Rais Samia Suluhu tumia madaraka yako mwachie huru Mbowe

Rais Samia Suluhu tumia madaraka yako mwachie huru Mbowe

Mbowe sio malaika ni Gaidi lililo jificha kwenye kichaka cha siasa.
Serikali haiwezi kuyumbishwa na Gaidi, Jeshi la Polisi na vyombo vyote vya ulinzi vipo imara.
Mbowe hawezi kuwa Juu ya sheria za Tanzania.
Mbowe ni Raia kama walivyo raia wengine wahalifu waliopo mahabusu.
Kama Mbowe ataachiwa kwa shinikinikizo lolote lile basi ni bora wahalifu wote waliopo jela nao waachiwe huru jambo ambalo halitowezekana
Hujui ulisemalo! Wewe sio judge Wala DPP ambao ndio wanaotakiwa kisheria kutoa maamuzi baada ya kusikiliza pande zote zinazotuhumiana!
Usijipe mamlaka usiyokuwa nayo kwani yatakupa stress zisizo na maana! Tafuta pesa ujitunze, ya Mbowe yatakupa mshituko wa moyo kwani mwezi wa tisa atakuwa mtaani!
 
Unamtaka Rais atumie mamlaka 'aliyonayo' kumwachilia Mbowe. Ukweli ni kwamba kwa mujibu wa Katiba, Rais hana mamlaka ya kufanya hivyo kwa kuwa shauri liko mahakamani. Atakuwa anaingilia mamlaka nyingine ambako ni kukiuka Katiba. Ni pale tu mahakama ikifikia uamuzi, kwa mfano kumfunga mshitakiwa, hapo ndipo Rais anaweza kuingilia kati na kumpunguzia adhabu au kumsamehe kabisa. Kumbuka hata watu wanaohukumiwa kunyongwa, Rais budi atie sahihi ili hukumu hiyo itekelezwe.
Soma vizuri. Kwa kutumia ofisi zilizopo kikatiba. Utaelewa namaanisha nini kama una akili za kujifunza.
 
Unaamini kuondoka kwa Mbowe (kwa namna yoyote ile) knaweza kuwapa nafuu CCM?Mimi sidhani hivyo!! Nkiangalia mtu kama Heche awe ndiye Mwenyekiti naamini hali itakuw atofauti sana.
Hakuna aliyejua kuwa mtu anaweza kuua askari "cold blood" na akatamba barabarani hapa Tanzania lakini imetokea.Binafsi naomba kama Mbowe ana hatia afungwe hata kunyongwa lakini ithibitike wazi!
Sijui wapi nimesema hivyo mimi siyo CCM, usiandike kabla ya kuelewa kitu.
 
Kwa heshima kubwa Mheshimiwa Rais SSH nawasilisha kwako ombi maalum kwamba, kwa mamlaka uliyo nayo na kwa kutumia ofisi zilizopo kikatiba mwachie huru Ndg. FREEMA AIKAEL MBOWE.

Hoja yangu naijenga katika misingi ya kuliponya Taifa na majeraha ya chuki na kutokuelewana.

Mhe. Rais nakariri maelezo ya ZZK ya hivi majuzi kuwa mashtaka ya Mbowe hayana maslahi kwa Taifa.

Mhe. Rais. Nakuomba sana na naomba kuwasilisha. Naamini kwa dhati utazingatia ombi hili maalum kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
PHD yako ni ya vitu gani mkuu PhD?
Kwani hujawahi kusikia uwepo wa wafungwa wa kisiasa?

'Maza Mizinguo pamoja na kutokuwa na PhD kama yako, anaelewa vizuri sana kwamba kesi inayomkabili Mbowe haina mashiko.
 
Kwa heshima kubwa Mheshimiwa Rais SSH nawasilisha kwako ombi maalum kwamba, kwa mamlaka uliyo nayo na kwa kutumia ofisi zilizopo kikatiba mwachie huru Ndg. FREEMA AIKAEL MBOWE.

Hoja yangu naijenga katika misingi ya kuliponya Taifa na majeraha ya chuki na kutokuelewana.

Mhe. Rais nakariri maelezo ya ZZK ya hivi majuzi kuwa mashtaka ya Mbowe hayana maslahi kwa Taifa.

Mhe. Rais. Nakuomba sana na naomba kuwasilisha. Naamini kwa dhati utazingatia ombi hili maalum kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
Kibatala akale wapi?
 
Mfa maji haishi kutapatapa.
aache kesi ya msingi ingurume kama kweli yeye sio Gaidi, kwa nn anataka kesi ifutwe hata kabla ngoma haijachezwa?! anafahamu uovu wake wote utawekwa hadharani ni wananchi wataijua tabia yake ovu dhidi ya nchi hii.
Unataka afutiwe kesi ili wananchi na dunia isifahamu uovu wake utakao anikwa mahakamani?!
 
Inawezek
Huwezi kuachia huru mtu ambaye haja hukumiwa kisheria. Tatizo ni waache kuweka kesi za kijinga kijinga za siasa
Inawezekana kabisa kwa kufutiwa mashitaka na ofisi ya DPP ambaye ni mteule wa Rais.
 
Kwa hiyo unataka aingilie uhuru wa mahakama ?
Shauri ni batili tangu mwanzo, hata tusio wanasheria tunajua mwanzo na hatima ya dhuluma na uonevu huu. Tunaishi kinafiki H.E Samia Mara kadhaa kasihi polisi na ofisi DPP, kuondoa mashauri yenye utata. Kumkomoa Mbowe kwa faida ya Nani? Chuki inayojengwa kuziba watu kudai Haki zao za kidemocrasia , binadamu atatafuta mbinu mbadala.RIP Jemedari Hamza.
 
Kati ya kitu ambacho hua nawashangaa waTanzani katika kushabikia upinzani ni kudhani viongozi wa UPINZANI ni Malaika wasio na dhambi

Mnapotoka pakubwa sana
 
Back
Top Bottom