Rais Samia Suluhu tupunguzie mateso, tumecheleweshwa sana ajira mpya

Ignorant! hayaja kukuta ww..
 
Watanzania inabidi tusisubiri ajira za serikali. Tufungue miradi zaidi mpaka leo hii kuna upungufu wa ngano, sukari, mafuta lakini unataka upate ualimu ambao pesa yenyewe ni ndogo badala ya kuwekeza.
Biashara sio hobby au professional kusema utafanya na kusurvive kirahisi.....

Si kila mtu kazaliwa kufanya biashara....
 
Juzi hapa niliandika uzi na kupendekeza kuwa muda umefika sasa kwa Tanzania tuanze kutumia mfumo wa malipo ya lisaa kwa wafanyakazi.....

Tukitumia huu mfumo kutakuwa na faida nyingi kuliko hasara.

1. Masaa ya kazi au kukaa kazini yatapungua. Kwa wastani mfanyakazi wa serikali huwa anatumia siku nzima kazini. Na hii humfanya ndani ya muda mfupi kuwa demoralized na kuboreka hatimae kukosa ufanisi kiutendaji.

Kwa mfano tukiweka mkataba kuwa mfanyakazi atafanya masaa wastani ni matano kwa siku au sita hii itampa nafasi ya kufanya mambo yake mengine na hata kufanya kazi na kampuni nyingine aidha za serikali au binafsi na kujiongezea ujira na kipato kizuri.

2. Kupungua kwa masaa ya kazi kutaweka gepu la uhitaji wa wafanyakazi, mfano, shirika likiwa na mtendaji ataeingia kazini kuanzia saa kumi na mbili then ikifika saa tano amemaliza shift yake anatoka kazini. Then kuanzia hiyo saa tano kwenda mbele kutakuwa na vacancy au nafasi itayohitaji mtu mwingine ashike shift ya saa tano hadi kumi na moja jioni kutimiza masaa sita mengine. Kutokea kumi na moja jioni masaa sita mengine ni hadi tano usiku, kutokea tano usiku hapo kama kampuni inakesha ni hadi kumi alfajiri, mzunguko unaendelea hivyo.

Hapo tayari kuna gape na wafanyakazi wangapi unaona......?!

Sasa zidisha mara idadi ya ajira zilizopo sasa..... Hivi tutatengeneza ajira ngapi na watu wangapi watasaidiwa kupata ajira ......?!

3. Ufanisi utaongezeka..... Mtu anae kaa ofisini masaa kumi na kitu siku nzima na ambae anakaa nusu au robo siku wanautendaji wa tofauti sana sababu ya kuwa na muda mchache wa kufocus na kazi.... Hii inawapa watu ari ya kuchapa kazi sana..... Na kuwa na hamu ya kuja kazini na kutopoteza muda wakiwa kazini sababu masaa yao yanatathiminiwa na kutazamwa namna wanazalisha....
 
Km kuna awamu vijana wamechezea bakora za maisha basi n awamu ya tano. Kijana umenyimwa ajira bas ukisema ngoj nijiajiri niombe mkopo kwa ndugu zangu watumishi wa umma nao wanakwambia hawana sent mana mishahara haijaongezwa mwaka wa 6 sasa hvo n hawawez ata ku top up mkopo, ukisema bas aya ngoja ukamkope mfanyabishar unaemjua akupe ata mtaji nae anajuta analia na kodi balaa hana mia... Ukisema ngoj usubirie labd mbunge wako atakutetea Bungeni anakwambia kijana kajiajiri, ukisem aya ngoj usikilize wataalam wanasemaj juu ya hili janga wanakwambia nenden veta wote tuwe mafund umeme, yan hii awamu ya tano ctaisahau kwa ukatili wake kwa vijana.
 
yataisha ASAP Mama Samia yuko Vizuri
 
Imeunganishwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana wewe ni msukuma ambaye mmeajiriwa kwa ule mpango wa rise Sukuma, mpango ambao ulikuwa unasubiri wasukuma wajilundike mtaani, then atoe ajira kuwachukua wote. Namchukia huyu shujaa wa Africa na dunia kwa ujumla.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo hili la ajira hususani kwa walimu tunalikuza sana kuliko uhalisia,kuna walimu kibao wamejazana sehemu za mijini na kwenye majiji na bado watazidi kuongezeka na gia yao siku hizi ni kuwa wanafuata huduma za matibabu mijini, wanajitengenezea ugonjwa feki.Ninao mfano mdogo wa walimu watatu wa history jijini mwanza ambao wanafundisha kidato kimoja yaani wamegawana topic!!!! NINACHOKIONA HAPA NI POOR DISTRIBUTION OF MAN POWER NA SIO UHABA hususani kwenye sekta ya elimu sijajua kwa sekta nyingine.Serikali iwahamishe walimu kutoka mijini ni wengi na wapelekwe kwenye upungufu.
 
Na sie tunasubiri increment zetu na Madaraja.Mheshimiwa kazi anayo.
 
Kipato 300000 kwa mwezi,HESLB-15% income tax,NSSF-10%,
Bado wategemezi,n.k,

Utaweza kuishi ?
Kama nimeweza kuishi bila huo mshahara kabisa, nikiupata nitaishi pia, usitake makuu kuliko uwezo wako mkuu!
Halafu hayo makato na hiyo 300k, ni kwa mtazamo wako tu, ila sio malipo kwa ngazi ya shahada (ualimu)
 
Na kwenye masomo ya sayansi napo ikoje, wanagawana topic pia!? Uhaba upo kwa namna flani, watuajiri tu!
 
Kipato 300000 kwa mwezi,HESLB-15% income tax,NSSF-10%,
Bado wategemezi,n.k,

Utaweza kuishi ?
Ni kweli ni unyonge lakini usikuze mambo tofauti na uhalisia, mshahara wa laki tatu ni kuwa level gani ya elimu?!, Tusiongee pasipo uhalisia, serikali ililiona hili ndo maana watu wa Diploma veta na certificate hawapewi mkopo wa bodi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…