Rais Samia Suluhu umeanza kuwa Dikteta mapema kuliko hayati John Pombe Magufuli

Kama kawa, usiombe ukutane na mchawi mwanamke. Hawana huruma hakika. Ila mama amebow kwa wahafidhina walioko ndani ya CCM kwani hajiamini naona. Nina hakika yeye kama yeye angeyaka utawala wa sheria ila ndani ya CCM kuna watu wameonja nyama ya mtu hawawezi kuacha.
 
Si kweli kwamba nimekutusi. Nimekutukana tusi gani? Mimi si kijana na situkani mtu. Nakuheshimu wewe lakini nashutumu unachosimamia.
 
Hayati Magufuli alisema analeta Maendeleo. Leo hakuna anayemkumbuka Magufuli na habari zake za Maendeleo bali anakumbukwa kwa kuminya na kukandamiza haki za Raia.
Maoni na mtazamo wako binafsi usiufanye kuwa maoni na mtazamo wa watanzania wote. Watu wenye mitazamo finyu kama wewe ndo wanaweza kuwa na generalizesheni za kitoto hivi.
 
Maoni na mtazamo wako binafsi usiufanye kuwa maoni na mtazamo wa watanzania wote. Watu wenye mitazamo finyu kama wewe ndo wanaweza kuwa na generalizesheni za kitoto hivi.
Lipa kodi ya simu, Huoni mbele
Hujui lolote

Ulienda shule kuokoteza maneno ya kiingereza
 
Hivi kwa nini mnapenda kusema uongo? Au mnadhani watu wote ni malimbukeni kama nyinyi?

Hakuna nchi yenye demokrasia kamili, kuanzia Marekani mpaka India, inayopanhia raia zake kipindi au mahali pa kufanya siasa. Marekani ndio kabisa. Tangu Trump ashindwe kwenye uchaguzi amekuwa akifanya kampeni ya kutaka matokeo yabatilishwe. Hata miezi sita haijapita toka Rais mpya aapishwe tayari anafanya mikutano ya hadhara akidai kuwa Biden alimuibia ushindi na si Rais wa halali.

Acolytes wake wanazunguka nchi nzima kutaka kubadilisha taratibu za upigaji kura ili kuhakikisha democrats hawatakuja kushinda tena. Wanafanya mikutano ya hadhara, wanafanya ya ndani (town hall meetings) na wanatumia media kikamilifu kuendeleza ajenda zao bila kubughudhiwa.

Democrats nao wanajibu mapigo. Wanaandaa maandamano na mikutano kuwapinga wasio mtakia mema Biden. Na kote huko hamna kiongozi (Rais au Gavana) anae agiza vyombo vya usalama viwashughulikie.

Katika demokrasi inayojitambua, kampeni za uchaguzi ujao zinaanza pale matokeo ya uchaguzi wa sasa yanapotangazwa. Haya mambo ya kumpangia mpinzani wako namna ya yeye kufanya siasa, muda wa kufanya siasa, mahali pa kufanya siasa na hata maneno atakayosema si ya demokrasi bali ni ya pseudo demokrasi!

Tunaona charade ya upinzani kuzuiwa kufanya shughuli zao wakati chama tawala wana carte blanche ya kufanya watakalo.

Leo wapinzani ambao ni raia wa nchi hii wanazuiwa kujadili na kuichambua Katiba halafu bado mnataka tuamini kuwa ni sehemu ya demokrasia? Watu wanakamatwa hotelini ili kuwazuia kuhudhuria kikao halali chini ya sheria na bado mnadai ni sehemu ya demokrasia? Leo kiongozi wa upinzani anaambiwa kuwa anatakiwa kufahamisha polisi akiingia kwenye mji mwingine kufanya shughuli za chama chake na mnadai hiyo ni demokrasi? Msitufanye wajinga.

Amandla...
 
Tumia Akili au Umetolewa Ubongo Katiba Mbovu iliyopo inaruhusu Mikutano Yeye Anazuia kwa Katiba Gani Naona Wamekutoa Ubongo
 
Yaaani mnampiga mkwala rais kisha mmataka akae kimya kuwafurahisha daaah akili matope si mlisema mtatumia wembe ule ule tumieni sasa.
Bunduki na mabomu yao ni maandishi yao humu jukwaani.

Silaha zenye nguvu mwisho mlangoni kurudi ilipo simu au laptop.
 
Ukishaona Rais fulani wa Afrika marafiki zake pamoja na wahisani wake wakuu ni Burundi na Zimbabwe jua kuwa hamna Rais humo

 
Chama chochote kishike dola mambo ni hayo hayo wacha Samia akupigeni spana hamtaki kumuheshimu na mnamzonga,ndio Kwanza miezi minne mnampanda kichwani
 
Ebu tutajie nchi moja tu duniani baada ya uchaguzi na serikali kutangazwa vyama vya siasa vinaendelea kufanya mikutano ya hadhara? Ata hiyo mikutano mkiruhusiwa mnazungumza Nini zaidi ya kueneza chuki? Mmesharuhusiwa kufanya mikutano ya ndani fanyeni matangazo na watu watakuja..magu nilikuwa simpendi lakini kwa hili nilimuunga mkono maaana haiwezekani mtu anafanya kazi wengine wanaangaika kufanya mikutano ya kuharibu....
 
Imeisha hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…