuamini?
 
...Natumai mzee Mohamed Said (member wa JF) nae atakuwa miongoni mwao...kila la kheri wazee wa Dar-es Salaam, kama ikimpendeza akimalizana na hao wa Dar Es-salaam anongee pia na wazee wa Dodoma!
 
CCM pekee huwezi kuona chama kingine amealikwa, utakuta akina Shibuda, Mrema na wengine
Asante mkuu. Nadhani kama wa vyama vingine nao wakialikwa litakuwa jambo la afya sana kwa ustawi wa siasa za Tanzania.
 
Safi sana Mheshimiwa Rais hawa wazee hata Baba wa Taifa aliwaheshimu sana.
 
Back
Top Bottom